picha

Kazi za virutubisho vya protini mwilini

Somo hili linakwenda kukuletea kazi za virutubisho vya protini mwilini

KAZI ZA VIRUTUBISHO VYA PROTINI MWILINI

 

 

Kwa kuwa sasa tunajua vyanzo vya protini sana ni vyemna tukaziona kazi za protini ndani ya miili yetu. Waandishi wengi wamekuwa wakiandika kazi za protini, na kuziorodhesha katika kazinyingi. Lakini katika makala hii itakuletea kazi zilizo kuu za protini.

 

1.Kujenga mwili; protini huhusika katika kujenga mwili, na uponaji wa vidonda na majeraha. Mwili kukua vyema na kujengenka vyema protini inahitajika katika kuhakikisha hili linafanyika. Ulaji wa protini ya kutosheleza uanaweza kuufanya mwili uwe katika umbo jema na lililojengeka vyema. Endapo mwili utapata majeraha protini itahusika katika kuziba majeraha na vidonda katika eneo husika. Kama wanavyosema mwili haujengwi kwa matofali, lakini unaweza kusema kuwa protini ndio tofali la kuujenga mwili.

 

2.Hutumika katika kutengeneza antibodies; hizi ni chembechembe za protini zinazopatikana kwenye damu. Chembechembe hini ni muhiu sana katika mfumo wa kinga. Hizi huweza kuulinda mwili dhidi ya mashambulizi ya maradhi na watutu waletao maradhi. Protini inahitajika ili kutengenezwa kwa chembechembe hizi kufanyike. Hivyo unaweza kusema kuwa protini ni muhumu katika mfumo wa kinga mwilini.

 

3.Utengenezwaji wa hemoglobin; hemoglobin ni aina za protini, na hii huhusika katika usafirishaji wa hewa ya oksijen na kabondioxide ndani ya miili yetu. Hemoglobin ni chembechembe ambazo ninakazi ya kuchukuwa hewa ya okijeni baada ya mtu kuivuta na kuipeleka kwenye moyp ambapo husambazwa, kwenda maeneo mengine. Kisha hemoglobinhukusanya hewa chafu nyenye kabondaiyokasaidi na kuipeleka kwenye mapafu. Ijapokuwa hemoglobin ni chembehembe za protini lakini pia imetokana na madini ya chuma. Upungufu wa madini ya chuma unaweza kuathiri mfumo wa damu.

 

4.Utangenezwaji wa enzymes. Hizi ni chembechembe zinazotambulika kama biological catalyst, yaani ni vichochezi vya kuchochoea michakato ya kikemikali iendelee kufanyika ndani ya miili etu. Enzymes huchukuwa nafasi kubwa katika kumenge’enya chakula katika hutau zote na katika maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Enzmes zinaweza kupatikana mdomoni, tumboni na katika utumbo mdogo. Umeng’enywaji wa chakula ili tupate vurutubisho enzymes hutumika.

 

5.Utengenezwaji wa homoni; ili mwili uweze kutengeneza homoni unahitaji protini. Homoni ni chembechembe za kikemikali ambazo husaidia katika kufanya kazi nyingi na tata mwilini. Utengenezwaji wa mayai kwa wanawake na mbegu za uzazi kwa wanaume unahitaji homon. Urekebishwaji wa sukari pia unahitaji homoni. Ilijasho liweze kutoka homoni huhusika katika kurekebisha joto mwilini. Homoni zinakazi nyingi sana mwilini. Lakini jambo la msingi kufahamu hapa ni kuwa homoni hutengenezwa kwa protini.

 

6.Utengenezwaji wa nywele na vinyweleo na kope pia hutokana na protini. Kama nilivyotangulia kukueleza kuwa protini ni matofali ya kuijenga miili yetu na hii ndio maana yake. Hata nywele zetu kama hatutapata protini ya kutosha katu huwezi kuna na nywele nzuru, na zenye afya ya kutosheleza. Nywele zinaweza kuwa katika hali isiyo ya kawiada ka hutapata protini ya kutosha.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Views 1337

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Dua za Mitume na Manabii     👉3 ai web app     👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zinazofanana:

Vyakula vya kupunguza presha ya kupanda

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula ambavyo vinaweza kupunguza presha ya kupanda

Soma Zaidi...
Faida za kula mayai

Posti hii inahusu zaidi faida anazozipata mtu anayekula mayai hasa wakati wa kifua kinywa, tunajua wazi kuwa mayai yana kiwango kikubwa cha protini pamoja na hayo kuna faida nyingi za kutumia mayai hasa wakati wa asubuhi kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
Umuhimu wa kutumia maembe kiafya.

Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kutumia maembe kiafya, tunajua wazi kuwa maembe ni tunda ambalo lina umuhimu kwenye afya na uwa na vitamini C kwa hiyo tunapaswa kujua faida zake kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
Asili ya Madini ya shaba

Posti hii inahusu zaidi asili ya madini ya Shaba, ni sehemu ambapo madini ya Shaba yanaweza kupatikana ni katika mimea na wanyama

Soma Zaidi...
Faida za kula Zaituni

Matunda ya zamani, matunda ya asili, Zaituni tunda lipendezalo, zijuwe faida zake leo

Soma Zaidi...