Makala hii inakwenda kukuonyesha faida za kula bamia kwa afya afya
Bamia ni katika matunda ambayo ni mboga na karibia maeneo mengi mboga hii inapatikana. Bamia ni katika mboga muhimu sana kwani ina faida nyingi sana. Ndani ya bamia kuna vitamin, madini na kambakamba. Bamia hutumiwa kuanzia majani, mbegu, bamia lenyewe , maua, kikonyo na matawi. Kwa ufupi mbamia wote ni mboga na huliwa.
Ndani ya bamia kuna fiber (kambakamba), folate, vitamin K na madini. Bamia husaidia katika kuboresha na kuimarisha afya ya moyo pia hulinda mwili dhini ya saratani. Jitahidi ukinunua bamia lisikae zaidi ya siku tatu ama nne. Madini ya potassium na sodium hupatikana katika bamia bila ya kusahau vitamin A ambavyo hupatikana pia kwenye bamia.
Ndani ya bamia kuna aina ya protin inayoitwa lectin, ambayo pia huweza kupatikana kwenye maharage na nafaka nyingine. Wataalamu wa afya walitumia lectin inayozalishwa na bamia kwa ajili ya kutibu seli za saratani ya matiti (breast cancer). matokeo ya utafiti huu ulionesha kuwa seli za saratani zilipunguwa kwa asilimia 63 na zilikufa kwa asilimia 73. tafiti nyingi zinahitajika kufanywa kuhusu swala hili.
Pia ndani ya bamia kuna folate. Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa watu ambao hawapati kula fotate za kutosha wapo hatarini zaidi ya kupata saratani ya matiti, nyia ya uzazi, ini na aina zingine za saratani. Pia baadhi ya tafiti zilizofanya mwaka 2016 zainaonesha kuwa fotate inaweza kuzuia athari za saratani ya matiti.
Tafiti pia zinaonesha kuwa folate ambayo hupatikana kwenye bamia husaidia katika kuzuia matatizo wakati wa ujauzito. Tafiti zinaonesha mwanamke ambaye hana folate za kutosha anakuwa hatarini kupoteza ujauzito wake au mtoto akajapata matatizo ya kiafya baadaye. Fotate ni muhimu sana kwa mwanamke wakati wa ujauzito na wakati wa kunyonyesha.
Mwaka 2011 tafiti za kisayansi zilikuwa zikichunguza athari ya bamia kwa wenye kisukari. Wataalamu walitengeneza poda kutokana na maganda ya bamia na mbegu zake. Kisha wakatumia katika kutibu kisukari kwa panya kama majaribio. Panya huyu alikuwa na tatizo la sukari ya kushuka. Matokeo haya yakaleta athari chanya. Hivyo inashauriwa kwa wenye kisukari kutumia sana bamia.
Tafiti zilizofanya na AHA (American Heart Association) zimesema kuwa kula chakula chenye kambakamba (fiber) hupunguza athari hasi za cholesterol ndani ya damu. Vyakula hivi pia hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na stroke (kupalalaizi).
Tafiti zinaonesha kuwa vyakula vyenye vitamin K kwa wingi kama bania ni mujarabu sana katika kuimarisha afya ya mifupa. Vitamin hivi husaidia mifupa kufyonza madini ya calcium. Watu wenyekula vitamin K kwa wingi wana mifupa imara na isiyokuwa na mipasuko (hii ni nadharia tu).
Bamia husaidia katika kuzuia kupata tatizo la kukosa choo kwani kuna kambakamba ndani ya bamia, hizi husaidia katika mmeng’enyo wa chakula na kusafiri kwa chakula kutoka tumboni kuelekea maeneo mengine kwenye almentary canal. Bamia hupunguza hamu ya kula, hivyo husaidia katika kupunguza uzito.
Pia itambulike kuwa zipo athari hasi za kula bamia kwa kupitiliza. Kwa mfano bamia hupunguza hamu ya kula, pia bamia huweza kupelekea kujaa gesi tumboni na kujaza tumbo. Kula bamia nyingi zaidi huweza kupelekea kupata vijiwe ndani ya figo kwani bamia zina madini ya calcium kwa wingi.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2023
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 Simulizi za Hadithi Audio
👉4 kitabu cha Simulizi
👉5 Kitau cha Fiqh
👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Faida za kula tango
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula tango Soma Zaidi...
Kazi ya Piriton
Posti hii inahusu zaidi kazi ya Piriton katika kutibu mzio au akeji ni dawa ambayo kwa lingine huitwa chlorpheniramine Maleate. Soma Zaidi...
Vyakula vyenye madini kwa wingi
Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya vyakula vyenye madini kwa wingi Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula Mbegu za papai
Soma Zaidi...
magonjwa na lishe
DARASA LA AFYA MAGOJWA YANAYOHUSIANA NA VYAKULA 1. Soma Zaidi...
Vyakula vya vitamin C
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za vyakula vya vitamin C Soma Zaidi...
VINYWAJI SALAMA KWA MWENYE KISUKARI
Kuchaguwa vinywaji si jambo rahisi, lakini inabidi iwe hivyo kama una tatizo la kisukari. Je unasumbuka kujuwa vinywaji salama? makala hii ni kwa ajili yako, hapa tutaona vinywaji ambavyo ni salama kwa mwenye kisukari. Soma Zaidi...
Vinywaji salama kwa mwenye kisukari
Vijuwe vinywaji salama kwa mgonjwa wa kisukari Soma Zaidi...
Ni nini maana ya mlo kamili?
Mlo kamili ni mkusanyiko kuu wa vyakula mbalimba kwa pamoja huimarisha na kuujenga  mwili wa binadamu na wanyama kwa sababu vinaleta virutubishi vyote vinavyohitajika.  Mkusanyiko wa vyakula vinavyotengeneza mlo kamili Kuna majina ya vyakula Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula maharagwe, njegere, kund na mbaazi
Soma Zaidi...
Faida za kula Faida za kula Boga
Makala hii inakwenda kukueleza faida za kula maboga, na mbegu zake kwa afya yako Soma Zaidi...
Faida za vyakula vya asili
Posti hii inahusu zaidi faida za matumizi ya vyakula vya asili, kama tunavyojua kwamba mababu na mabibi zetu walitumia vyakula vya asili wakaishi miaka mingi kweli. Soma Zaidi...