Posti hii inahusu zaidi Dalili za saratani kwa watoto, ni Dalili ambazo ujitokeza kwa watoto na ikiwa mlezi au mzazi akiziona tu anaweza kutambua mara moja kwamba hii ni saratani au la na kama bado ana wasiwasi anaweza kupata msaada zaidi kutoka kwa wataa
Dalili za saratani kwa watoto wadogo.
1.Kwanza kabisa mtoto anakuwa na uvimbe usio wa kawaida na ambao hauna maumivu kwenye sehemu za mashavu, kwenye shingo, tumbo, miguuni na sehemu zozote za mwili, kwa mara ya kwanza uvimbe huu unakuwa hauna maumivu hata kidogo lakini ikiwa umetibuliwa au kuchokonolewa uvimbe huu unaweza kubadilika na kutengeneza kitu kingine na kusababisha maumivu kwa mtoto.
2. Kwa hiyo baada ya kuona uvimbe wa aina hii na mtoto anaendelea na maisha bila kuonyesha Dalili yoyote ya maumivu kwanza kabisa mtoto anapaswa kupelekwa kwa wataalamu wa magonjwa ya saratani na epuka kabisa kutingisha uvimbe huu kwa kutumia waganga wa kienyeji ambao hawana utaalamu wowote au mzazi mwenyewe kuamua kuchokonoa uvimbe huu, mpeleke mtoto hospitalini ili aweze kupata utaratibu kutoka kwa wataalamu wa afya.
3. Macho ya mtoto kuwa mekundu kuvimba, kuongezeka, au upofu kwa ghafla.
Kwa kawaida kwa upande wa macho ya mtoto yanaanza kidogo kidogo kuwa mekundu na siku kwa siku wekundu unazidi na hatimaye mtoto anashindwa kuona linaweza kuanza jicho moja na baadae likaingia la pili au yote mawili yanaweza kupata shida kwa wakati mmoja na kama mtoto hajapata huduma mapema upofu unaweza kutokea kwa mtoto .
4. Pia kwa wakati mwingine damu utoka puani na kwenye fizi.
Na pia hizi ni mojawapo ya Dalili za saratani kwa watoto wadogo kwa sababu damu zikianza kutoka puani uanza kidogo kidogo na uongezeka zaidi pale kama kuna joto la kwenye mazingira likiwa juu na pia mtoto damu uanza kupungua siku kwa siku na hata damu ikiongezwa inapungua na kwa upande wa fizi ikitokea mtoto kama amefikia wakati wa kupiga maswaki akipiga damu utoka kwa wangi kwenye fizi. Kwa hiyo walezi na wazazi wanapaswa kufika kwa wataalamu wa afya ili kupata matibabu zaidi.
5. Mtoto kukonda na kupungua uzito bila sababu.
Kwa wakati mwingine mtoto anaanza kukonda na kupungua uzito bila sababu na huku anakuwa anacheza kawaida ila anakonda na uzito unapungua kwa hiyo Mama anapaswa kumpeleka mtoto huyo kwa wataalamu wa afya ili kuweza kujua tatizo ni nini kwa mtoto, na kwa wakati huu hata mtoto akipewa lishe ya aina yoyote anaongezeka kidogo na baadae hali inakuwa kama kawaida yaani kukonds na kupungua uzito.
6. Maumivu ya kichwa kwa mda mrefu na kutapika.
Kwa kawaida kwa watoto wale ambao wanaweza kuongea anaweza kukwambia jinsi anavyojisikia mara nyingi utasikia analalamika kuhusu kichwa kwa wale ambao hawajui kuongea atakuwa analia mara kwa mara , na pia kwa upande wa kutapika mtoto anaweza kutapika kwa mda mrefu hata kama hajala lolote anatapika tu na pia kwa wakati mwingine matapishi huwa mengi kuliko chakula ambacho anakula hali ambayo uwatia wasiwasi pia wazazi wengine wanaweza kuwa na imani potovu kuhusu hilo.
7. Mtoto anaweza kudhoofika na kuacha kucheza pamoja na watoto wengine.
Kwa upande mwingine mtoto anakosa raha anaanza kudhoofika na anashindwa kucheza na wengine kwa wakati mwingine Mama au walezi wanaweza kuchukulia kubwa ni sehemu ya maisha kubwa mtoto huwa hachezi kumbe kuna tatizo ndani yake kwa hiyo uchunguzi kwa mtoto ni lazima ili kuweza kuona kuna tatizo gani, kwa hiyo wazazi au walezi wanapaswa kuwa pamoja na watoto ili kuangalia mabadiliko katika makuzi yao.
8. Kwa wakati mwingine mtoto akipata ajali kidogo anatokea na damu nyingi ukilinganisha na kidonda chake kwa hiyo unakuta damu inapungua mwilini na kwa mara nyingine Dalili za wazi ujitokeza ambapo mtoto akipata ka jeraha na damu zikitoka anabadilika rangi na kuwa na rangi nyeupe fulani hivi kwenye mwili.
9.Kwa hiyo kitu ambacho tunapaswa kuelewa kubwa saratani kwa watoto pengine uonyesha dalili mbalimbali ambazo zinaweza pengine kuleta mashaka kwa wazazi kwa hiyo basi wazazi na walezi wanapaswa kuwa makini ili kuepukana na Imani za kishirikina na kuweza kujua wazi kuwa ni magonjwa ambayo yako kwenye jamii mbalimbali.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi sababu za kupasuka kwa mfuko wa uzazi hasa mama anapokalibia kujifungua.
Soma Zaidi...Kupata Ukimwi ama HIV hufungamana na mambo mengi. Si kila anayefanya ngono zembe nabmuathiria naye lazima aathirike. Hiivsibkweli, ila tangu kuwa hali hii ni hatari kwani kupata maambukizi ni rahisi sana.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi viti vilivyopo kwenye maji ya Amniotic fluid, ni jumla ya vitu vyote vilivyopo kwenye maji ya Amniotic fluid.
Soma Zaidi...Tezi dume hii ni tezi inayopatikana katika katika mfumo wa uzazi wa mwanaume Ila hujulikana kama PROSTATE GLAND. pia hukua karibu na kibofu Cha mkojo na mirija ya mkojo hutumika kuzalisha majimaji (simen) yanayobeba mbegu hivyo bas mk
Soma Zaidi...Majimaji yanayitoka kwenye uke yanafungamana na taarifa nyingi kuhusu afya vya mwanamke. Ujauzito, maradhi, mabadiliko ya homoni na zaidi.
Soma Zaidi...Ni kweli kuwa kutema mate mara kwa mara inaweza kuwa ni dlili za ujauzito. Lakini itambulije kuwa pekee sio kithibitishi cha ujauzito.
Soma Zaidi...Jifunze sababu kuu zinazosababisha kuhisi maumivu makali ya tumbo wakati wa kushiriki tendo la ndoa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dalili za uvimbe kwenye kizazi,hizi ni Dalili ambazo ujitokeza kwa akina mama ambao wana uvimbe kwenye kizazi kwa hiyo endapo mama ameona Dalili kama hizi anapaswa kuwahi hospitali mara moja kwa uangalizi zaidi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mabadiliko ya mzunguko wa damu kwa wajawazito, tunajua wazi kuwa wajawazito pindi ujauzito ukiingia tu, kila kitu kwenye mwili ubadilika vile vile na mzunguko wa damu ubadilika.
Soma Zaidi...