image

Jifunze ni kwa namna gani Malaika waliweza kuwasiliana ana manabii Malimbali

Wakatibmeingibe Allah anapotaka kuwasiliana na wanadamu hutuma Malaika wake.

(c)Kuletewa Ujumbe na Malaika kutoka kwa Allah (s.w)

 

Kutuma ujumbe wa Malaika ni njia nyingine anayoitumia Allah (s.w) katika kuwaelimisha wanaadamu hasa katika mambo ya msingi ya maisha ya mwanaadamu hapa ulimwenguni. Hii ni njia maalum aliyoitumia Allah katika kuwasiliana na Mitume na miongoni mwa watu wengine wema. Kuhusu jinsi Mtume (s.a.w) aliyofundishwa na Allah (s.w) tunafahamishwa katika aya zifu atazo:

 

Naapa kwa nyota zinapoanguka. (Zinapokuchwa). Kwamba mtu wenu (huyu Muhammad) hakup otea kwa ujinga wala hakukosa. (na hali ya kuwa anajua); wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake). (53:1-3)

 

Hayakuwa haya (anayosema) ila ni wahyi (ufunuo). Uliofunuliwa (kwake).Amemfundisha (malaika) mwenye nguvu sana mwenye uweza. Na yeye yu katika upeo wa kuona (Horizon) katika mbingu kwa juu kabisa.(53:4-6)

 

Kisha (ukaribu wao) ni kama baina ya upinde na upinde au karibu zaidi. Na akamfunulia huyo Mtumwa wake (Mwenyezi Mungu) aliyoyafunua. Moyo haukusema uwongo uliyoyaona.(Moyo wake ulisadikisha haya yaliyotokea). Je! Mnabishana naye juu ya yale anayoyaona (daima)? (53:7-12).

 

Katika mafunzo ya Qur-an na Hadithi tunafahamishwa kuwa malaika Jibril ndiye malaika mkuu aliyehusika na kupeleka ujumbe kwa Mitume wa Allah (s.w). Lakini pia kutokana na aya za Qur-an sio yeye pekee aliyehusika tu na kupeleka ujumbe wa Allah kwa Mitume bali wajumbe wengine pia walihusika. Katika aya zifuatazo tunafahamishwa juu ya wageni (wajumbe) wa Nabii Ibrahim (a.s): waliomletea habari njema ya kumpata mtoto Is-haqa na habari ya kuhuzunisha ya kuangamizwa kwa watu waovu wa Kaumu ya Lut (a.s) aliyekuwa mpwawe:

 

Na uwaambie khabari za wageni wa (Nabii) Ibrahim. Walipoingia kwake na wakasema:“Salaam” (Salaamun Alaykum, akawajibu; kisha) akasema (alipoona wamekataa kula chakula alichowawekea). “Kwa hakika sisi tunakuogopeni”.Wakasema: “Usituogope, Sisi tunakupa khabari njema ya (kuwa utazaa) mtoto mwenye ilimu kubwa ”. (15:51-53)

 

Akasema: “Oh! Mnanipa khabari hii, na hali ya kuwa uzee umenishika! Basi kwa njia gani mnanipa khabari njema hiyo?” Wakasema: “Tumekupa khabari njema iliyo haki: basi usiwe miongoni mwa wanaokata tamaa”. Akasema: “Na nani anayekata tamaa ya rehema ya Mola isipokuwa wale waliopotea?”
(15:54-5 6)

 


Akasema: (Tena) kusudi lenu (jingine) ni nini enyi mliotumwa?” Wakasema: “Hakika sisi tumetumw a kwa wale watu wakosaji (tukawaangamize).(51:57-58)

 

(Wa tu w a Na bii Lut.) “Isipokuw a w a liomfu a ta Lu t. Bila shaka sisi tutawaokoa wote hao (waliomfuata Lut)” Isipokuwa mkewe. Tunapimia ya kuwa atakuwa miongoni mwa watakaokaa nyuma (waangamizwe)”.

 

Basi wajumbe walipofika kwa watu wa Lut (kwa sura za kibinaadamu). (Lut) alisema:“Hakika nyinyi ni watu msiojulikana (na mimi; sikujueni)”.(15:61-62).

 

Wakasema:“Basi sisi tumekuletea yale ambayo walikuwa wanayafanyia shaka, (nayo ni maangamizo yao)”.“Na tumefika kwako kwa (hilo jambo la) haki (la kuangamizwa) na hakika sisi ni wenye kusema kweli.

 


“Basi ondoka na watu wako katika kipande cha usiku (pingapinga la usiku), na wewe ufuate nyuma yao; wala yeyote katika nyinyi asigeuke nyuma (na mwende upesi upesi) mnakoamrishwa ”.

 

Na tukamkatia (Nabii Luti) jambo hili; la kwamba mizizi yao itakatwa asubuhi (yaani wataangamiziliwa mbali as u b uh i)” (15:66)
Zakaria (a.s) mlezi wa Maryamu mama wa Nabii Issa (a.s) aliletewa habari na malaika ya kumzaa Yahya (a.s) kama tunavyofahamishwa katika aya zifuatazo:

 

Pale pale Zakaria akamwomba Mola wake, akasema: “Mola wangu! Nipe kutoka kwako mtoto mwema. Wewe ndiye usikiaye maom bi (ya wanaokuomba)”.

