Je, utamsaidia vipi mtu aliyeumwa na nyuki?
Posti hii inazungumzia kuhusiana na kumsaidia mwenye aliyeumwa na nyuki.nyuki na wadudu ambao wakikushambulia Sana na ukikosa msaada unaweza kufa au kuwa katika Hali mbaya.
Mtu aking'antwa na nyuki Kuna dalili ambazo huonekana Kama vile
1.kuvimba .
2.mapigo ya moyo kuenda haraka.
3.maumivu Tena maumivu haya huwa Ni makali Sana endapo umeshambuliwa na nyuki wengi.
4.kupoteza fahamu. Hii hutegemea na ulivyong'atwa
5.kuwa na kizunguzungu.
6.kichwa kuuma.
8.mwili kuwasha hii unaweza isitokee kwa wote kwasababu hutegemeana na mzio (allergy) wa mtu
Huduma ya kwanza kwa aliyeng'ntwa na nyuki.
1.linda usalama wako na usalama wa mgonjwa.hii husaidia ili na wewe unayemtoa usije ukang'atwa kwahiyo kabla ya yote unatakiwa kujiweka Safi.
2.mtoe kwenye Hilo tukio; baada ya hapo unamwondoa mgonjwa kwenye Hilo tukio ili kumsaidia asiendelee kung'antwa na nyuki.
3.mweke sehemu Safi yenye hewe na Kama inawezekana mweke penye baridi .
4.angali Hali ya mgonjwa Kama amepoteza fahamu kiasi kwamba ukimwita Kama anaitika, Kama anasikia maumivu ili ujue mgonjwa Yuko katika Hali gani.
5.angali mgonjwa Kama anapumua na mapigo ya moyo Kama yapo Kama hayapo mwahishe mgonjwa hospitalini.
6.mwondoe ncha za nyuki kwa kutumi kitu chenye ncha Kali Kama vile sindano,Pini n.k na kifaa hiko kiwe Ni kisafi hakijawahi kutumiwa na mtu yoyote ili kumwepusha asipate Magonjwa mengine na pia kumsaidia mgonjwa kuwa katika Hali nzuri.
7.mwekee barafu kwa kukandamiza ili Kupunguza au kuondoa uvimbe na maumivu na usikandamize Sana dakika kumi zinatosha maana ukikandamiza mda mrefu hupelekea kupata oedema.
8.kama unadawa za maumivu mpatie mgonjwa ili Kupunguza maumivu.
9.Angalia mabadiliko ya mgonjwa, ikiwa hayajabadilika mpeleka mgonjwa kituo Cha afya.
Mwisho; Kuna mambo muhimu ya kuangalia wakati mtu ameng'atwa na mdudu . utaangalia Kama hewa ipo, anapumua na mapigo ya moyo.kingine angalia Hali ya mgonjwa Kama anajielewa au hajielewi .
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 web hosting 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Maumivu ya kifua yanayosababishwa na kupungua kwa mtiririko wa Damu kwenye moyo.
 Maumivu ya kifua yanayosababishwa na kupungua kwa mtiririko wa damu kwenye misuli ya moyo, kitaalamu huitwa Angina ni dalili ya Ugonjwa wa ateri ya Coronary. Ugonjwa huu kawaida hufafanuliwa kama kufinya, shinikizo, uzito, kubana au maumivu kwenye
Soma Zaidi...Umuhimu wa kupima virus vya ukimwi kwa wajawazito na wanaonyonyesha
Post hii inahusu umuhimu wa kupima virus vya ukimwi kwa mama wajawazito na wanaonyonyesha. Ni hatua ya kupima Mama akiwa mjamzito na wakati wa kunyonyesha ili kuepuka hatari ya kumwambikiza mtoto
Soma Zaidi...Zijue kazi za uke (vagina)
Uke ni sehemu ambayo imo ndani ya mwili wa mwanamke, sehemu hii ufanya kazi mbalimbali hasa wakati wa kujamiiana, kubarehe na kujifungua kwa mama.
Soma Zaidi...Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na shambulio la moyo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na shambulio la moyo
Soma Zaidi...Faida za seli
Posti hii inahusu zaidi faida za seli. Seli ni chembechembe hai za mwili ambazo hufanya kazi mbalimbali katika mwili wa binadamu.
Soma Zaidi...Njia za kuingiza chanjo mwilini
Posti hii inahusu njia mbalimbali ambazo utumika kupitisha chanjo, njia hizo utegemea na kazi ya chanjo kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...