Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Kwa nini Wengi wanaoswali hawafikii Lengo la Swala zao?
Miongoni mwa sababu ya wengi kutofikia malengo ya swala zao ingawa wanaziswali misikitini tena kwa jamaa ni;
Hawajui lengo halisi la swala.
Waislamu wengi huswali kwa lengo la kufutiwa madhambi na kupata thawabu na sio kuepukana na machafu na maovu, ambalo ndio lengo kuu la swala. Kupata thawabu na kufutiwa madhambi ni matunda ya swala.
Rejea Quran (29:45) na (72:23).
Waislamu wengi hawana ujuzi sahihi juu ya swala.
Pamoja na waislamu wengi kutekeleza swala zao kwa jamaa lakini wengi wao hawajui kabisa miiko, sharti na nguzo za swala ila wanafuata mkumbo tu.
Rejea Quran (7:205), (7:55) na (4:142).
Waislamu wengi hawahifadhi swala zao.
Pamoja na kuswali kwao bado wengi hawazingatii na kutekeleza kikamilifu sharti na nguzo za swala zao inavyotakiwa.
Rejea Quran (107:4-5) na (23:1,8).
Wengi hawaswali kwa Unyenyekevu swala zao.
Kukosa unyenyekevu (utulivu wa mwili, fikra na uzingativu) hupelekea mwenye kuswali kutofikia lengo na matunda ya swala.
Rejea Quran (29:45), (23:1-2) na (23:10-11).
Kutosimamisha Swala za jamaa ipasavyo.
Waislamu wengi hawaswali jamaa misikitini au hawazingatia sharti za swala ya jamaa kama kunyoosha safu ipasavyo, kugusanisha mabega, vidole, n.k.
Rejea Quran (23:1-2).
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inakwenda kukufundisha mambo ambayo hubatilisha udhu yaani mam,boa mbayo yanaharibu udhu.
Soma Zaidi...Ni kwa nini Allah ametutaka tugunge. Je kuna lengo gani hasa katika kufunga.
Soma Zaidi...Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...(iii) Adhabu ya UzinifuKatika Sheria ya Kiislamu mtu haadhibiwi mpaka atende kwa uwazi matendo yenye kuvuruga utaratibu na amani ya jamii.
Soma Zaidi...