Faida za kula uyoga

Kula uyoga kwa faida kubwa, ja unazijuwa faida za kula uyoga kiafya

Faida za kula uyoga

20. Uyoga (mushroom)
Uyoga pia ni katika vyakula vya asili, ijapokuwa upatikanaji wake umekuwa mchache siku hizi. Shukrani ziwaendee wataalamu wa kilimo, kwa sasa tunaweza kuzipata mbegu za uyoga kutoka maabara na kulima uyoga popote pale. Wataalamu wa mimea wanaamini kuwa uyoga si katika mimiea kwani uyoga upo katika kundi la viumbe liitwalo fungi (kingdom fungi). ila tunapozungumzia vyakula uyoga tunauweka kwenye kundi la mbogamboga. Uyoga una virutubisho vingi na vizuri kwa afya.

Kulinda mwili zidi ya cancer, Kama ilivyokuwa kwenye matunda na mboga zingine kuwa kuna antioxidant ambayo hii ni chembechembe inayopambana na sumu na kemikali ambazo zinaweza kuathiri seli za mwili wako. Basi kwenye uyoga pia kuna antioxidant kama iliyo karoti na matunda mengine tuloona hapo juu. Hii husaidia kwa kiwango kikubwa kupambana na kuuwa seli za kansa au saratani ambazo zinatengenezwa mwilini.

Mna kwenye uyoga madini yanayoitwa selenium, madini haya huwezi kuyapata kwenye matunda mngi sana na mbogamboga nyingi lakini haya utayapata kwa urahisi kwenye uyoga. Madini haya husaidia katika kuuwa seli sa saratani, pia kuzuia kuota kwa uvimbe unaosababishwa na saratani na aina zingine za vimbe.

Uyoga una vitamin D, ambavyo hivi pia husaidia katika kupambana na kuthibiti kukuwa kwa seli za saratani mwilini. Vitamin D husaidia katika utendaji mwema wa kazi za DNA. Itambulike kuwa saratani huanza kuathiri DNA ndio baadae huendelea kukuwa ndani ya mwili na baadae kuathiri sehemu za mwili. Hivyo uyoga una chembechembe hizi ambazo husaidia katika kupamba na nsa saratani.

Uyoga husaidia katika kuthibiti na kupamabana na kisukari hususan type 2 diabetes. Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa ulaji wa vyakula vyenye kambakamba (fiber) husaidia katika kushusha kiwango cha sukari kwenye damu. Hivyo husaidia katika kuimarisha afya ya itengenezwaji wa insulin.

Husaidia katika kuimarisha afya ya moyo, uwepo wa lkambakamba, madini ya potassium pamoja na vitamin C husaidia kwa kiwango kikubwa katika kuimarisha afya ya moyo (cardiovascular health). ulaji wa vyakula vyenye madini ya potassium kwa wingi pamoja na sodium kwa kiwango kidogo husaidia katika kupunguza shinikizo la damu hivyo husaidia kwa wale wenye presha ya kupanda ya damu.

Husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga mwilini (immune system). madini ya selenium yaliyomo kwenye uyoga kusaidia katika kushawishi na kustimulate mfumo wa afya mwilini katika kupambana na wadudu wavamizi. Madini haya husaidia katika kusahwishi T-cell au CD4 katika kupambana na wadudu wavamizi kama bakteria, virus na fangas. Beta-glucan inayopatikana kwenye ukuta wa seli za uyoga husaidia katika kuufanya mwili upambane vyema na wavamisi na kupamba nna na vijidudu vya maradhi.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 2118

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Dua za Mitume na Manabii    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

JITIBU KWA TANGAIZI: faida za kiafya za tangaizi

Tangaizi ni katika mimea yenye asili na bara la asia hususan nchi ya China.

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula samaki

Posti hii itakwenda kukupa faida za kula samaki kwenye mwili wako.

Soma Zaidi...
Faida za kitunguu thaumu mwilini

Makala hii itakuletea faida za kitunguu thaumu katika afyabyako.

Soma Zaidi...
Faida za mchaichai/ lemongrass

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za mchaichai

Soma Zaidi...
Faida za uyoga mwekundu

Posti hii inahusu zaidi faida kuhusu uyoga mwekundu ni uyoga unaopatikana katika sehemu mbalimbali na pia kuna waliofanikiwa kupandikiza na kuweza kuvuna ila uyoga huu una siri mbalimbali kama tutakavyoona.

Soma Zaidi...
Papai lililo iva ni salama kwa mama mjamzito au halifai

Papai ni moja kati ya matunda yenye vitamini C na virutubisho vinginevyo. Lakini papai pia ni moja kati ya vyakula ambavyo mjamzito anatakiwa awe makini navyo.

Soma Zaidi...
Hizi ndio kazi za madini mwilini mwako

Post huu inakwenda kukupa orodha ya madini muhimu kwa ajili ya afya yako.

Soma Zaidi...