Mambo yanayoharibu swala yaani yanayobatilisha swala.

Post hii itakufundisha mambo ambayo yatasababisha swqla yako isikubaliwe.

Mambo yanayobatilisha Swala

Mtu akiwa katika swala yuko katika hali maalum na haruhusiwi kufanya kitu kingine nje ya swala hata vile vitendo vya kawaida alivyovizoea. Hivyo ukiwa ndani ya swala ukifanya au kukitokea moja ya mambo yafuatayo, swala yako itakuwa imebatilika na itabidi uanze upya.

 


(a) Kutoelekea Qibla kwa kifua pasi na dharura yoyote ya kisheria. (b) Kupatikana na hadathi kubwa, ndogo au ya kati na kati.


(c) Kufikwa na najisi mwilini, nguoni au mahali pa kuswalia.


(d) Kuvukwa na nguo ukawa uchi. Wanaume wanaovaa shati fupi wajihadhari sana hapa kwani,hasa wakati wa kurukuu na kusujudu, migongo yao (viuno vyao) chini ya usawa wa kitovu (panda za makalio) huwa wazi na hivi huhesabiwa kuwa wako uchi.


(e) Kusema au kutamka makusudi lau herufi moja yenye kuleta maana nje ya maneno ya swala.Mtume (s.a.w) amesema: gHakika ya hii swala, haifai ndani yake maneno ya watu kwani swala yenyewe ni Tasbih, Takbir na kusoma Qur-an. (Muslim).


(f) Kula au kunywa japo kwa kusahau. (g) Kufanya jambo lisilowiana na swala mfululizo mara tatu. (h) Kuiacha nguzo yoyote ya swala. 


(i) Ukizidisha nguzo yoyote ya swala makusudi.
(j) Kumtangulia Imam au kuchelewa kwa nguzo mbili za kimatendo kwa makusudi.
(k) Kutia nia ya kuikata swala au kujishauri moyoni kuwa uikate au usiikate swala.
(l) Kuwa na shaka kuwa umetimiza au hujatimiza sharti au nguzo yoyote ya swala.
(m) Kupotewa na akili au kulala ndani ya swala.
(n) Kutoa Salaam kwa makusudi kabla ya kwisha swala.
(o) Kuswalishwa na asiyekuwa Muislamu.
(p) Kukhalifu utaratibu wa nguzo za swala, yaani kutangulia kutekeleza nguzo ya swala kabla ya kutekeleza nguzo inayostahiki kutangulia katika utaratibu wa swala.
(q) Kuleta dua ya kuomba kitu haramu au muhali.
(r) Kumshirikisha Allah (s.w) katika kuleta dua yaani kuleta dua ya kuomba kitu cha halali lakini humuombi Allah (s.w) peke yake.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1725

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Ni zipi najisi katika uislamu

Post hii inakwenda kukupa orodha ya vitu vilivyo najisi.

Soma Zaidi...
Nini maana ya funga na ni lipi lengo lake

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu lengo la funga na maana yake katika uislamu.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kuoga josho la kiislamu ( janaba, hedhi na nifasi)

Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kuoga josho kisheria.

Soma Zaidi...
Kwa nini imefaradhishwa kufunga mwezi wa Ramadhani

Unaweza kijiuliza ni kwa nini hasa kimepelekea kufaradhishwa kufunga mwezi wa Ramadhani.

Soma Zaidi...
Namna ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa.

Post hii inakwenda kukugundisha jinsi ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa.

Soma Zaidi...