picha

DUA WAKATI WA KURUKUU,KUITIDALI, KUSUJUDI NA NAMNA YA KUSOMA TAHIYATU

6.

DUA WAKATI WA KURUKUU,KUITIDALI, KUSUJUDI NA NAMNA YA KUSOMA TAHIYATU

6. Kurukuu
Baada ya kusoma Suratul-Fatiha na Surah nyingine, au baadhi ya aya katika sura nyingine unasema Allahu-akbar kisha unarukuu (kuinama). Rukuu ni nguzo ya swala pamoja na kujituliza humo. Katika rukuu ni sunnah kumsabihi Allah (s.w) kwa kusema kimya kimya mara tatu au zaidi “Subhana Rabbiyal’Adhiim” “Utukufu ni wako Ee Bwana (Mlezi) wangu Uliye mkuu”

7.Kuitidal
Kuitidali ni kusimama wima kutoka kwenye rukuu, ni sunnah kusema wakati wa kunyanyuka maneno haya:“sami’a llahu liman hamidahu” Mwenyezi Mungu anamsikia kila mwenye kumhimidi. Na baada ya kusimama sawa ni sunnah kusema “rabbanaa walakal-hamdu”ewe mola wetu sifa zote za ukamilifu ni zako. Pia ni sunnah kusema maneno haya “rabbanaa walakal-hamdu mil-as-samaawati wamil-al-ardhi wamil-amashi-ita minshai-in ba’adah” Ewe Mola wetu sifa zote za ukamilifu ni za kwako, kutoka mbinguni, kutoka ardhini na katika vitu vyote vilivyo baina yao (mbingu na ardhi) na kutoka katika vinginevyo unavyo viridhia

8.Kusujudi
Ni nguzo pamoja na kujituliza katika sujudi. Mkusujudi ni kuvituliza chini viungo saba kwa utaratibu wa swala. Vingo hivyo ni , paji a uso, viganya viwili vya mikono, magoti mawili na matumbo ya nyayo za vidole vya miguuni.viungo vyote hivi vinatakiwa vielekee kibla. Paji la uso ni pamoja na pua iguse chini.utasema kwenye sijda “subhaana rabbiyal-a’alaa” utukufu ni wa kwako Mola uliye tukuka.

9.kukaa baina ya sijda mbili
Hiki ni kitako kinachopatikana baada ya kutoka kusujudi. Sifa ya kikao hiki ni kukalia unyayo wa mguu wa kushoto na kuweka mikono miwili juu ya mapaja. Ni sunnah kusema maneno haya: “rabbigh-firliy warhamnii wa’afinii warzuqniy”Ewe Mola wangu nisamehe, na unirehemu, na unipe afya na uniruzuku

10.kikaa tahiyyatu
Katika kukaa Thiyyatu mtume alikuwa akikalia futi la mguu wa kushoto na kusimamisha futi la mguu wa kulia na katika tahiyyatu ya mwisho alikaa chini na kuulaza mguu wa kushoto katika uvungu wa mguu wa kulia na alisimamisha futi la mguu wa kulia, katika vikao vyote hivyo viwili,

Mtume (s.a.w) alivilaza viganja vyake juu ya mapaja karibu na magoti kama tunavyoelezwa katika hadith ifuatayo: Abdullah bin Jubair(r.a) ameeleza kuwa wakati Mtume (s.a.w) alipokaa tahiyyatu, alikuwa akiweka kiganja chake cha mkono wa kulia juu ya paja lake la kulia na kiganja cha mkono wa kushoto juu ya paja la mguu wa kushoto na alikuwa akinyoosha kidole chake cha shahada (wakati wa k u s e m a , “ A s h - h a d u anllaaillaha illallah) na kukiegemeza juu ya kidole gumba na alikuwa akiweka kiganja chake cha mkono wa kushoto juu ya goti lake (la mguu wa kushoto). (Muslim).


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Views 7642

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Bongolite - Game zone - Play free game     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

Njia ambazo Allah hufundisha wanadamu elimu mbalimbali

Ni kipi chanzo cha Elimu, na ni kwa namna gani Allah hufundisha Elimu kwa wanadamu?

Soma Zaidi...
Ni nini maana ya Ilhamu katika uislamu?

Ilhamu ni moja katika njia ambazo Allah huwasiliana na wanadamu na kuwafundisha mambo mablimbali.

Soma Zaidi...
Shirk na aina zake

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Nguzo za Imani kwa mujibu wa mafunzo ya kiislami.

Makala hii inakwenda kukufundisha kuhusu nguzo sita za imani katika Uislamu.

Soma Zaidi...
Kwa namna gani nabii Musa na Bi Mariam waliweza kuzungumza na Allah nyuma ya pazia

Nabii Musa na Mama yake nabii Isa bi Mariam waliweza kuwasiliana na Allah nyuma ya pazia.

Soma Zaidi...