Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa alieye ingiwa na uchafu puani (foreign body)
Ishara na Dalili ya kitu kuingia kwenye pua (foreign body).
1. Kutoa makamasi au usaha.
2.kutokwa na Damu.
3.Pua kuwasha.
4.Maumivu
5. Ugumu wa kupumua kupitia pua iliyoathiriwa.
6.kutoa harufu mbaya Kama uchafu ukikaa kwa muda mrefu
Sababu zainazopelekea kuingia kwenye pua Ni
Vitu vilivyowekwa kwenye pua vinaweza kujumuisha
1. Chakula.
2.Mbegu
3. Maharage yaliyokaushwa
4. Kifutio
5. Pamba
6. Shanga
7. Vifungo vya kwenye nguo.
Mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa aliyeingiliwa na uchafu au kitu kwenye pua
1. Usichunguze kitu hicho kwa kutumia pamba au zana nyingine kwasababu unaweza ukakisukumia Ndani zaidi.
2. Usijaribu kuingiza kitu hicho kwa kuvuta pumzi kwa nguvu.
3. Badala yake, pumua kupitia kinywa chako hadi kitu kiondolewe.
4. Piga pua yako taratibu ili kujaribu kuachilia kitu, lakini usipige kwa nguvu au mara kwa mara.
5. Ikiwa pua moja tu imeathiriwa, funik pua ambayo haijaathiriwa na kisha pumua kwa upole kupitia pua iliyoathirika.
6. Ikiwa kitu kinaonekana na unaweza kukishika kwa urahisi na kibano, kiondoe unaweza kujitoa kwa utaratibu zaidi.
7. Usijaribu kuondoa kitu ambacho hakionekani au kushikika kwa urahisi.
10 Mpeleke mgonjwa hospitali kwa usimamizi zaidi Tena ikitokea Kama kitu kilichoingia puani hakionekani,au hakijatoka.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia wagonjwa waliopata maambukizi kwenye milija na ovari, ni wagonjwa waliopata maambukizi kwenye milija na ovari.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kujikinga na kisukari
Soma Zaidi...Presha ya kupanda hutokea pale kipimo kinaposoma zaidi ya 120/80mm Hg.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na presha ya kushuka
Soma Zaidi...Endapo U.T.I inajirudiarudia baada yavkutibiwa inawezabkuwa ikakupa mawazo mengi. Katika post hii nitakufafanulia nini ufanye.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna chanjo ya polio inavyotolewa na ratiba zake yaani kuanzia siku ya kwanza mpaka pale mtoto anapomaliza chanjo hii kwa hiyo tuone ratiba ya chanjo ya polio.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi malengo ya kutibu ukoma, ni malengo ambayo yamewekwa na wizara ya afya ili kuweza kutokomeza ukoma kwenye jamii
Soma Zaidi...