image

Dalili za kujifungua hatua kwa hatua

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za kujifungua hatua kwa hatua

DALILI ZA KUJIFUNGUWA HATUA KWA HATUWA:

Ni ndoto za wanawake wengi siku moja abebe ujauzito, azae mtoto kisha aitwe mama. Haswa hata wanaume hupendelea hivyo. Ila mwanamke anapofikia kujifunguwa hapa ndipo kizaazaa huonekana. Sasa makala hii itakwenda kukueleza dalili za kujifunguwa.

Daliili za kukaribia kujifunguwa kwa siku kadhaa1.Maumivu ya nyonga kuongezeka2.Uchovu kuongezeka3.Kutoa damu yenye utelezi4.Viungo kuachia5.Njia ya kuzalia kutanuka zaidi.6.Maumivu ya tumbo kuongezeka.7.Maumivu ya tumbi na kutungwa.8.Kuharisha9.Maumivu ya mgongo kuongezeka

 

Dalili za kujifunguwa kwa masaa machache:1.Mikazo ya tumbo inayotokea katika muda maalumu2.Kutokwa na damu yenye utelezi3.Kutokwa na utelezi kwa wingi4.Njia kuachia zaidi5.Mtoto kushuka karibu na njia ya kutokea.

 

Uchungu wa kujifunguwa:Uchungu wa kujifunguwa hauwezi kuelezeka kwa maandishi machache haya. Hata hivyo kuna machache naweza kukueleza ijapokuwa huwenda usiwe uhalisia. Kujifunguwa kunapitia hatuwa kuu tatu ambazo ni kama ifuatavyo:-

 

1.Katika hatuwa ya kwanzacevix (mlango wa mimba) hulegea na kufumguka kwa sentimita 10. hata hivyo kulegea kwa cevix kunaweza kuanza siku chache nyma, kidogo kidogo. Majimaji yanayotoka ukeni huongezeka baada ya kupasuka kwa utando uliomzunguka mtoto. Katika hatuwa hii mikazo ya tumbo la kujifunguwa yanaweza kuwa makali sana ndani ya sekunde 30 mpaka 60 kisha yanakata kwa dakika kama 4 ama 5 kisha huanza tena kama hivi.

 

Katika hatuwa hii maumivu yanaweza kuwa makali sana kiasi cha kuwa kama vile hayakati. Hapa mtoto anaanza kusogea kwenye njia ya kuzalia. Wakati huu atakuwa ana sukumana na njia ya haja kubwa na hapa mwanamke anaweza kujisikia kuenda haja kubwa. Baadhi ya wanawake walio mara ya kwanza kupata ujauzito wanaweza kwenda chooni na hatimaye anazalia chooni. Kumbuka mikazo ya tumbo haupoi hata kwa dawa za kukata maumivu.

 

2.Hatua hii ya piliHatuwa hii huanzia toka pale mlango wa kuzalia unapofunguka hadi mwisho (sentimita 10) mpaka mtoto atakapozaliwa. Mikazo ya tumbo katika hatuwa hii inazidi na kuwa katika mpangilio maalumu kwa kuachana. Kila mkazo unapokuwa mkubwa hapa mwanamke atajihisi kusukuma mtoto. Hapa mwanamke atahisi moto kwenye uke wake wakati mtoto anashuka ama atahisi kutanuka kwa uke wake hasa pale kichwa cha mtoto kinapoanza kutoka.

 

Kipindi hiki mama mamzito atakuwa anapewa maelekezo kuhuku kusukuma mtoto ili kuwezehsa kuzaa kwa haraka. Kuna mengi ambayo daktari ama anayezalisha atatakiwa kuyafanya hapa ili kuwezesha kujifunguwa kwa salama. Mtoto ataanza kutokeza kichwa kisha shingo ikifuatiwa na mabega na baadaye mwili kumalizia. Katika hatuwa hii wahudumu wa afya huwa makini zaidi maana ndio hatuwa yenye hatari sana. Hatuwa hii kwa wanawake ambao ndio ujauzito wao wa kwanza inaweza kuchukuwa lisaa limoja mpaka masaa mawili (1 - 2)

 

3.Hatuwa ya tatuHatuwa hii huanza pale mwanamke atakapojifunguwa. Hatua hii huhu huhusisha kutowa placent, ama kondo la uzazi. Hatuwa hii inaweza kuchukuwa mpaka dakika 30. upotevu wa damu hapa utaendelea kuwepo ijaokuwa si mkubwa. Mikazo ya tumbo la uzazi itasaidia kupunguza upotevu wa damu. Kitukibaya zaidi katika hatuwa hii ni endapo damu itatoka kwa wingi.

