Uendeshaji wa dola ya uislamu madinah

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

. Uendeshaji wa Dola ya Kiislamu Madinah.

Dola (Serikali) ya Kiislamu Madinah ilipata mapato yake kupitia njia zifuatazo;

 

  1. Zaka na Sadaka ndio ilikuwa njia kuu ya kukusanya mapato ya serikali (Dola) ya Kiislamu iliyowahusu waislamu wote wenye uwezo.

 

  1. Jizya – Ni kodi waliokuwa wanalipa wasiokuwa waislamu wanaume tu wenye uwezo wa kuwa askari kwa ajili ya ulinzi wa Dola.

 

  1. Al-Kharaj – Ni kodi waliolipa wasiokuwa waislamu, walio na mashamba katika Dola ya Kiislamu.

 

  1. Al-fay – Ni mapato yanayotokana na mashamba ya Serikali (Dola) ya Kiislamu Madinah.

 

  1. Al-Ghanimah (Ngawira) – Ni mapato yanayotokana na mali ilitekwa katika vita, iliyolipwa 1/5 ya mali yote ilyotekwa.

 

  1. Ushr – Ni kodi (ushuru) iliyotolewa na waislamu wenye ardhi katika Serikali (Dola) ya Kiislamu kwa kiwango cha 10% kwa maji ya asili (mvua) na 5% kwa maji ya kumwagilia.

 

  1. Zaraib – Ilikuwa ni kodi zilizotozwa na serikali (Dola) ya Kiislamu kwa muda kwa ajili ya maslahi ya nchi.

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1562

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana: