Fahamu kuhusu Ugonjwa wa ukoma
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa ukoma, ni Ugonjwa unaosababishwa na mdudu anayeitwa mycobacterium leprae, mdudu huyu kwa kawaida uathiri sana sehemu za ngozi na sehemu za Neva mbalimbali za mwili
Fahamu kuhusu Ugonjwa wa ukoma.
1. Kwa kawaida hapo mwanzoni kabisa Ugonjwa huu haukuwa na dawa , kwa hiyo watu waliopatwa na Ugonjwa huu walionekana ni watu wenye balaa kwa hiyo hawakuruhusiwa kuishi na watu wengine kwenye jamii, lakini kadiri siku zinavyokwenda kutoka siku moja kwenda nyingine watu wameelewa kuhusu Ugonjwa huu na dawa imepatikana kwa hiyo watu wanapona kwa kufuata mashariti mbalimbali.
2.ugonjwa huu uweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kugusana na mtu mwenye ukoma hasa wakigusana na maji maji ya mtu mwenye ukoma na hasiye na ukoma na pengine kwa njia ya hewa hizi , kwa hiyo watu wanapaswa kuwa makini wakati wanapoishi na watu wa ukoma ili kuweza kuepuka hali ya kusambaa kwa ugonjwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
3. Pia mgonjwa anaweza kuwa na Dalili mbalimbali kama vile kuharibika kwa ngozi, kuharibika kwa mfumo wa Neva, pengine mtu anaweza kuwa mgumba kama Ugonjwa umeingia mpaka ndani, pia kunakuwepo na kuharibika kwa mifupa na pengine mtu anaweza kuwa mgumba, kwa hiyo Dalili hizo uweza kuanza taratibu na kuenea taratibu kwenye mwili wa mtu na matibabu yasipotolewa mapema hali ya mtu huwa mbaya zaidi.
4. Kwa hiyo tunajua wazi kuwaa Ugonjwa huu una tiba na dawa zipo kwa hiyo hakuna sababu ya kuwatenga wagonjwa walioathirika na Ugonjwa huu kwa sababu matibabu yakitolewa ipasavyo Mgonjwa anapona Kawaida na kurudia kwenye hali ya kawaida,kwa hiyo watu wenye tabia ya kutenga wagonjwa wenye matatizo haya wanapaswa kupewa elimu ili kuweza kuwajali wagonjwa hawa ili waweze kupata matibabu ipasavyo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 web hosting 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Kichaa cha mbwa.
Post hii inahusu zaidi kichaa cha mbwa,au kwa kitaalamu huitwa rabies, utokea pale mtu anapongatwa na mnyama ambaye ni jamii ya mtu au mbwa mwenyewe
Soma Zaidi...Madhara ya kutotibu maambukizi chini ya kitovu
Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu maambukizi chini ya kitovu ni madhara ambayo yanaweza kutokea kwa mgonjwa pale ambapo matibabu yanapokuwa hayatolewi kwa mgonjwa wa maumivu chini ya kitovu.
Soma Zaidi...Sababu za mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu.
Post hii inahusu zaidi mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu na kwa kitaalamu huitwa retention of urine.
Soma Zaidi...Fangasi wanaosababisha mapunye dalili zao na jinsi ya kupambana nao
Fangasi hawa ni maarufu sana kwa mapunye ya kichwani ama kwenye ngozi mikononi ama miguuni.
Soma Zaidi...