Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo,ni njia ambazo mtu anaweza kutumia Ili kuzuia uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.zifuatazo ni njia zinazoweza kutumika kama mtu amepata uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.
1. Kufanya usafi baada ya kujamiiana.
Mwanamke na mwanaume wanapomaliza kujamiiana wanapaswa kufanya usafi hasa kwa mwanamke Ili kuweza kutoa bakteria ambao wanakuwa wameingia kwenye uke kwa kufat hivyo mwanamke anaweza kuepuka kuambukizwa magonjwa yanayosababisha uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, kwa hiyo ni lazima kufanya usafi baada ya kujamiiana.
2. Kuepuka kutumia sabuni za kunukia na marashi kwenye sehemu za mwili.
Kuepuka kutumia sabuni za kunukia na za Siri kwenye sehemu za Siri kwa sababu vitu kama hivyo usababisha kuua bakteria wazuri na kubakiza bakteria wabaya ambao uleta maambukizi kwenye kwa sababu bakteria wazuri wanazuia maambukizi ya Magonjwa na kubakiza wabaya ambao usababisha kila ugonjwa na hatimaye maambukizi kuongezeka, kwa hiyo kwa kutumia sabuni za kawaida hazina kemikali nyingi ambazo uharibifu bakteria wazuri .
3. Unapomaliza kukojoa tu hakikisha unasafisha vizuri Ili kuhakikisha kuwa wadudu wameisha kwenye mwili, unapomaliza kukojoa tu unapaswa kupangusa vizuri Ili kuepuka bakteria kuendelea kuwepo kwenye kibofu Cha mkojo na kuendelea kusababisha maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo.
4. Ukihisi kuwa una mkojo hakikisha unakojoa Ili kuacha hali ya bakteria kuendelea kuwepo kwenye sehemu mbalimbali za mwili, kwa sababu bakteria wakiendelea kuwepo kwenye kibofu Cha mkojo wanazaliana na kukua na baadae kuleta maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo na hatimaye kuleta uvimbe Ila tukisafisha vizuri tunaweza kuepusha magonjwa ya uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.
5. Safisha kutoka mbele kwenda nyuma.
Tunaposafisha tunapaswa kusafisha kutoka mbele kwenda nyuma Ili kuepuka kutoa bakteria kutoka kwenye sehemu za kinyesi kwenda sehemu za kibofu Cha mkojo, kwa hiyo tunapaswa kusafisha kutoka mbele kwenda nyuma kwa Sababu bakteria wa kwenye kinyesi akiungua kwenye kibofu Cha mkojo anaketa maambukizi kisha uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.
6. Daima epuka sana kuvaa nguo zilizobana kwenye sehemu za Siri kwa Sababu hewa hauwezi kupita na kusababisha bakteria kukaa kwenye sehemu mbalimbali za kibofu Cha mkojo lakini tukivaa nguo ambazo hazibani tunaruhusu hewa kuingia kwenye sehemu za Siri na bakteria wanaweza kutoka kwa urahisi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Malengelenge sehemu za siri ni maambukizi ya kawaida ya zinaa ambayo huathiri wanaume na wanawake. Makala ya malengelenge sehemu za siri ni pamoja na maumivu, kuwasha na vidonda katika sehemu yako ya uzazi. Lakini huenda usiwe na dalili au ishara za mal
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na Magonjwa yanayosababisha madhara kwenye mapafu na kitaalamu hujulikana Ugonjwa wa Acute Respiratory Distress Syndrome (ARDS) hutokea wakati Majimaji yanapojaa kwenye vifuko vidogo vya hewa nyororo (alveoli) kwenye mapafu
Soma Zaidi...Kama unasumbuliwa na presha post hii ni kwa ajili yako. Hapa tutakuoatia ushauri kutokana na swali alilouliza mdau wetu.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Kichaa cha mbwa ni virusi hatari vinavyoenezwa kwa watu kutoka kwa mate ya wanyama walioambukizwa. Virusi vya kichaa cha mbwa kawaida hupitishwa kwa kuuma.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea namna na jinsi ya kujikinga au kuzuia Ugonjwa wa ini.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu maambukizi chini ya kitovu ni madhara ambayo yanaweza kutokea kwa mgonjwa pale ambapo matibabu yanapokuwa hayatolewi kwa mgonjwa wa maumivu chini ya kitovu.
Soma Zaidi...Malaria husababishwa na vijidudu vidogo parasite wanaojulikana kama plasmodium. Vijidudu hivi hubebwa na mbu aina ya anophelesi. Kuna ina nyingi za plasmodium lakini aina 5 tu ndizo husababisha malaria
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa kusinyaa kwa Misuli. Ni maradhi yanayopelekea uzalishwaji hafifu wa misuli, hivyo kupelekea misuli kukosa protini, kushunwa kukuwa na kusinyaa.
Soma Zaidi...