image

Hukumu na sherei zinazohusu ajira na kazi katika uislamu

Wajibu wa KufanyakaziUislamu siyo tu unawahimiza watu kufanya kazi na kutokuwa wavivu bali kufanya kazi ni Ibada.

Hukumu na sherei zinazohusu ajira na kazi katika uislamu

Wajibu wa Kufanyakazi
Uislamu siyo tu unawahimiza watu kufanya kazi na kutokuwa wavivu bali kufanya kazi ni Ibada. Kila jambo lenye manufaa kwa watu binafsi, familia, jamii (n.k) laweza kuhesabiwa kuwa ni Ibada kwa Allah yakitimia masharti mawili; usafi wa nia (Ikhlasi) na kutenda jambo kwa kuzingatia mipaka ya sheria ya Kiislamu. Hivyo kazi ni Ibada. Kufanya kazi ni wajibu alionao mtu mbele ya Allah.Qur-an inawahimiza Waislamu kutenda kazi nzuri zenye manufaa katika eneo lolote lile.


Na sema: Tendeni mambo (mazuri). Mwenyezi Mungu atayaona mambo yenu hayo na Mtume wake na Waislamu. Na mtarudishwa kwa mjuzi wa siri na dhahiri; naye atakwambieni (yote) mliyokuwa mkiyatenda.” (9:105) Katika aya hii Mwenyezi Mungu amefungua milango kwa watu kutenda mambo yote mema katika eneo lolote la uchumi au siasa na yeye ataliona na atalilipa.



Uchaguzi wa kazi
Uislamu umempa mtu uhuru wa kuchagua kazi yoyote aipendayo maadamu kazi hiyo ni ya halali kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu. Na ni wajibu wa serikali ya Kiislamu kuhakikisha kuwa watu wanapata fursa ya kufanya kazi wazipendazo. Watu watafanya kazi kwa mujibu wa vipaji vyao, kwani Mwenyezi Mungu amewajaalia watu vipawa mbali mbali:



“Na amewanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja kubwa ili akufanyieni mtihani kwa hayo aliyokupeni.” (6:1 65).
Kila mtu anafanyiwa mtihani kwa neema au kipawa alichopewa. Katika maisha yetu ya kila siku wanaadamu ni viumbe wanaotegemeana kila mmoja ananufaika kwa kazi ya mwenzake. Daktari atamhitaji Muashi kumjengea nyumba yake na Muashi atamhitaji Daktari kumtibu maradhi yake n.k. Katika Uislamu kazi hutegemea uwezo tu hakuna kazi zilizotengwa kwa ajili ya watu wa ukoo au kabila au nasaba fulani.



Tofauti ya malipo
Tofauti ya mapato au malipo ipo kwa sababu ya utendaji, uwingi au ubora wa bidhaa zilizozalishwa. Ni halali kwa fundi aliyetengeneza mashati kumi, hasa amzidi kipato yule aliyetengeneza matano. Au yule aliyetengeneza kitu bora lazima amzidi yule aliyetengeneza kitu duni. Aidha tafauti ya mapato pia ni halali iwepo kutokana na muda mrefu wa mafunzo baadhi ya kazi zikilinganishwa na nyingine. Kwa mfano ikiwa mtu ataajiriwa kufuta mavumbi katika madirisha ya ofisi atahitajia siku moja tu ya kuelekezwa namna ya kuifanya kazi hiyo.


Lakini mtu akiajiriwa kutengeneza madirisha hayo atahitajia muda mrefu zaidi katika kujifunza useremala hawezi kuelekezwa kwa siku moja tu halafu akaweza kuunda dirisha. Hivyo malipo ya mfutaji na mtengenezaji wa madirisha hayawezi kuwa sawa. Malipo yao yakiwa sawa basi watu wanaweza kuzikwepa kazi zinazohitaji mafunzo ya muda mrefu kama udaktari, usanifu majengo uhandisi (n.k.) na kukimbilia zile zenye mafunzo ya muda mfupi kama utarishi, uhudumu, kufagia ofisi n.k.
Aidha malipo hayatakuwa halali iwapo shughuli anayoifanya Muislamu ni faradhi. Kwa mfano; si halali kwa Imamu kupokea mshahara kwa ajili ya kusalisha swala za faradhi, si halali kupokea malipo kutokana na kumhudumia maskini, n.k.