 

Mara Malaika wakamlingania hali amesimama akiswali chumbani, kwamba Mwenyezi Mungu anakupa khabari njema za (kuwa utazaa mtoto; umw ite) Yahya, atakayekuw a mw enye kumsadikisha (Mtume atakayezaliwa) kwa neno litokalo kwa Mw enyezi Mungu (Naye ni Nabii Issa) na atakayekuw a bwana kabisa na mtawa na Nabii anayetokana na watu wema (Nao ni nyinyi).
14

 


“Akasema (Zakaria): “Mola wangu! Nitapataje mtoto, na hali uzee umenifikia, na mke wangu ni tasa?” Akasema (Mwenyezi Mungu), “Ndiyo vivyo hivyo; Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo)”.

 

Akasema: “Mola wangu! Niwekee alama (ya kunitambulisha kuwa mke wangu kishashika mimba nipate kufurahi upesi)”. Akasema: “Alama yako ni kuwa hutaweza kusema na watu kwa siku tatu isipokuwa kwa ishara tu. Na mtaje Mola wako kwa wingi na umtukuze (kwa kuswali) wakati wa jioni na asubuhi”. (3:41)
Pia Bibi Maryamu aliletewa ujumbe na malaika kutoka kwa Allah kama inavyodhihirika katika aya zifuatazo:

 


Na mtaje Maryamu Kitabuni (humu). Alipojitenga na jamaa zake, (akaenda) mahali upande wa mashariki (wa msikiti). Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Muhuisha Sharia yetu (Jibrili) - akajimithilisha kwake (kwa sura ya) binaadamu aliye ka mili.

 

(Maryamu) akasema: “Hakika mimi najikinga kwa (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa rehema (Aniepushe) nawe. Ikiwa unamuogopa Mungu (basi ondoka nenda zako).”

 

(Malaika) akasema: “Hakika mimi ni Mjumbe wa Mola wako: ili nikupe mwana mtakatifu ” (19:16-19)
Pamoja na Malaika kuleta ujumbe kwa Mitume na miongoni mwa watu wema, pia kuna Malaika waliokuja kufundisha elimu ya uchawi kama sehemu ya mtihani kwa wanaadamu. Malaika waliotumwa na Allah kufundisha uchawi kama mtihani kwetu ni Haruta na Maruta kama inavyobainishwa katika Qur-an:

 

 

 

Wakafuata yale waliyoyafuata mashetani, (wakadai kuwa yalikuwa) katika ufalme wa (Nabii) Suleiman, na Suleiman hakukufuru, bali mashetani ndio waliokufuru,wakiwafundisha watu uchawi na (uchawi) ulioteremshwa kwa Malaika wawili, Haruta na Maruta, katika (mji wa) Babil. Wala (Malaika hao) hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: “Hakika sisi ni mtihani (wa kutazamwa kutii kwenu); basi usikufuru”. Wakajifunza kwao ambayo kwa mambo hayo waliweza kumfarikisha mtu na mkewe (na mengineyo). Wala hawakuwa wenye kumdhuru yoyote kwa hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza ambayo yatawadhuru wala hayatawafaa. Na kwa yakini wanajua kwamba aliyekhiari haya hatakuwa na sehemu yoyote katika akhera. Na bila shaka ni kibaya kabisa walichouzia (starehe za) nafsi zao (za akhera). Laiti wangalijua, (hakika wasingefanya hivi)”. (2:102).
Aya hii inazidi kututhibitishia kuwa hapana chochote ambacho anakijua mwanaadamu ila itakuwa amefundishwa na Allah (s.w)           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/01/Thursday - 09:14:22 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 535


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Upeo wa Elimu waliyokuwa nayo Mitume
Soma Zaidi...

Taqwa (Hofu ya kumuogopa Allah) ni popote ulipo
عَنْ أَبِي ذَرٍّ جُنْدَبِ بْنِ جُنَادَةَ، وَأَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، عَنْ رَسُولِ اللَ... Soma Zaidi...

Tawhiid
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

(b)Umbile la Mwanaadamu ni la kidini
Ukizingatia maana halisi ya dini, kuwa dini ni utaratibu wa maisha, utadhihirikiwa kuwa umbile la mwanaadamu ni la kidini. Soma Zaidi...

Maana ya uislamu.
Kwenye kipengele hichi titajifunza maana ya uislamu,na maana nyingine tofauti. Soma Zaidi...

KUAMINI MALAIKA WA ALLAH (S.W.)
Soma Zaidi...

Mtazamo wa uislamu juu ya dini
Kwenye kipengele hichi tutajifunza mitazamo ya kikafiri juu ya dini. Soma Zaidi...

Shirk na aina zake
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

KAZI ZA MALAIKA
Malaika wamepewa kazi ya kumtumikia Allah(SW) kwa kumtukuza na kumtakasa, kama wanavyosema wenyewe:Hakuna yoyote miongoni mwetu ila anapo mahali pake mahususi. Soma Zaidi...

Sifa za Allah Mwenyezi Mungu
Soma Zaidi...

Nini chanzo cha elimu zote na ujuzi wote
Ninichanzo cha Elimu? (EDK form 1 Dhanaya Elimu) Soma Zaidi...

Madai ya Makafiri dhidi ya kuwepo kwa Allah (s.w) na Udhaifu wa Madai hayo.
2. Soma Zaidi...