Jinsi ambavyo mtu anazuiliwa kurithi mali ya marehemu

Endapo mtu yupp katika orodha ya wanaotakiwa kutithi, anaweza kuzuiliwa kurithi kwa kuzingatia haya.

Kuzuiliana
Tumeona kuwa wanaume wenye kurithi ni 15 na wanawake wanaorithi ni 10. Lakini wote hawa 25 wakikutana pamoja hawawezi kurithi wote bali baadhi yao huwazuilia wengine wasipate kitu au wasipate fungu kubwa. Katika kipengele hiki tunaonyesha wanaozuiliwa na wasiozuiliwa.

 


1.Mtoto mwanamume hazuiliwi na mtu.
2.Mjukuu huzuiliwa na mtoto mwanamume na kila mtoto wa kiume aliyeko mbali huzuiliwa na aliyoko karibu na marehemu. 3.baba hazuiliwi na mtu.
4.Babu wa upande wowote huzuiliwa na baba au babu wa karibu zaidi (kama vile baba yake baba humzuilia babu yake baba).
5.Ndugu wa kwa baba huzuiliwa na ndugu wa kwa baba na mama; na kila amzuiliaye yeye (huyo ndugu wa kwa baba na mama) vile vile huzuiliwa na dada wa kwa baba na mama akiwa pamoja na binti au binti wa mtoto wa kiume (mjukuu) au wote wawili.
6.Ndugu wa kwa mama huzuiliwa na mtoto au mtoto wa mtoto mwanamume au baba au babu.
7.Mume hazuiliwi na mtu wala
8.Mke hazuiliwi na mtu.
9.Binti hazuiliwi.
1O.Mama hazuiliwi.
11.Bibi huzuiliwa na mama.

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1127

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰2 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    ๐Ÿ‘‰4 Madrasa kiganjani    ๐Ÿ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    ๐Ÿ‘‰6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Dhamana ya Kuchunga Ahadi Katika Uislamu

Kuchungaย au kutekelezaย ahadiย ni miongoni mwa vipengele muhimu vya tabia ya muumini wa kweli.

Soma Zaidi...
Ni nini maana ya twahara na kujitwaharisha?

Posti hii inakwendabkukujiulisha maana ya twahara na jinsi ya kujitwaharisha.

Soma Zaidi...
NAMNA YA KUCHINJA KATIKA UISLAMU

ุนูŽู†ู’ ุฃูŽุจููŠ ูŠูŽุนู’ู„ูŽู‰ ุดูŽุฏูŽู‘ุงุฏู ุจู’ู†ู ุฃูŽูˆู’ุณู ุฑูŽุถููŠูŽ ุงู„ู„ู‡ู ุนูŽู†ู’ู‡ู ุนูŽู†ู’ ุฑูŽุณููˆู„ู ุงู„ู„ูŽู‘ู‡ู ุตู„ู‰ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆ ุณู„ู… ู‚ูŽุงู„ูŽ: "ุฅู†ูŽู‘ ุงู„ู„ูŽู‘ู‡ูŽ ูƒูŽุชูŽุจูŽ ุงู„ู’ุฅูุญ...

Soma Zaidi...