Posti hii inahusu zaidi dalili la jeraha la kawaida kwenye ubongo, jeraha la kawaida utokea kwa sababu mbalimbali kama vile kupata ajali na kugongwa na kitu chochote kichwani,
Dalili za jeraha la kawaida kwenye ubongo.
1. Kuchanganyikiwa au kupoteza fahamu
Ni dalili ambayo ujitokeza hasa kama mtu amepatwa na jeraha kwenye ubongo hali hii utofautiana na jeraha kali kwa sababu kupoteza fahamu na kuchanganyikiwa uwa ndani ya masaa ishilini na manne, na baadae mgonjwa uwa kawaida Ila uhisi maumivu katika kichwa kwa hiyo huduma anayopaswa kupewa na dawa ya maumivu na kuendelea kupumzika na hali huwa kama kawaida .
2.Kutokumbuka kilichotokea.
Mgonjwa wa jeraha la kawaida hakumbuki kilichotokea kwa sababu pengine anakuwa amepoteza kabisa fahamu kwa hiyo mara nyingi ukumbuka lile tukio la mwanzoni ambalo utokea kwa hiyo mgonjwa akizinduka mara nyingi uuliza Niko wapi na kwa sababu gani kwa hiyo anapaswa kupewa majibu na kuulizia jinsi anavyojisikia na kwa wakati huu anapaswa kupewa mda wa kupumzika na hapaswi kuulizwa maswali mengi kwa sababu anaweza kugongwa na kichwa.
3.Kichwa kuuma kizunguzungu na uchovu.
Kwa mgonjwa aliyepata jeraha la kawaida uhisi maumivu ya kichwa, kizunguzungu na uchovu hii ni kwa sababu ya mshutuko ambao utokea kwenye ubongo kwa hiyo mgonjwa anapaswa kupewa dawa ya maumivu Ili kupunguza maumivu ya kichwa na pia hapaswi kutembea tembea kwa sababu ya kizunguzungu na Akitaka kwenda sehemu inabidi aende na mtu Ili kuepuka kudondoka na kusababisha matatizo mengine na mgonjwa Upata uchovu kwa sababu pengine wakati wa ajali Kuna sehemu alijikwaruza na hali hii utulia ndani ya masaa ishilini na manne.
4. Kutoona vizuri au kuona maruweruwe.
Mgonjwa wa majeraha ya kawaida mara nyingi huwa haoni vizuri na kwa wakati mwingine uona maruweruwe kwa sababu ya mshutuko kwenye ubongo ambao upelekea nevu za kwenye macho na kutenguka kidogo na baadae hali hii utulia, kwa hiyo mgonjwa wa namna hii anapaswa kutumia hata kusinzia kabisa na hatimaye hali huwa kawaida.
5. Kichefuchefu na kutapika.
Mgonjwa mwenye majeraha ya kawaida uhisi kichefuchefu na kutapika kwa mda hali hii utokea kwa sababu ya mshutuko ambao uingiliana na mfumo wa umengenywaji wa chakula na kwa hiyo hali hii udumu ndani ya masaa ishilini na manne. Kwa hiyo mgonjwa anapaswa kufanyiwa huduma zote za mtu Mwenye Kichefuchefu kama vile kula vyakula vigumu vigumu mfano mkate na chapati na pia kula kidogo kidogo kwa mda mrefu na pia kukaa wima.
6.kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa wagonjwa wenye majeraha ya kawaida kwenye ubongo dalili zao pengine zinaweza kuogopesha wahudumu wa mgonjwa lakini kwa kawaida udumu ndani ya masaa ishilini na manne na mda unaniofuata mgonjwa huwa kawaida na kuendelea na matibabu hasa kupunguza maumivu.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupambana na saratani
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi magonjwa ya moyo, kwa kawaida watu wakisikia habari za magonjwa ya moyo huwa hawaelewi yanakuwaje kuwaje, Leo nataka niwafahamishe kuhusu magonjwa ya moyo na sehemu mbalimbali zinazoathirika.
Soma Zaidi...kovu (Fibrosis) ya ini inayosababishwa na aina nyingi za magonjwa na hali ya ini, kama vile Homa ya Ini na unywaji pombe kupita kiasi. Ini hufanya kazi kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na kuondoa vitu vyenye madhara katika mwili wako, kusafisha damu yako
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea sababu za maumivu ya tumbo kitovu i
Soma Zaidi...mm nahis miguu pamoja na mikono kuishiwa nguvu ni mgongo kuuma ni dalili za ugonjwa gan ?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kufanya figo kuharibika.hili ni janga ambalo linawakumba Watu wengi siku hizi na kusababisha kupoteza maisha kwa wagonjwa wa figo hasa hasa kwa wale ambao hawana uwezo wa kulipia hela ya kusafishia figo.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na Magonjwa yanayosababisha madhara kwenye mapafu na kitaalamu hujulikana Ugonjwa wa Acute Respiratory Distress Syndrome (ARDS) hutokea wakati Majimaji yanapojaa kwenye vifuko vidogo vya hewa nyororo (alveoli) kwenye mapafu
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa vipele kwenye midomo na sehemu za siri .Ni ugonjwa ambao kwa kitaalamu huitwa herpes zoster
Soma Zaidi...