Kukosa Ute wakati wa tendo la ndoa.

Posti hii inahusu zaidi sababu za kukosa Ute wakati wa tendo la ndoa,ni Dalili ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha estrogen kwenye mwili ukilinganisha na homoni ya projestoren.

Kukosa Ute wakati wa tendo la ndoa.

1. Kama tulivyotangulia kusema kwamba kukosa Ute wakati wa tendo la ndoa ni Dalili ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha estrogen kuliko progesterone ila kuna dalili nyingine ambazo zinaweza kutokea kwa sababu ya kukosa Ute wakati wa kujamiiana ni kama ifuatavyo.

 

2. Kukosa hisia na hamu ya kufanya mapenzi.

Kuna wakati mwingine kunakuwepo hali ya mtu kukosa hisia kabisa na hamu ya kufanya mapenzi inaisha hali ambayo inasababisha wanafamilia kupata shida kwa sababu ya mmoja wapo kushindwa kutimiza wajibu kwa mwingine, kama ikitokea kwa familia ni kitendo cha kukaa na kuongea ili kuweza kupata suluhisho na kupata matibabu mapema.

 

2. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Kuna wakati mwingine  kunakuwepo na malalamiko wakati wa kufanya tendo la ndoa kwa sababu ya kuwepo kwa maumivu makali yanayosababishwa na michubuko ya maumivu kwa sababu ya msuguano unaosababishwa na uume wakati wa tendo la ndoa, hali hii ikitokea usababisha mmoja kuchukia tendo la ndoa kwa sababu ya kuwepo kwa misuguano wakati wa tendo.

 

3.uwepo kwa damu baada ya tendo la ndoa.

Kwa sababu ya kuwepo kwa misuguano mikali wakati wa tendo la ndoa usababisha kutokwa na damu baada ya tendo hali hii inaweza kuwepo kwa mda wa siku moja au mbili kwa sababu ya kuwepo kwa misuguano.

 

4. Hedhi kukosa mpangilio maalumu.

Kwa sababu ya kukosa Ute ina maana kwamba kuna homoni ambayo inazalisha Ute kupungua hata hivyo na katika sehemu mbalimbali za via vya uzazi usababisha hedhi kukosa mpangilio.

 

5. Kwa sababu ya kuwepo kwa mabadiliko mbalimbali kwenye mwili, tatizo hili mara nyingi uwapata wale wanaotumia sana au waliowahi kutumia uzazi wa mpango kwa matumizi ya P2, vitanzi, sindano, vidonge na aina yoyote ya uzazi wa mpango isipokuwa za asili.

 

6. Kwa hiyo hali hiyo ikitokea kwa familia ni vizuri kabisa kutafuta matibabu mapema ili kuweza kuepuka matatizo ya kuchepuka kwenye familia kwa sababu ya mmoja kati ya wana familia hana kabisa hamu ya mapenzi na mwingine anayo.

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 4509

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Maji ya Amniotic

Posti hii inahusu zaidi maji ya Amniotic ni maji ambayo uzunguka mtoto na kufanya kazi mbalimbali kama ifuayavyo.

Soma Zaidi...
Umuhimu wa kunyonyesha mtoto

Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kunyonyesha mtoto, kunyonyesha ni kitendo cha Mama kutumia titi lake Ili kuweza kumpatia mtoto lishe kwa kipindi chote ambacho Mama upaswa kutumia kwa kunyonyesha mtoto wake kwa hiyo Kuna faida ambazo mama uzipata kutoka

Soma Zaidi...
Madhara ya kufanya tendo la ndoa na mwanamke akiwa katika siku zake.

Tendo la ndoa wakati wa siku za hedhi ni halia mbayo jamii nying zinakataza. Katika vitabu vya dini pia haviruhusu, hata ki saikolojia utaona kuwa sio jambo jema. Hata hivyo hapa ninakuletea madhara yake kiafya

Soma Zaidi...
Njia za kuzuia mimba zisiharibike.

Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuzuia mimba zisiharibike, kwa sababu kila mama anayebeba mimba anategemea kupata mtoto kwa hiyo na sisi hamu yetu ni kuhakikisha kwamba mtoto anazaliwa kwa kuzuia mimba kuharibik

Soma Zaidi...
siku za kupata mimba

Makala hii inakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata mimba na dalili za siku hizo.

Soma Zaidi...
Tiba ya awali kwa mwanamke mwenye changamoto ya PID

Posti hii inahusu zaidi tiba ya awali kwa mwanamke mwenye changamoto ya PID, tunaita tiba ya awali kwa sababu baada ya kupima na kugunduliwa kwamba una tatizo au changamoto ya PID ni vizuri kutumia tiba hiii baadae ndipo utumie dawa.

Soma Zaidi...
Nini husababisha maumivu ya uume

Kama uume wako unauma ama unahisi kuwa unaunguza ama kuchoma choma, post hii imekuandalia somo hili.

Soma Zaidi...
Mda wa kufanya tendo la ndoa baada ya kujifungua

Posti hii inahusu zaidi mda ambao mama anapaswa kukaa bila kufanya tendo la ndoa mara tu baada ya kujifungua.

Soma Zaidi...