Postii inafundisha maandalizi ya mama kwa ajili ya kujifungulia hii Ni muhimu Sana kwa wale ambao hawajawahi kujingua Ni mara yao ya kwanza wanatakiwa kujua na kuelewa vifaa na mahitaji kujifungulia na kwa wale wanaohudhuria clinic huwa wanafundisha.
Yafuatayo Ni maandalizi ya Mama mjamzito kwa ajili ya kujifungulia;
1.kuwepo na usafiri ; mama anapo hudhurua clinic hufundishwa dalili za Hatari hivyo ujauzito sio kitu Cha kushtukiza hvyo unatakiwa kujipanga ili kutafuta usafiri mapema .
2.mtu atakayebaki nyumba; husaidia kulinda nyumba na familia iliyobaki pia na kuangalia usalama wa hapo nyumbani.
3.mtu wa kumsindikiza; mama anapoenda kujifungua awe na msaidizi kwa ajili ya kuenda kumsaidia na msindikizaji huyu awe anajiweza ili aweze kumsaidia mama pale atakapohitajika msaada wake.
4. Vifaa vya kujifungulia; Kawaida mama akiwa anahudhuria cliniki hupewa mwongozo wa kila kitu hivyo anatakiwa awe na vifaa kwa ajili ya kujifungulia ,na vifaa hivyo Ni Kama vile
1. karatasi aina ya nailoni kwaajili ya kutandikia kitanda anachojifungulia mama ili kuepusha kuchafua mazingira.
2. mipira ya Kuvaa mikononi (gloves) hizi hutumika wahudumu wanapokua wanamuhudumia mama akiwa anajifungua.
3. Kiwembe Cha Upasuaji hutumika kukatia kitovu kilichounganisha Mtoto na kondo la nyuma ili kutenganisha pia kukatia nyuzi wakati mama anaposhonwa Kama akiwa amechanika.
4. kibanio Cha kitovu (clamp) hutumika kubania kitovu kikitenganishwa ili kisitoe Damu.
-5. vitenge au khanga ; ambazo hutumika kumfunikia mtoto,kutandikia kwenye nailoni,mama kujifungua na nguo hizi zisiwe mpya ziwe Ni khanga zilizotumika.
6. malapa ambayo atavaa mam anapotaka kwenda kuoga,kufanya mazoezi maana hawezi kutembea bila kitu mguuni.
7. beseni (dishi) au ndoo ndogo hutumika kuwekea ndoo chafu pia kiafa hiki hutumika mama kunisaidia wakati anakaribia kujifungua maana hauruhusiwi kwenda chooni.
8. sabuni na mafuta ya mama
9. Pamba kubwa na nyuzi za upasuaji
10. pedi kubwa za mama ambapo akijifungua anaweza kuitumia Ila so lazima maana mama anaweza kuitumia khanga.
11. vifaa vya Mtoto Kama vile soksi, bebshoo,pampasi,kofia,mafuta ya Nazi ili vimpatie Mtoto joto pia na leso laini kwaajili ya kumfutia Mtoto.
5.fedha; mama na familia kiujumla wanatakiwa kujipanga kwa matumizi ya hela pale zitakapohitajika wawe nazo.
Mwisho; mama mjamzito anapohudhuria kliniki hupewa mwongozo wote na swala la ujauzito sio la kushtukiza Ni kitu ambacho kipo wazi hivi mama au familia unatakiwa kujipanga na maandalizi.
Mwisho; mama mjamzito anapojigundua tu kuwa ana mimba anatakiwa awahi cliniki kwaajili ya kupewa eleimu juu ya kujikinga,Mambo Hatari kujua na vifaa na Mambo mengine mengi.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Posti hii inahusu zaidi sababu za kuziba kwa mrija wa kizazi ambayo kwa kitaalamu huitwa follapian tube, ni sababu ambazo ufanya mirija ya follapian tube kuziba.
Soma Zaidi...Nitajuwaje kama mjamzito amekaribia kujifunguwa, ni dalili gani anaonyesha, dalili za uchungu wa kujifunguwa
Soma Zaidi...Kupata ujauzito hufungamana na mambo mengi ikiwepo afya vya wawili yaani me na mume na mengineyo. Unaweza kushiriki sikuvhatari na usiupate mimba. Postivhii ibakwendavkukufahamisha undani wa jambo hili.
Soma Zaidi...Nina swali langu:-je maumivu ya nyonga na tumbo la chini ni dalili ya mimba?
Soma Zaidi...Download Kitabu cha elimu ya Ujauzito na malezi ya mimba.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukupa sababu zinazoweza kupelekea uke kuwa mkavu yaani kukosa majimaji wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Posti hii inakwenda kukueleza jinsi ya kuwjuwa kama mtoto ni wa kike ama wa kiume.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi vipimo muhimu kabla ya kubeba mimba,ni vipimo vya moja kwa moja kutoka maabara na vingine sio vya maabara.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za hatari kwa mama mjamzito, kwa sababu kuna baadhi ya Dalili zikitokea kwa mama mjamzito ni vizuri kabisa kuwahi hospitali mara moja.
Soma Zaidi...