Navigation Menu



Ni yupi mtume wa mwisho? na je ni kwa nini Muhammad ndiye mtume wa mwisho?

Ni yupi mtume wa mwisho? na je ni kwa nini Muhammad ndiye mtume wa mwisho?

Mwisho wa Utume



Maswali ambayo huweza kuulizwa ni: Kwa nini wahyi ukatike? Kwa nini Mitume wasiendelee kuletwa hadi kiyama? Kwa nini Muhammad (s.a.w) afunge mlango wa Utume?
Ili kulielewa vizuri suala hili la mwisho wa Utume yafaa kwanza tuzingatie kuwa kilicho muhimu na cha msingi kabisa kwa Mtume yeyote si kule kuwepo kimwili bali ni kule kuufikisha kwake ujumbe aliopewa na Mwenyezi Mungu (s.w) ili watu wake wasiwe na hoja tena iwapo watachagua kupotea.


Na lau ingekuwa lililo muhimu kwa Mtume ni kule kuwapo kimwili basi Mwenyezi Mungu angelimpeleka Mtume mara tu baada ya kufariki Mtumealiyetangulia. Kilicho cha msingi ni mafundisho aliyokuja nayo. Maadamu ujumbe aliouleta uko hai basi Mtume huyo yu hai. Hivyo kifo halisi cha Mtume ni kule kupotea kwa mafundisho aliyoyaleta. Mitume wote waliomtangulia Muhammad (s.a.w) mafundisho yao yalipotea, kwani yalichanganyika na hekaya mbali mbali. Katika vitabu vilivyoitangulia Qur-an, kwa mfano Taurat, Injil, na Zaburi hakuna hata kimoja ambacho kipo katika hali ya usahihi wake wa asili. Hata wafuasi wa vitabu hivyo wanakiri kuwa nakala walizonazo leo si zile walizopewa Mitume. Si hivyo tu bali hata historia za maisha ya Mitume waliomtangulia Muhammad (s.a.w) zimechanganywa na ngano za kushtusha kabisa, hata inakuwa vigumu kupambanua haki na batili.


Kinyume chake mafundisho aliyokuja nayo Muhammad (s.a.w) yako hai kabisa na hayajaharibiwa na katu hayawezi kuharibiwa. Qur-an, kitabu alichoteremshiwa kipo tena katika lugha ile ile ya asili bila ya kupunguza wala kuzidisha japo nukta moja. Historia kamili ya maisha yake, maneno yake, maagizo yake, vitendo vyake, vyote vimehifadhiwa kwa usahihi kabisa kiasi ambacho karne 14 zimepita lakini bado historia yake ni ya wazi na kamili kama kwamba tunamuona kwa macho yetu. Katika kila kipengele cha maisha yetu tunaweza kupata muongozo na mafundisho kutoka kwa Muhammad (s.a.w). hii ndio sababu hakuna haja ya kuletwa Mtume mwingine baada yake.
Zaidi ya hayo yapo mambo matatu ambayo husababisha kuhitajika kuja kwa Mtume mwengine baada ya yule aliyetangulia:



(1)Iwapo mafundisho ya Mtume aliyetangulia yamechanganywa na hekaya za nzushi, kuharibiwa na kupotea. Katika hali kama hiyo Mtume anahitajika ili aje aifundishe dini katika usahihi wake wa awali.



(2)Iwapo mafundisho ya Mtume aliyeondoka hayakukamilika na hivyo kukawa na haja ya kuyakamilisha, kuyarekebisha, au kuongeza jambo fulani.



