Makala hii inakwenda kukueleza faida za kula maboga, na mbegu zake kwa afya yako
19. Boga (pumpkin)
Boga ni katika vyakula vya asili walivyotumia mababu zetu toka enzi za zamani sana. Boga ni katika chakula chenye vitamin A. pia boga husaidia katika kushusha presha kwani mna kwenye mbegu za maboga aina ya mafuta pytoestrogens ambayo ndio hupunguza shinikizo la damu (hypertension).
Maboga husaidia katika ku[ata usingizi mnono kwani mna kwenye mbegu za maboga typtophan aina ya amino asid ambayo husaidia katika kurelax. Pia mna beta-carotene na aina zingine za antioxidant ambazo husaidia katika kuzuia kupata cancer.
Maboga ni muhimu katika kuboresha na kuimarisha afya ya nguvu za kiume. Pia chakula hiki ni muhimu kwa afya ya moyo. Kwani kutokana na kambakamba zilizomo kwenye maboga mlaji anakuwa na nafasi ndogo sana ya kuweza kupata mabonjwa ya moyo (coronary heart diseases).
Chakula cha maboga pia husaidia katika kuzuia na mlaji kupata ugonjwa wa kisukari. Pia huimarisha vyema afya ya mwenye kisukari. Chakula hiki husaidia katika ufyonzwaji wa glucose kwenda kwenye tishu za mwili. Pia husaidia katika kubalans kiwango cha sukari ndani ya mwili.
Maboga husaidia katika kuboresha na kuimarisha mfumo wa kinga mwilini (immune system). kwani vitamin C pamoja na beta-carotene husaidia mara dufu katika kuimarisha mfumo wa kinga ili kuweza kupambana na maradhi mbalimbali mwilini. Isitoshe beta-carotene kuweza kubadilishwa kuwa vitamin A, na hali hii huweza kusaidia katika kuzalishwa kwa seli hai nyeupe mwilini ambazo ndio hupambana na maradhi na vijidudu vishambulizi kama bakteria, fangas na virusi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya kuoambana na mafua
Soma Zaidi...Posti hii moja kwa moja inaenda kuelezea vyakula vya nyuzinyuzi zinazopatikana kwenye matunda na mboga mboga.
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukuonyesha faida za kula bamia kwa afya afya
Soma Zaidi...Zijuwe sababu kuu za kuwepo kwa maumivu ya tumbo baada ya kula chakula
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi madini ya Shaba mwilini,ni madini ambayo ufanya kazi mbalimbali mwilini, kama ifuatavyo
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu aina za vyakula vya wanga na umuhimu wake mwilini
Soma Zaidi...Makala hii itakuletea faida za kitunguu thaumu katika afyabyako.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu matunda yenye vitamin C kwa wingi
Soma Zaidi...