 

Hali hii inaweza kupelekea tatizo lijulikanalo kama postpartum haemorrhage na kupelekea upungufu wa damu na uchovu. Hivyo wakunga na wahudumu wataendelea kuwa makini sana katika hatuwa hii. Katika hatuwa hii ndipo mtoto atatenganishwa na placenter.

 

NINI UFANYE UKIWA KATIKA UCHUNGU WA KUJIFUNGUA KATIKA1.Kunywa maji ama juisi kwa wingi ama chai2.Unaweza pia kula kitu kitamu cha kufyonza kama utaruhusiwa. Hii ni kwa ajili ya kukuongezea nguvu3.Badilisha mikao kuaa, kulala, ubavuubavu, chalichali, kusimama na kukaa na kadhalika)4.Kama utaweza kuoga maji ya moto fanya hivyo kabla ya kuingia leba5.Mwambie msimamizi wako kama ataruhusiwa kuingia akufanyie maseji mgongoni ana akusuguesugue6.Jitahidi kurilax kati ya mikazo ya tumbo usisukume mtoto mpaka uambiwe kufanya hivyo7.Unaweza kuomba dawa za maumivu kama utaruhusiwa.8.Usione aibu hata kidogo ukiwa katika leba. Hao unaowaonea aibu wameshaona kila kitu kwako na kwa watu wengine. Kama unataka kulia lia sana, tambuwa kuwa kila kitakachokutokea hapo ni siri na katu hakuna atakayehadithia, hata hivyo kila kitu ni kawaida sana katika leba.9.Fuata maelekezo kama utakavyoambiwa na wahudumu wako. Kosa lolote utakalofanya kumbuka linaweza kuhatarisha maisha yako na ya mtoto wako.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 4150


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

maumivu sehemu zinazoota mavuzi na kuwa namaumiv wakat wa haja ndogo na pia kwenye kichwa cha uume kunakua kama kunavimba
Je kupata maumivu sehemu zinazoota mavuzi na kuwa namaumiv wakat wa haja ndogo na pia kwenye kichwa cha uume kunakua kama kunavimb hizo syo dalili moja wapi? Soma Zaidi...

Njia za uzazi wa mpango
Posti hii inahusu zaidi kuhusu njia za uzazi wa mpango, uzazi wa mpango ni njia za kupanga uzazi Ili kupata idadi ya watoto unaohitaji Soma Zaidi...

Kujaa gesi tumboni
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kujaa tmgesi tumbon Soma Zaidi...

Huduma kwa mama ambaye mimba imetoka moja kwa moja.
Post hii inahusu zaidi huduma kwa mama ambaye mimba imetoka moja kwa moja, aina hiyo ya mimba kwa kitaalamu huitwa complete abortion. Soma Zaidi...

Nimegundua ni mjamzito na kibaya zaid namtoto mchanga nimefanyiwa opaleshen naomba ushauli wako mkuu
Inatakiwa angalau nafasivkati ya mtoto na mtoto wapishane miaka miwili. Soma Zaidi...

Njia za kuondoa fangasi sehemu za siri
Makala hii itakujuza baadhi ya njia utakaoweza kuzifuata ili kukabiliana na fangasi sehemu za siri kwa wanaume Soma Zaidi...

MAJIMAJI YA UKENI, PIA MIWASHO YA UKENI, FANGASI WA UKENI, UCHAFU UNAOTOKA UKENI, SARATANI AU KANSA YA KIZAZI
Soma Zaidi...

Hatua za Kuzuia Maambukizi ya Uvimbe kwenye ovari na mirija ya uzazi
Posti hii inazungumzia kuhusiana na hatua za kujikinga na Maambukizi ya Uvimbe kwenye ovari na kwenye mirija ya uzazi Soma Zaidi...

Mimba iliyotungia nje, sababu zake na dalili zake. Nini kifanyike kuizuia?
Mimba hatari iliyotungia nje ya mji wa mimba, ni zipi dalili zake na ni kivipo mimba inatungia nje? Soma Zaidi...

KUWAHI KUMALIZA TENDO LA NDOA MAPEMA: kumwaga mbegu mapema
Hii ni hali inayowapata sana wanaume huwa wanamaliza hamu ya tendo la ndoa mapema kabla ya mwenza kuridhika. Soma Zaidi...

Sababu za Ugonjwa wa kifafa cha mimba.
Posti hii inahusu zaidi sababu za kifafa cha mimba, kwa kawaida mpaka sasa hakuna taarifa zozote kuhusu sababu za kuwepo kwa kifafa cha mimba ila kuna visababishi vinavyofikiliwa kama ni Dalili za kifafa cha mimba kama ifuatavyo Soma Zaidi...

Je nitahakikisha vipi Kama Nina ujauzito
Somo hili linakwenda kukueleza njia za kuhakiki Kama u-mjamzito Soma Zaidi...