Faida za kula ukwaju
Uchachu wa ukwaju, ndio ubora wake, kuna virutubisho vingi kwa kula ukwaju, soma makala hii
22. Faida za ukwaju (Tamarind)
Ukwajju ni katika mimea ambayo matunda yake yanatumika katika kutengenezea madawa ya hospitali. Kinywaji cha ukwaju hutumika katika kutibu kuharisha, kukosa choo, homa na aina za vidonda vya tumbo. Tofauti na matunda pia majani na maganda ya mti huu pia hutumika katika kutibu vidonda. Wataalamu wa afya bado wanaendelea kuuchunguza mti huu kwa ajili ya kupata tiba zaidi.
Antioxidant ambayo ipo kwenye ukwaju husaidia katika kudhibiti na kulinda mwili dhidi ya maradhi ya moyo, saratani na kisukari. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa ukwaju husaidia katika kushusha kiwango cha sukari kwenye damu. Pia kwa watu wenye kutaka kupunguza uzito, ukwaju pia husaidia.
Ukwaju una virutubisho vingi sana kama vile:- madini ya magnesium, potassium, chuma, calcium na phosphorous. Pia kuna vitamin B1 (thiamin), vitamin B2 (riboflavin), vitamin B3 (niacin). pia kuna vitamin C, k na B6 na B5. kwa ufupi ukwaju ni katika matunda ya asili yalotumiwa na watu toka zamani sana.
Katika ukwaju kuna polyphenols kama vile flavonoids ambayo husaidia katika kudhibiti kiwango cha cholesterol na triglycerides. Antioxidant zilizomo kwenye tunda hili husaidia katika kulinda mwili dhidi ya maradhi ya moyo. Pia ukwaju husaidia katika kutengeneza dawa za malaria.
Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa ukwaju husaidia katika kupunguza uzito. Itambulike kuwa kuzidi uzito mwilini kunahusianishwa sana na maradhi ya moyo, ini, na figo. Hivyo ukwaju husaidia katika kupunguza choloesterol mbaya (LDL) na husaidia katika kuongeza cholesterol nzuri (HDL).
Ukwaju una potassium bitartipate ambayo hii husaidia katika upatikanaji wa choo na kuzuia kuganda kwa choo. Mizizi na maganda ya mkwaju husaidia sana kwa maumivu ya tumbo. Uw.epo wa procyanidins kwenye ukwaju husaidia katika kulinda ini dhidi ya uharibifu. Pia ukwaju hutumika katika kutibu alongβatwa na nyoka.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Kitau cha Fiqh π2 ai web app π3 Kitabu cha Afya π4 Bongolite - Game zone - Play free game π5 kitabu cha Simulizi π6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Faida za kula Nazi
Nazi ni katika matunda bora sana kiafya, Soma faida zake kwa afya yako
Soma Zaidi...Chungwa (orange)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula chungwa/orange
Soma Zaidi...Vyakula vya kupambana na saratani
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya kupambana na saratani
Soma Zaidi...Vyakula vya vitamin E
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya vitamin E
Soma Zaidi...