Navigation Menu



image

KIKAO CHA KUMFUKUZA MTUME MUHAMMAD KUTOKA MAKKAH (MAKA), KIKAO ALICHOHUDHURIA IBLISI

KIKAO CHAKALIWA KUJADILI HATMA YA MUHAMMAD KATIKA MJI WA MAKAHiki ni kikao kizito hakijapata kutokea toka muhammad katika ji wa maka.

KIKAO CHA KUMFUKUZA MTUME MUHAMMAD KUTOKA MAKKAH (MAKA), KIKAO ALICHOHUDHURIA IBLISI

KIKAO CHAKALIWA KUJADILI HATMA YA MUHAMMAD KATIKA MJI WA MAKA

Hiki ni kikao kizito hakijapata kutokea toka muhammad katika ji wa maka. Ni katika jimba la mikutano lililofahamika kama AN-NADWAH hii ilikuwa ndio nyumba ya bunge la watu wa maka kujadili mambo yao. Lengo kubwa ni kupunguza kasi ya kuenea kwa uislamu na kumfanya muhammad aachane kabisa na jambo hili la kutangaza dini iliyo nje ya mila zao. Na hii ilitokea pale makabila ya Aws na Khazraj walipotishia kumpokea Muhammad endapo atakwenda Yathrib (Madina).


Kiakao kilikaliwa mnamo tarehe 12 mwezi wa tisa mwaka 622 B.K au ni sawa na tarehe 26 mfunguo tano (safar) kwa mujibu wa kalenda ya kiarabu.na tukio hili lilitokea miezi miwili na nusu baada ya mkataba wa ‘Aqabah. Katika siku hiyo mkutano ulifanyika kwa umakini zaidi, umakini ambao katu haujapata kutokea kabla.


1.Mkutano huu ulihudhuriwa na watu 14 karibia kutoka katika kila kabila. Watu hawa walikuwa nai:-
2.Abuu Jahal Ibn Hisham kutoka katika kabila la Banuu Makhzumi,
3.Jabir Ibn Mut’im, Tua’aima Ibn ‘Ady na Harith Ibn ‘Amir kutoka kabila la Banuu Naufal Ibn ‘Abd Manafi
4.Watoto wawili wa Ibn Rabia nao ni Shaiba na ‘Utbah, Abuu Sufian Ibn Harb kutoka katika kabila la Banii ‘Abd Shams Ibn ‘Abd Manaaf
5.Nadhr Ibn Haarith kutoka kkabila la Banii ‘Abd Dar
6.Abuu Bakhtar Ibn Hishaam na Zam’at Ibn Aswad, na hakim Ibn Hizaam kutoka katika kabila la Banii Asad ibn ‘Abd al-’Uzaa
7.Nubiyah na Munabih watoto wa Hajaaj kutoka kabila la banii Saham
8.Umayyah Ibn Khalaf kutoka kabila la banii Jumah.


Wakati wahudhuriaji walipokusanyika nje ya mlango wa jumba hili la mikutano, ghafla akaja mzee mmoja. Mzee aliyeonekana nadhifu sana. Mzee huyu akaja hadi mlangoni, walipomuuliza ni nani wewe akajibu kuwa yeye ni mtu kutoka maeneo ya Najd na amepetakhabari juu ya mkutano huu, hivyo atawakilisha watu wa najd na kutoa mawazo yake.


Watu walipojiridhisha wakamruhusu na kwa pamoja kundi likaingia ndani. Ukweli wa mambo ni kuwa mzee huyu hakuwa ni mtu wa Najid bali alikuwa ni iblisi na alikuja ili kuhakikisha inapatikana rai itakayokuwa ni mujarabu katika kummaliza Muhammad. Basi punde baada ya watu kuingia ndani mkutano ukaanza. Rai mbalimbali zikaanza kutolewa na huku mzee wa Najd (Iblis) akawa anapangua rai hizo kwa hija zilizo madhubuti. Miongoni mwa rai hizo ni kama zifuatazo:-


A.Basi mtu mmoja a;liyetambulika kwa jina la Abuu Aswad akazungumza kuwa “tumtoeni (tumfukuzeni) Muhammad kwenye mji wetu (Makkah) na aende kokote atakakotaka na katu tusijali popote atakapokwenda, tukifanya hivyo kwa hakika tutakuwa tumesalimika na mambo yatarudi kama yalivyokuwa.


