MAGONJWA YA INI NA DALILIZAKE, NA KUKABILIANA NAYO
Ini ni katika viungo vikuu katika mwili wa binadamu. Ni katika viungo vichache ambavyo vikikatwa vinaweza kujirudisha, yaani kukuwa. Ini ni katika viungo vinavyo shambuliwa na vimelea vya maradhi mbalimbali pamoja na sumu za vyakula. Ini mwilini husaidia katika mmengenyo wa chakula, na kuondoa sumu za vyakula mwilini. Endapo ini litadhurika kwa namna yeyote ile afya ya mtu katu haitakuwa salama, na athari zake endapo zitachelewa kupatiwa matibabu hupelekea kifo.

Katika makala hii tutakwenda kuyaona baadhi ya maradhi ya ini, dalili zake na njia za kukabiliana nayo. Kuwa nasi kwenye makala hii, na wasambazie wengine uwapendao, kulinda afya zao. Makala kama hizi na nyinginezo utazipata kwenye tovuti yetu www.bongoclass.com

Maradhi yanayoshambulia figo yapo mengi sana, na yapo ambayo hurithiwa na mengine hayarithiwi. Na yapo ambayo huambukizwa na mengine hayaambuizi. Ifuatayo ni orodha ya maradhi ya ini:-SABABU ZA KUTOKEA KWA MARADHI YA INI:
Ili tuone sababu hizo kwanaz atuone aina za maradhi ya ini. Na himo kwenye aina hizo ndipo utakapojua ni sababu ipi imesababisha maradhi hayao:-

A. Maradhi ya ini yanayosababishwa na maambukizi
Maradhi ya ini yanayosababishwa na maambukizi yanajulikana kama homa ya heatitis. Homa hii husababishwa na virusi wanaotambulika kama hepatisis viruses. Miongoni mwa virusi hao ni:-
1.hepatitis A
2.Hepatitis B
3.Hepatitis CB. Maradhi ya ini yanayosababishwa na mashambulizi ya mfumo wa kinga mwilini, kushambulia seli za ini. Kitaalamu hutambulika kama immune system Abnomality au Autoimune. Maradhi ya ini yanayosababishwa kwa njia hii ni:-
1.Autoimmune hepatitis
2.Primary biliary cirhosis
3.Primary sclerosing cholangitis
C. Maradhi ya ini yanayosababishwa kwa kurithi
Unaweza kurithi maradhi ya ini kutoka kwa wazazi wako ,ima mmoja wapo ama kwa wote. Maradhi ya ini yanayosababishwa na kurithi ni:-
1.Homochromatosis
2.Hyperoxaluria na oxalosis
3.Wilson’s diseasesD. Maradhi ya ini yanayosababishwa na saratani (cancer)
1.saratani ya ini
2.Saratani ya nyongo
3.Kuvimba vya iniDALILI ZA MARADHI YA INI
Katika maradhi yote tulioyataja hapo juu, ynashirikiana kwa pamoja katika dalili zifuatazo:
1.macho na ngozi kuwa na rangi ya njano.
2.Maumivu yasiyo ya kawaida yanayoendana na kuvimba mwili
3.Kuvumba kwenye miguu na vifundo vya miguu (ankles)
4.Kuuma kwa ngozi
5.Mkojo kuwa na rangi nyeusi ama giza
6.Kupata choo chenye rangi kupauka, ama kuwa na damu
7.Uchovu mkali sana na usio wa kawaida
8.Kichefuchefu na kutapika
9.Kukosa hamu ya kula
10.Ngozi kuchubuka kwa urahisi.MAMBO YANAYOHATARISHA AFYA YA INI NA KULETA MARADHI YA INI
1.unywaji wa pombe kupitiliza
2.Kujidunga sindano kwa kushirikiana
3.Uwekaji wa tatuu
4.Kuongezewa damu
5.Muingiliano wa majimajin ya mwili na damu
6.Kupanya ngono zembe
7.Kisukari
8.Kuzidi kwa uzitoVIPI UTAWEZA KUZUIA MARADHI YA INI
1.Punguza unywaji wa pombe
2.Jiepushe na tabia hatarishi kama kujidunga masindano, kushirikiana vitu vya ncha kali, ngono zembe n.k
3.Pata chanjo ya baadhi ya maradhi ya ini kama hepatitis
4.Ilinde ngozi yako
5.Hakikisha huna uzito wa kuzidi
6.Fanya mazoezi
7.Unapopuliza dawa za wadudu vaa kitambaa puani (mask)