Matunda ya zamani na ya asili, zijuwe faida za kiafya za tango
17.Tango (coccumber).
Tango ni katika mimea jamii ya matikiti na maboga. Tango ni katika matunda ambayo unatakiwa uyale sana kwenye maisha yako. Tafiti zinaonesha kuwa asilimia 95 ya tango ni maji. Tango lina vitamin K, B vitamins, copper, potassium, vitamin C, na madini ya manganese.
Tango lina anti-inflammatory flavonol ambayo huitwa fisetin. Hii husaidia katika kuimarisha afya ya ubongo. Hii husaidia katika kutunza kumbukumbu na kuimarisha afya ya mfumo wa fahamu pamoja na neva.
Tafiti zinaonesha kuwa tango lina polyphenols ambazo huitwa lignans (pinoresinol, lariciresinol, and secoisolariciresinol), husaidia katika kuzuia kupata aina mbalimbali za saratani (cancer) kama saratani ya kizazi kwa wanaume na wanawake.
Tango pia lina antioxidant flavonoids, kamavile quercetin, apigenin, luteolin, na kaempferol, ambazo husaidia katika kupambana na maradhi kama saratani na maradhi mengineyo.
Tango hupunguza joto tumboni, pia huondoa bajteria wanaoleta harufu mbaya mdomoni. Tafiti zinathibitisha kuwa tango husaidia katika kuondoa misongo ya mawazo na hii ni kutokana na uwepo wa vitamin B1, vitamin B5, and vitamin B7 (biotin) kwenye tango.
Tango huimarisha afya ya moyo na kupumguza shinikuizo la damu. Tanago husaidia mfumo wa kumengβenya chakula ufanye kazi kwa ufanisi. Tango husaidia katika kuthibiti uzito wa mwili.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Tangaizi ni katika mimea yenye asili na bara la asia hususan nchi ya China.
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukueleza faida za kula maboga, na mbegu zake kwa afya yako
Soma Zaidi...unayopaswa kuyajuwa kuhusu protini na vyakula vya protini, faida zake na hasara zake. Madhara ya kiafya yanayohusiana na protini pamoja na kuyaepuka madhara hayo
Soma Zaidi...Some Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula mihogo
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kazi kuu tatu za vitamini C
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya vitamin E
Soma Zaidi...Post hii itakwenda kukufundisha faida za kiafya za kula asali
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula magimbi
Soma Zaidi...