B.Basi hapo mzee wa Najd (Iblis) akasema kuwa: kwa hakika jambo hili sio salama kabisa kwenu. Akasema “hivi hamjaona jinsi yalivyo matamu maneno yake?, na utamu na ufasaha wa matamko yake, kama mkimtoa atakwenda kupata wafuasi wengine wasiokuwa nyinyi, na atakuwa na nguvu kisha atakuvamieni na kukutoeni kwenye miji yenu, na afanye atakachokitaka. Kwa hakika rai hii sio salama toeni rai nyingine isiyokuwa hii.


C.Mtu mwingine aliyefahamika kwa jina la Abuu Al-Bakhtar akasema “mfungieni kwenye chumba chenye milango madhubuti, na kisha abakie humo na yampate yele yalowapata waliotangulia kabla yenu (baada ya kupewa adhabu kama hii) mpaka mauti yamkute”


D.Baada ya kutolewa rai hii mzee wa Nadj (Iblis) akaipinga tena rai hii kwa kusema hapana hili pia si jema, kwa hakika naapa kwa Allah kuwa kama mtafanya hivyo wafuasi wake watakuja kumtoa. Watu walionekana pia kukubali wazo hilo kuwa rai hii pia sio salama. Kwani hata nduguzake wangemtoa wasingeweza kumuacha, kwani walisha mfungia kabla hapo yeye na familia yake.


E.Basi baada ya muda mkuu wa makafiri wa Makkah Abuu Jahal akazungumza “kwa hikika naapa kwa Allah kuwa njina rai ambayo hamjaitoa” watu wakasema ni ipi rai hiyo? Akasema “na tuchukuwe kutoka katika kabila mtukijana mmoja mwenye nguvu na afya njema, kisha tumpatie upanga ulio safi na mkali kisha kila mmoja katia vijana hawa akampige (Muhammad) upanga mmoja na wamuue na wakifanya hivi atakuwa ameuliwa na kabila zote za watu wa Makkah hivyo hata familia yake haitaweza kulipiza kisasi.


F.Watu walionekana kuikubali rai hii na hata mzee wa Najd (Iblis) hakuweza kuipinga rai hii hata kidogo. Na kisha akasema mzee wa Najd “hii ndio rai ambayo hakuna rai nyingine (bora zaidi) kuliko hii.

Baada ya kumaliza kikao kwa kukubaliana kutekeleza hoja ya kumuua Muhammad, watu wote walitawanyika. Vijana kutoka katika kila kabila walichukuliwa tayari kwa akwenda kummaliza Muhammad. Mambo makubwa na miujiza ya hali ya juu ilitokea, darasa lijalo tutaendelea na kipande kijacho.



                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 676


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

HISTORIA YA NABII LUTI
Soma Zaidi...

Jinsi tukio la Karatasi lilivyotokea wakati wa Mtume siku chache kabla ya kifo chake
Tukio la kartasiTukio la ‘kartasi’ lililonakiliwa katika vitabu vya Muslim na Bukhari kuwa siku tatu kabla ya kutawafu Mtume (s. Soma Zaidi...

Kuanzishwa kwa vitenge vya ulinza na Usalama, na usalama wa taifa
Soma Zaidi...

Haki na Hadhi za Mwanamke katika jamii za mashariki: China, India na Japani hapo zamani
2. Soma Zaidi...

Ghasia na chokochoko za Makhawariji na kuuliwa kwa Ally
Soma Zaidi...

Mafunzo yatokanayo na maandalizi haya ya ki ilhamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Zakaria(a.s) Akabidhiwa Ulezi wa Maryam
Baada ya kupigwa kura juu ya nani awe mlezi wa Maryam, Nabii Zakaria akachaguliwa kuwa mlezi wa Maryam. Soma Zaidi...

Mjadala juu ya ndoa ya Mtume Muhammad s.a.w na bi Khadija.
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w sehemu ya 16. Hapa utajifunza maandalizi wa mjadala wa ndoa hizi. Soma Zaidi...

Hadhi na haki za Mwanamke katika jamii za Mashariki ya Kati bara la arabu hapo zamani
Soma Zaidi...

Kuchaguliwa kwa Makhalifa wanne baada ya kutawaf (kufariki) kwa Mtume muhammad (s.a.w)
8. Soma Zaidi...

Musa(a.s) Ahamia Madiani
Mchana wa siku moja Musa(a. Soma Zaidi...

Kisa cha Israa na Miraji na kufaradhishwa swala tano
Safari ya Mi'rajKatika mwaka wa 12 B. Soma Zaidi...