Hifadhi ya Wafanyakazi
Uislamu pia umeweka taratibu za kuhifadhi haki na maslahi ya Wafanyakazi. Kwanza kila mfanyakazi lazima awe na mkataba na mwajiri wake. Mkataba huo uweke wazi malipo yake na kazi yake na makubaliano yao mengine. Mkataba huo ni bora uwe kwa maandishi lakini waweza pia kuwa kwa mdomo.
Mwenyezi Mungu ameagiza katika Qur-an kuwa watu watekeleze kikamilifu ahadi zao za halali.


“Enyi mlioam ini tekelezeni w ajibu …” (5:1)
Katika Hadith iliyosimuliwa na Bukhari, Mtume (s.a.w) amesema kuwa miongoni mwa watu watatu ambao Mtume (s.a.w) atawakataa siku ya Kiyama ni yule anayemwajiri mfanyakazi halafu asimpe haki zake.Katika Hadith nyingine amesema;Mlipeni mtu mliyemuajiri kabla ya jasho lake halijakauka. Mradi wa Hadith hii ni kuwa mtu asicheleweshewe malipo yake. Kama mapatano ni kila wiki au kila mwezi n.k. basi muda huo ukifika tu mtu alipwe.Vivyo hivyo kwa mfanyakazi malipo ya kazi yatakuwa ni halali iwapo atatimiza kipimo walichoafikiana na mwajiri kwa mshahara huo. Kutegea kazi humfanya mtu achukue sehemu ya malipo isiyo haki yake. Kwa hiyo, kipato kinachotokana n a kazi iliyotegewa kimechanganyika na kipato cha haramu. Uislamu unamtaka kila muumini awe mwaminifu na muadilifu katika kazi baada ya kupatana na kukubaliana na muajiri.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 559


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Fadhila za kufunga mwezi wa ramadhani
Soma Zaidi...

MALI ZISIZORUHUSIWA KUTOLEWA ZAKA
*Suala la kumilikiwa binaadam (utumwa), japokuwa linaendelea kutajwa kwenye Sharia (katika vitabu), ni suala ambalo haliko. Soma Zaidi...

Jinsi uislamu ulivyokomesha biashara ya utumwa wakati na baada ya mtume Muhammad (s.a.w)
Soma Zaidi...

Maana ya shahada
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Hili ndio lengo la kufunga.
Ni kwa nini Allah ametutaka tugunge. Je kuna lengo gani hasa katika kufunga. Soma Zaidi...

Kufunga Mwezi wa ramadhani kisheria
Soma Zaidi...

Maandalizi kwa ajili ya kifo
Mwanadamu anatakiwa aishi huku akikumbuka kuwa ipo siki atakufa. Hivyo basi inatupata lujiandaa mapema kwa ajili ya kifo. Soma Zaidi...

Je manii ni twahara au najisi?
Post hii itakwenda kukufundisha hukumu ya manii kuwa ni twahara ama ni najis Soma Zaidi...

namna ya kuswali 6
Lugha ya Swala Lugha ya swala,kuanzia kwenye Takbira ya kuhirimia Swala mpaka kumalizia swala kwa Salaam, ni Kiarabu. Soma Zaidi...

Maana ya swala
Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno Swalaat lina maana ya ombi au dua. Soma Zaidi...

Faida za funga
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Ni kwa nini lengo la Funga na swaumu halifikiwi na wafungaji?
Kwa nini Lengo la Funga halifikiwi na Wafungaji Wengi? Soma Zaidi...