Mbinu za kuzuia na kuepukana na maradhi ya uti wa mgongo

Posti hii inahusu zaidi njia au mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuepukana na tatizo la ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo.

Mbinu za kuweza kupambana au kuepukana na Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo.

1. Kwanza kabisa tunapaswa kutoa elimu kwa watu ili kuweza kuwajulisha watu kuwepo kwa ugonjwa huu, namna unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine jinsi unavyoweza kutibiwa na mbinu au njia za kuzuia Ugonjwa huu ili usiendelee kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

 

2. Pia kama kuna Dalili za kuwepo kwa Ugonjwa huu kwenye jamii, jamii inapaswa kuepukana na mikusanyiko isiyo ya lazima ili kuepuka madhara makubwa ambayo yanaweza kutokea kama mtu mmoja ana Ugonjwa huu kwenye mkusanyiko anaweza kusambaza kwa wengine na kusababisha kuendelea kuwepo kwa Maambukizi.

 

3. Kuwaelimisha watu kuacha tabia za kugusana moja kwa moja ambazo zinaweza kusababisha kuenea kwa Ugonjwa huu kwa mfano kubusiana, na pia kwa wale wenye tatizo hili hawapaswi kutema tena mate ovyo wawe na sehemu maalum kwa ajili ya kuweka mate siyo kuyasambaza hali ambayo Usababisha kuendelea kuenea kwa ugonjwa na kuweza kuongeza namba ya waathirika wa Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo.

 

4. Pia madawa ya kutibu Ugonjwa huu yanapaswa kuwepo na pia kila aina ya kipimo inapaswa kuwepo ili kuweza kutambua visababishi mbalimbali,na pia kwa upande wa watoto wadogo wanapaswa kutolewa chanjo mapema ili kuweza kuwa na kinga ya kupambana na ugonjwa huu endapo utatokea .

 

5. Kwa wale wenye imani tofauti au potofu kuhusu Ugonjwa huu ni lazima waache ili kuweza kuwapeleka wagonjwa hospitalini na kupata matibabu mapema ili kuokoa maisha kwa sababu Ugonjwa huu bila matibabu yoyote hali inaweza kuwa mbaya na hatimaye kuwapoteza wapendwa wetu.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/06/07/Tuesday - 07:18:17 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1055


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-