Swala ya jamaa.

Swala ya jamaa.

Kipengele hiki tutajifunza kusimamisha swala ya jamaa,swala za ijumaa.

6.5 Kusimamisha Swala ya Jamaa

Swala ya jamaa inaanzia na watu wawili (imamu mwenyewe na maamuma moja).

  1. Kusimamisha swala ya jamaa ni amri kama aya ya Qur’an (4:102) inavyobainisha.
  2. Kusimamisha swala katika jamaa ina ubora kwa daraja 27 kuliko ya mtu peke yake.
  3. Kusimamisha swala ya jamaa hupelekea ukamilifu na ubora wa swala kwa kuepukana na vishawishi vingi ndani ya swala.
  4. Kusimamisha swala ya jamaa ina jenga umma wa waislamu na kuwa wa moja na kushikamana ipasavyo.

Zifuatazo ni miongoni mwa sababu za kutoswali jamaa msikitini kisheria;

  1. Machafuko ya hali ya hewa kama vile; mvua, baridi au jua kali sana, n.k.
  2. Wakati ukiwa na njaa na chakula kimetengwa mezani.
  3. Kushikwa (kuwa) na haja ndogo au kubwa.
  4. Kuwa mgonjwa au muuguzi.
  5. Kuwa na hofu ya kudhuriwa njiani kama vile; wanyama wakali, n.k.

-     Swala ya Jamaa huanza kwa watu wawili, imamu na maamuma moja.

      Rejea EDK Kitabu cha 1, Sekondari, Uk. 136-141.

 

-     Imamu ni kiongozi, hivyo mtu yeyote mwenye sifa zifuatazo anafaa kuoza swala;

  1. Mwenye kuweza kuisoma Qur’an vizuri na kuielewa vizuri.
  2. Anayefahamu na kuelewa vizuri Hadith na Sunnah za Mtume (s.a.w).
  3. Mwenye tabia njema na siha (afya) nzuri.
  4. Mwenye umri mkubwa.

 

-   Swala ya Ijumaa ni faradh inayosimamishwa siku ya Ijumaa badala ya swala ya adhuhuri.

 

-   Si lazima kutimia idadi fulani ya waumini ili kuswihi swala ya Ijumaa, uthibitisho wa hadith ya Mtume (s.a.w) ni kuwa watu wawili, imamu na maamuma wanatosheleza kuswaliwa Ijumaa.

 

  1. Swala ya Ijumaa ni faradh (amri) ya Allah (s.w) kwa waislamu wote wanaume na wanawake wasio na udhuru wa kisheria.

Rejea Qur’an (62:9-10)

 

2.Kutoswali swala ya Ijumaa bila udhuru kisheria ni miongoni mwa sababu za kupata madhambi na kustahiki adhabu za Allah (s.w).

 

 

-     Wanaolazimika kuswali swala ya Ijumaa ni Waislamu wote wenye sifa zifuatazo;

  1. Wenye afya nzuri (wasio wagonjwa, vikongwe, vilema wasiojiweza, n.k.)
  2. Waungwana (wasio watumwa)
  3. Waliobaleghe (sio watoto)
  4. Wakazi wa mji (wasio wasafiri)
  5. Wasio katika kizuizi kama vile; mvua, n.k.

-     Swala ya Ijumaa ni faradh kwa kila muislamu mwanamume na mwanamke aliye baleghe asiye na udhuru, isipokuwa wafuatao;

  1. Wanawake
  2. Watoto wadogo
  3. Vikongwe na Vilema
  4. Wagonjwa na wenye kuuguza wagonjwa
  5. Wasafiri
  6. Kuzuizi (machafuko) ya hali ya hewa kama vile; mvua, joto kali sana, n.k.
  7. Kuwa na hofu ya kudhuriwa njiani.

 

-     Lengo ni kuwausia, kuwatanabaisha na kuwakumbusha waislamu juu ya wajibu wao kwa Allah (s.w).

 

-     Khatibu ni sharti awe na udhu na akhutubu akiwa amesimama na kuwaelekea watu anaowakhutubia.

 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views: 2854

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii     👉2 Bongolite - Game zone - Play free game     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 ai web app     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

Misingi ya fiqh

Kwenye kipengele hichi tutajifinza vyanzo mbalimbali vya sheria ua kiislamu.

Soma Zaidi...
Uislamu unavyokemea tabia ya ombaomba

Uislamu umekataza tabia ya kuombaomba kama ndio njia ya kuendesha maisha. Pia ukaweka suluhisho la kukomesha tabia hiyo

Soma Zaidi...
Njia za kuzuia na kupunguza zinaa katika jamii

(ii) Hatua za Kuzuia Uzinzi JamiiUislamu pamoja na kutoa mafunzo ya maadii yanayomuwezesha mtu binafsi ajiepushe kwa hiari yake na kitendo kibaya cha zinaa, umechukua hatua mbali mbali ambazo huifanya zinaa isiwe kitendo chepesi katika jamii.

Soma Zaidi...
Wanaostahiki kupewa zakat

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Haki ya kumiliki mali na mipaka yake katika uislamu

Je unaijuwa mipaka yako katika kumiliki mali. Ama unajuwa haki zako katika mali inayomiliki. Endelea na somo

Soma Zaidi...