Kipengele hichi tutajifunza namna ya kusimamisha swala ukiwa safarini na vitani na nguzo zake.
6.4.Kusimamisha Swala za Faradh katika nyakati za Dharura.
- Swala imepangiwa muda maalumu, isiswaliwe nje ya muda wake ila kwa udhuru wa kisheria.
- Hapana ‘kadha’ (kulipa swala) au kuswali swala nje ya wakati wake bila dharura kisheria.
Rejea Qur’an (4:103), (2:286), (2:185), (5:6).
Rejea Qur’an (4:43) na (5:6).
2. Kama mgonjwa hajimudu kujitwaharisha kwa maji au tayammamu na hana mtu wa kumsaidia, basi atatayammamu kwa ishara na kuswali kwa ishara (kifikra) pia.
Rejea Qur’an (5:6).
3. Mgonjwa anaruhusiwa kuswali akiwa amekaa na kuelekea Qibla kama anaweza, na atarukuu na kusujudu kwa kukaa au kwa ishara jinsi atakavyoweza.
4. Iwapo hawezi kukaa basi ataswali akiwa amelala kwa ubavu akiwa ameelekea Qibla kama anaweza, vinginevyo ataelekea popote na kulala chali au kulala vyovyote awezavyo.
5. Mgonjwa anaruhusiwa kuchanganya swala na kuzifupisha kama msafiri kulingana na hali ya ugonjwa na mazingira yake.
- Muislamu akiwa safarini anawajibika kutekeleza swala kama ifuatavyo;
Rejea Qur’an (5:6), (4:101) na (2:238-239).
2. Anaruhusiwa kupunguza swala zenye rakaa 4 na kuswali rakaa mbili mbili ambazo ni Adhuhuri, Alasir na Ishaa tu.
3. Pia msafiri ameruhusiwa kuunganisha swala 2, Adhuhur na Alasir, Magh’rib na Ishaa tu kwa kuziswali muda mmoja, kwa kuzitanguliza muda wa swala ya mwanzo (Jamu’ Taq’diim) au kuzichelewesha na kuziswali muda wa swala inayofuata (Jamu’ Ta’akhiir)
4. Pia msafiri anaruhusiwa kuswali huku akiwa anatembea au anaendelea na safari kwenye kipando chake.
Kusimamisha swala ya faradh katika uwanja wa vita ni kama ifuatavyo;
Rejea Qur’an (4:102-103).
- Askari wagawanyike katika makundi mawili, ambayo yataswalishwa jamaa na imamu mmoja.
- Swala itafupishwa kama ilivyo katika swala ya safari, kwa kuswaliwa rakaa mbili yenye rakaa 4.
- Kundi moja litaanza kuswali na imamu likiwa na silaha zao na jingine likiwa katika ulinzi.
- Imamu ataswali rakaa moja ya mwanzo na kundi la mwanzo, na watakaponyanyuka rakaa ya pili, kila askari atamalizia rakaa ya pili kivyake haraka na baada ya kutoa salaam atarudi kuchukua nafasi ya ulinzi.
- Imamu atabakia amesimama katika rakaa ya pili mpaka kundi la pili litakapounga jamaa nyuma yake ndipo ataendelea kumalizia rakaa yake ya pili.
- Imamu atakapomaliza rakaa ya pili atatoa salaam na kila askari atasimama na kivyake kumalizia rakaa ya pili haraka na kutoa salaam pia.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Kabla ya kuhubiriwa uislamu watu wa Maka walikuwa na tarayibu zenye dhuluma ndani yake katika ugawaji wa mirathi.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Hapa tunakwenda kuona jinsi ya kuzitathmini swala zetu.
Soma Zaidi...Huwezi kuruhusiwa kumrejea mke endapo utamuacha kwa talaka hizi mbili.
Soma Zaidi...Hspa utajifunza sasa jinsi ya kugawa mirathi kutokana na viwango maalumu.
Soma Zaidi...