Navigation Menu



NGUZO ZA UISLAMU: SWALA NA SHAHADA NA FAIDA ZAKE

NGUZO ZA UISLAMU.

NGUZO ZA UISLAMU: SWALA NA SHAHADA NA FAIDA ZAKE

NGUZO ZA UISLAMU: SWALA NA SHAHADA NA FAIDA ZAKE

NGUZO ZA UISLAMU.
1. Maana ya Shahada.
Shahada mbili ndio nguzo ya kwanza ya Uislamu na ndio kiingilio cha mtu katika Uislamu kwa kuyakinishwa moyoni, kutamkwa kinywani na kuthibitishwa kwa vitendo.
Rejea Qur’an (41:30-31), (2:8) na (33:40).

2. Maana ya Kusimamisha Swala.
Ni kuswali kwa kutekeleza kikamilifu nguzo, sharti zote za swala na kuwa na unyenyekevu (khushui) ndani ya swala.

Nafasi na Umuhimu wa Kusimamisha Swala katika Uislamu.
Swala imesisitizwa na ina umuhimu katika Uislamu kwa sababu zifuatazo;

i.Kusimamisha Swala ni Amri ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Mwenyezi Mungu (s.w) ameamrisha waumini (waislamu) wote wasimamishe swala zote za faradh na sunnah ipasavyo.
Rejea Qur’an (29:45), (4:103) na (14:31).

ii.Kusimamisha swala ni nguzo ya Pili ya Uislamu.
Baada ya shahada mbili, nguzo ya pili na ya msingi mno katika Uislamu ni kusimamisha swala.

iii.Swala humtakasa muislamu na mambo machafu na maovu.
Bila shaka swala ikiswaliwa vilivyo humuepusha mja na mambo machafu na maovu.
Rejea Qur’an (29:45).

iv.Swala ni amali ya mwanzo kabisa kuhesabiwa siku ya Qiyama.
Swala ya muumini ikitengemaa vizuri ndio sababu ya kufaulu kwake Duniani na Akhera pia.
Rejea Qur’an (23:1-2,9), (87:14-15) na (22:34-35).

v.Kutosimamisha swala ni sababu ya mtu kuingizwa motoni.
Hii ni baada ya muislamu Kupuuza swala kwa kutozingatia sharti na nguzo zake kikamilifu na kukosa unyenyekevu (khushui) ndani ya swala.
Rejea Qur’an (74:42-47), (68:42-43) na (107:4-5).

Lengo la Kusimamisha Swala.
Lengo kuu la kusimamisha swala ni kumkinga mja na mambo machafu na maovu kwa kutekeleza kikamilifu sharti, nguzo na sunnah za swala pamoja na kuwa na khushui ndani ya swala kama ifuatavyo;
i.Swala inamtakasa mja kwa kuzingatia na kutekeleza sharti zake zote kikamilifu ambazo ni kuwa twahara, sitara (kujisitiri), kuchunga wakati wa swala na kuelekea Qibla.
ii. Swala inamtakasa mja kwa kutekeleza kikamilifu nguzo na sunnah za swala kama kumsifu na kumtukuza Mwenyezi Mungu (s.w), kusoma Qur’an, kutoa ahadi ya kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (s.w), kuomba dua na kutekeleza vitendo vyote vya swala.

Faida (matunda) ya kusimamisha swala katika jamii.
Swala za faradhi zikisimamishwa vilivyo faida zifuatazo hupatikana katika jamii;

i.Usafi na unadhifu wa mwili.
Kwani muislamu hawezi kuswali mpaka ahakikishe kuwa msafi (twahara) kikamilifu katika nguo na mwili pia na sehemu ya kuswalia.
Rejea Qur’an (7:31).

ii.Utakaso wa Nafsi.
Kwa kutekeleza sharti na nguzo za swala pamoja na mnyenyekevu katika swala, hupelekea mja kuwa mtiifu ipasavyo kwa Mola wake muda wote.

iii.Swala za jamaa huimarisha udugu, umoja na usawa.
Kuswali katika jamaa huleta udugu, umoja na usawa wa kweli na kuepusha mfarakano, chuki na ubaguzi miongoni mwa waislamu.
Rejea Qur’an (49:10,13).

iv.Swala za jamaa huwafunza waislamu uongozi bora.
Swala huongozwa na imamu (kiongozi) wa waumini husika anayetokana na wao kutokana na sifa maalumu za kuwa kiongozi.



Kwa nini Wengi wanaoswali hawafikii Lengo la Swala zao?
Miongoni mwa sababu ya wengi kutofikia malengo ya swala zao ingawa wanaziswali misikitini tena kwa jamaa ni;

1.Hawajui lengo halisi la swala.
Waislamu wengi huswali kwa lengo la kufutiwa madhambi na kupata thawabu na sio kuepukana na machafu na maovu, ambalo ndio lengo kuu la swala. Kupata thawabu na kufutiwa madhambi ni matunda ya swala.
Rejea Qur’an (29:45) na (72:23).

2.Waislamu wengi hawana ujuzi sahihi juu ya swala.
Pamoja na waislamu wengi kutekeleza swala zao kwa jamaa lakini wengi wao hawajui kabisa miiko, sharti na nguzo za swala ila wanafuata mkumbo tu.
Rejea Qur’an (7:205), (7:55) na (4:142).

3.Waislamu wengi hawahifadhi swala zao.
Pamoja na kuswali kwao bado wengi hawazingatii na kutekeleza kikamilifu sharti na nguzo za swala zao inavyotakiwa.
Rejea Qur’an (107:4-5) na (23:1,8).

4.Wengi hawaswali kwa Unyenyekevu swala zao.
Kukosa unyenyekevu (utulivu wa mwili, fikra na uzingativu) hupelekea mwenye kuswali kutofikia lengo na matunda ya swala.
Rejea Qur’an (29:45), (23:1-2) na (23:10-11).

5.Kutosimamisha Swala za jamaa ipasavyo.
Waislamu wengi hawaswali jamaa misikitini au hawazingatia sharti za swala ya jamaa kama kunyoosha safu ipasavyo, kugusanisha mabega, vidole, n.k.
Rejea Qur’an (23:1-2).





                   

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 1029


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Ni ipi hukumu ya muislamu anayekula mwezi wa Ramadhani bila ya sababu ya kisheria
Endapo muislamu hatafunga mwezi wa Ramadhani bila ya ruhusa je atatakiwa afanye nini. Je ataweza kuilipa funga hiyo? Soma Zaidi...

Haki na wajibu wa mtoto kwa wazazi na katika jamii
Soma Zaidi...

Haki za viumbe na mazingira
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Ufumbuzi wa tatizo la riba.
Uislamu ndio dini pekee ambayo inatoa ufumbuzi juu ya suala la riba. Soma Zaidi...

Namna ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa.
Post hii inakwenda kukugundisha jinsi ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa. Soma Zaidi...

Kwa nini waislamu wanaoa mke zaidi ya mmoja
Post hiibitakugundisha hekima ya kuruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja katika sheria za kiislamu. Soma Zaidi...

Ni zipi siku ambazo ni haramu kufunga? na ni kwa nini hairuhusiwi kufunga katika siku hizo
Soma Zaidi...

Kumkafini (kumvisha sanda maiti)
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Lengo la kusimamisha swala
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Yaliyo haramu kwa mwenye hadathi kubwa.
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ya haramu kwa mwenye hadathi kubwa Soma Zaidi...