faida za kula tunda zabibu kwa ajili ya afya yako
1.Zabibu (grapefruit).
Hili ni tunda ambalo lina historia kubwa kwenye maisha ya wanaadamu. Tunda hili linaweza kupatikana maeneo mengi duniani. Zabibu ni moja kati ya matunda yanayotambulika kuwa na mchango mkubwa katika kuboresha Afya ya mwanadamu tka zamani sana.
Zabibu linatambuliwa kuwa ni chanzo kizuri sana cha vitamini na madini kwenye miili yetu. zabibu ni katika matunda ambayo yana vitamini kwa wingi kuliko mengi katika matunda ambayo tunayala. Itambulike kuwa vitamini na madini ni katika virutubisho muhimu vinavyofanya mwili wako kuwa madhubuti na afya njema sikuzote.
Tunda hili pia hitambulika kuwa na uwezo mkubwa wa kusaidia kupunguza uzito wenye madhara mwilini mwako. Itambulike kuwa uzito ukizidi mwilini kuna matatizo mengi ya kiafya unaweza ukayapata kama kupata maradhi ya kisukari na shinikizo la damu. Hivyo tunda hili husaidia katika kupunguza uzito mwilini mwako. Ni vyema ukala tunda hili kabla ya kula chochote.
Tunda hili pia linatambulika kuwa na uwezo wa kusaidia kuweka madhubuti insulini iwe katika hali ya kawaidi. Itambulike kuwa insulin ikisumbua huweza kusababisha ugonjwa wa kisukari. Pia tunda hili husaidia katika kudhibiti afya ya figo. Kwa mfano zabibu hupunguza hatari za kupata maradhi ya figo yanayoitwa kidney stone yaani vijiwe vinavyokaa kwenye figo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kunywa chai
Soma Zaidi...Usiogope kuwashwa, kula pilipili ni nzuri kwa afya yako ia virutubisho vingi sana
Soma Zaidi...Uchachu wa ukwaju, ndio ubora wake, kuna virutubisho vingi kwa kula ukwaju, soma makala hii
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula pilipili
Soma Zaidi...Zijuwe sababu za upungufu wa damu, dalili za upungufu wa damu na kazi za damu mwilini,n avyakula vya kuongeza damu
Soma Zaidi...Posti hii moja kwa moja inaenda kuelezea vyakula vya nyuzinyuzi zinazopatikana kwenye matunda na mboga mboga.
Soma Zaidi...