(3)Iwapo Mtume aliyetangulia alipelekwa kwa watu wa taifa fulani maalum au nchi fulani maalum na hivyo kuwepo haja ya kuletwa Mtume kwa watu wa taifa au nchi nyingine. Au pengine Mtume anaweza kuletwa ili amsaidie Mtume mwingine, lakini kwa kuwa hii si kanuni ya kawaida, hatujaita kama sharti la nne. Katika Qur-an ipo mifano miwili ya hali kama hiyo. Nabii Haruni (a.s) alikuwa msaidizi wa Nabii Musa (a.s). Nabii Lut (a.s) Ismail (a.s) na Is-haq (a.s) walikuwa wasaidizi wa Nabii Ibrahim (a.s).
Haya matatu ndiyo masharti makuu ya kimsingi yanayohitajika ili aletwe Mtume mwingine. Kati ya hayo hakuna hata sharti moja lililopo leo. Kwanza mafundisho ya Mtume wa mwisho, Muhammad (s.a.w) yako hai, yamehifadhiwa na yatadumu hadi siku ya Kiyama. Mwongozo aliouleta kwa walimwengu wote ni sahihi na kamili na umehifadhiwa katika Qur-an humo kuna ahadi ya ulinzi wa Allah (s.w) kama tunavyofahamishwa:


“Hakika sisi ndio tulioteremsha mawaidha (haya hii Qur-an); na Hakika sisi ndio tutakaoyalinda.” (15:9).
Pia sunnah zake zimehifadhiwa kikamilifu kiasi ambacho mtu anaweza kujua pasi na shaka yoyote nini mafundisho ya Mtume juu ya jambo fulani. Hivyo sharti la kwanza linaondoka.
Pili, Mwenyezi Mungu amekamilisha mwongozo wake kwa Nabii Muhammad (s.a.w) na hivyo Uislamu ni dini kamilifu kwa ulimwengu wote. Allah (s.w) anasema katika Qur-an:


“… Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kukutimizieni neema yangu juu yangu na nim ekupendeleeni Uis lam u uw e dini yenu … (5:3)




                   


           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 1500


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

mitume
Labda itaulizwa: Kwanini Mtume Muhammad (s. Soma Zaidi...

(b)Umbile la Mwanaadamu ni la kidini
Ukizingatia maana halisi ya dini, kuwa dini ni utaratibu wa maisha, utadhihirikiwa kuwa umbile la mwanaadamu ni la kidini. Soma Zaidi...

Taathira ya Imani ya Malaika katika maisha ya kila siku
Kuamini Malaika ni imani ambayo pindi ikithibiti vema moyoni, huleta taathira kubwa sana katika maisha ya kila siku na hivyo kubadili kabisa tabia na mwenendo wa Muumini. Soma Zaidi...

Maana ya uislamu.
Kwenye kipengele hichi titajifunza maana ya uislamu,na maana nyingine tofauti. Soma Zaidi...

ENYI WAJA WANGU NIMEIKATAZA NAFSI YANGU DHULMA
Soma Zaidi...

Taqwa (Hofu ya kumuogopa Allah) ni popote ulipo
عَنْ أَبِي ذَرٍّ جُنْدَبِ بْنِ جُنَادَةَ، وَأَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، عَنْ رَسُولِ اللَ... Soma Zaidi...

(c)Vipawa vya Mwanaadamu
Vipawa vya mwanaadamu ni sababu nyingine inayomfanya mwanaadamu asiweze kuishi bila ya kufuata dini moja au nyingine. Soma Zaidi...

Dalili na ishara za jeraha kwenye ngozi
Posti hii inaonyesha dalili,sababu na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa aliyepata jeraha kwenye ngozi kwa kuingiliwa na kitu Kama mwiba,Pini,sindano n.k Soma Zaidi...

Kwa nini Uislamu ndio dini pekee inayostahiki kufuatwa
Kwa nini uislamu ndio dini pekee ya haki ambayo watu wanatakiwa waifuate. Soma Zaidi...

Haki za kielimu za mwanamke katika uislamu
Haki ya ElimuKatika Uislamu kujielimisha ni faradhi inayowahusu Waislamu wote, wanaume na wanawake: "Soma kwa jina ? Soma Zaidi...