Pera ni tunda bora lakini pia ni dawa, tambua umuhimu wa tunda hili kiafya
Pera ni katika matunda yanayopatikana maeneo mengi duniani. Tunda hili ni katika matunda yenye kutia afya zaidi katika miili yetu hasa kwa wale wenye maradhi sugu. Tunda hili hutumika mapaka majani yeke na kuleta faida nyingi sana. Hata wazee wetu wa zamani walikuwa wakitumia mmea huu kwa ajili ya tiba asili. Sasa hebu tuanze kuziona faida hizo:-
Katika tafiti iliyofanyiwa watu 19 imethibitisha kuwa kunywa majimaji yatokanayo na majani ya mpera husaidia katika kushusha kiwango cha sukari na athari hii huweza kuendelea mpaka masaa mawili. Tafiti nyingine aliyofanyiwa watu 20 wenye aina ya kisukari type 2 diabetes waliligundulika kuwa kunywa majani ya mpera kumeshusha sukari kwa asilimia 10%.
Pia kiwango cha madini ya potassium (chumvi) iliyomo kwenye pera pamoja na kambakamba zilizomo kwenye pera husaidia katika kuimarisha afya ya moyo. Pia ulaji wa mapera unaweza kuondoa cholesterol zilizo mbaya (LDL cholesterol) na kuongeza cholesterol nzuri). Hivyo hupunguza nafasi ya kupata maradhi ya shinikizo la damu la juu yaani presha ya kupanda na kupata kiharusi yaani kupalalaizi. (stroke).
Tafiti iliyofanyiwa wanawake 197 ambao huwa wanapata maumivu wakati wa kupata sikuzao, tafiti imeonesha kuwa unywaji wa miligram 6 za maji ya majani ya mpera husaidia kupunguza maumivu haya. Pia utafiti zaidi umeonesha kuwa majani ya mpera husaidi kupunguza maumivu haya mara dufu tofauti na kutumia dawa za kupunguza maumivu. Pia tafiti zinaonesha kuwa majani ya mpera hupunguza maumivu wakati wa kukojoa kwa wale wanaopata maumivu haya.
Pia majani ya pera yakitengenezwa majimaji yake husaidia katika kuboresha afya ya mfumo mzima wa mmeng’enyo wa chakula. Kwa wale wenye tatizo la kuharisha majani ya mpera ni mujarabu sana katika kuondoa ama kupunguza tatizo. Pia kuna tafiti nyingi zinaonesha kuwa pera husaidia katika kuuwa vijidudu vibaya ndani ya matumbo yetu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula kisamvu
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna nzuri ya kuandaa mchai chai kwa ajili ya matumizi mbalimbali, Ili kutumia mmea wa mchai chai zifuatazo ni mbinu za kuandaa mmea huu.
Soma Zaidi...Matunda ya zamani, matunda ya asili, Zaituni tunda lipendezalo, zijuwe faida zake leo
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kunywa chai
Soma Zaidi...Je! unatambuwa madhara ya vyakula vya protini na mafuta? ungana nasi kwenye somo hili
Soma Zaidi...Tezi za lymph huanza kuonyesha dalili za kuwa mwili upo katika mapambano dhidi ya vijidudu vya maradhi. Ishara ni pale utakapoona tezi za lymph zina maumivu. Tezi hizi hupatikana kwenye mapaja, kwapa nashingo.
Soma Zaidi...