FAIDA ZA VITAMINI C NA UMUHIMU WA VITAMINI C MWILINI
Utafahamu faida za vitamini C mwilini pamoja na kujuwa umuhimu wa vitamini C

FAIDA ZA VITAMINI C MWILINI
Kama tulivyokwisha kuona vyakula vya vitamini C kama vile papai, machungwa, mananasi, maembe, malimao na ndimu. Pia tuliona baadhi ya kazi za vitamini C ambazo ni kusaidia katika kuuwa kemikali mbaya mwilini, kuipa nguvu miili yetu ya kupambana na maradhi. Katika makala hii nitakwenda kukujuza umuhimu wa vitamin C katuka mwili wa kila kiumbe akiwemo binadamu.
Faida na umuhimu wa vitamini C
1.Hulinda mwili dhidi ya maradhi ya kiseyeye (scurvy): Haya ni maradhi ambayo hufanya mwili uweze kutoa damu kwenye mafinzi, mwili kuchubuka kwa urahisi, kuchelewa kupona kwa majeraha. Kusoma zaidi kuhusu ugonjwa huu pitia zaidi makala zetu.
2.Kulinda mwili zidi ya maambukizi na mashambulizi:
Tafiti mbalimbali zilizofanya zinaonesha kuwa vitamini C inaweza kusaidia kupunguza nguvu za virusi waletao mafua na homa ya mafua. Baadhi ya tafiti zinadiriki kusema kuwa vitamini hivi kuponyesha mafua yaa kwa haraka, lakini ambalo halina shaka ni kuwa vitamini c vinaweza kupunguza kupata mafua ya mara kwa mara au kufanya mafua yaondoke kwa haraka.
3.Vitamini C ni muhimu sana katika mfumo wa kinga mwilini. Kwani vitamini C husaidia katika Antimicrobial yaani katika kuzuia vijidudu shambulizi mwilini kama bakteria na virusi, pia vitamini C husaidia katika Natural killer cell yaani katika kuuwa vijidudu shambulizi ama kuvizuia visiendelee kukua mwilini, pia vitamini C husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga kwa kuimarisha seli hai nyeupe ziitwazo lymphocyte hizi ndizo seli ambazo askari mkuu wa mwili dhidi ya vimelea vya maradhi kama virisi, fangasi, protozoa na bakteria.
4.Kulinda miili yetu dhidi ya saratani (cancer):
Tafiti mbalimbali zimefanywa kuhusu aina ya saratani na zinavyohusiana na vitamini C kama saratani ya matiti na mapafu. Ijapokuwa tafiti hizi hazikuweza kuthibitisha moja kwa moja kuwa vitamini C vinasaidia kuondoa saratani hizi kalaki kuna mambo ambayo tafiti hizi yametufungua mawazo:
A. Vitamini C husaidia kuborsha afya na kuishi vyema kwa wagonjwa wa saratani
B. Vitamini C inaweza kuuwa seli zinazotengeneza uvimbe wa saratani
5.Husaidia kulind miili yetu dhidi ya maradhi yanayohusu mishipa ya damu na moyo (cardiovascular)
6.Husaidia kulinda miili yetu dhidi ya maradhi ya ubongo na kusahasahau
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 ai web app 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 web hosting 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
JITIBU KWA TANGAIZI: faida za kiafya za tangaizi
Tangaizi ni katika mimea yenye asili na bara la asia hususan nchi ya China.
Soma Zaidi...Maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kulia, sababu zake na dalili zzake
Hapa utajifunza sababu za kupatwa na maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kulia
Soma Zaidi...Naombakujua kujua Kama huu uyoga unasaidia kansa Kama kwawazee
Mpaka sasa hakuna dawa ya kuponyesha saratani wala kinga ya saratani. Hata hivyo vipo vyakula ambavyo vinakadiriwa kuwa hupunguza hatari ya kuweza kupata saratani. Je unadhani uyoga ni moja ya vyakula hivyo?
Soma Zaidi...Vuvimbiwa na kujaa gesi tumboni (Bloating): Jinsi ya kuepuka.
gesi tumboni husababishwa na kile tunachokula, jinsi tunavyokula, au hata hewa tunayomeza bila kujijua. Makala haya yanakupa njia za vitendo za kurejesha utulivu tumboni mwako.
Soma Zaidi...Lishe sahihi kwa wazee: Nini cha kuzingatia?
Kadiri tunavyozidi kuzeeka, mwili wetu hubadilika. Hitaji la nishati hupungua, lakini hitaji la virutubisho hubaki juu—au hata kuongezeka. Lishe sahihi katika uzee sio tu kwa ajili ya "kushiba," bali ni kinga dhidi ya magonjwa, njia ya kudumisha nguvu za misuli, na ufunguo wa kuishi kwa heshima na afya njema. Makala haya yanakupa mwongozo wa mambo muhimu ya kuzingatia katika kula kwa afya katika umri wa utu uzima.
Soma Zaidi...