Na tukiutafiti Uislamu kwa makini kama mfumo kamili wa maisha tunaona unadhihiri ukweli wa aya hii ya Qur-an.
Na tukiutafiti Uislamu kwa makini kama mfumo kamili wa maisha tunaona unadhihiri ukweli wa aya hii ya Qur-an. Uislamu unatoa mwongozo wa maisha haya na ya akhera na hakuna jambo lililo muhimu katika kumuongoza mwanaadamu
lisilokuwemo katika mwongozo aliokuja nao Muhammad (s.a.w). Hivyo hoja ya kuhitaji Mtume ili aje kukamilisha dini pia inaondoka.
Hata hivyo kuna baadhi ya watu wanaosema kwamba kupita tu kwa muda mrefu ni sababu ya kuhitaji Mtume mwingine. Hii ni kwa sababu wanasema mwongozo ulioletwa karne 14 zilizopita ni wa kale mno kiasi kwamba hauwezi kukidhi mahitaji ya watu wa leo. Mawazo haya hayana msingi kabisa, kwa sababu zifu atazo:
(i)Mafunzo ya Uislamu ni ya milele, kwa sababu ni ufunuo utokao kwa Mwenyezi Mungu mjuzi wa yote ya kale, ya sasa na yajayo, tena basi mwenye uhai wa milele. Elimu ya binaadamu ndiyo yenye ukomo, na ni jicho la binaadamu ambalo haliwezi kuona hata kesho achilia mbali miaka milioni mmoja ijayo. Elimu na hikima ya Mwenyezi Mungu imesalimika na upungufu kama huo.
(ii)Uislamu umeegemeza mafundisho yake juu ya umbile la binaadamu. Na umbile la binaadamu limesalia vile vile katika zama zote. Watu wote wamejengwa kwa majengo yale yale yaliyowajenga watu wa kale kabisa na hivyo umbile lao kimsingi ni lilelile.
(iii)Katika maisha ya binaadamu kuna mizani inayoridhisha kabisa baina ya mambo yanayodumu na mambo yanayobadilika. Misingi muhimu na maadili makuu hayabadiliki na sura ya nje ndiyo inayoweza kubadilika kutokana na kupita kwa muda.
Qur-an na sunna zinatoa kanuni au misingi ya kudumu na kwa kutumia ijitihadi misingi hiyo inaweza kutekelezwa kadri hali itakavyobadilika.
Uislamu ndio dini pekee iliyoweka utaratibu madhubuti unaoweza kuoanisha maendeleo ya binaadamu na misingi ya Kitabu cha Allah (s.w) na Sunnah ya Mtume wake Muhammad (s.a.w).
Na tukirudi katika lile sharti letu la tatu kuhitajia kuletwa Mtume mwingine, tunaona kuwa Muhammad (s.a.w) hakuletwa kwa taifa au watu maalum bali kwa walimwengu wote.
Qur-an in as em a:“Sema (Ewe Nabii Muhammad): “Enyi w atu! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi nyote”. (7:158)“Nasi hatukukutuma ila uwe rehema kwa walimwengu wote.” (21:107).
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Nao husema (kwa maskhara): "Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya?
Soma Zaidi...Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Lengo tarajiwa la Muhtasari huu ni kutuwezesha kuzibaini fika sifa za Waumini zilizoainishwa katika Qur'an, kisha kujipamba nazo ili tuwe waja wema watakaorehemewa na kuridhiwa na Allah (s.
Soma Zaidi...Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu nuzo 6 za imani ya uislamu na pia utajifunz akuhusu mafunzo yanayoweza kupatikana kwenye Nguzo hizi.
Soma Zaidi...Huwaoni wale wanaodai kwamba wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako?
Soma Zaidi...