Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Furqaan (25:64-76)

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Furqaan (25:64-76)

4.Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Furqaan (25:64-76)



Katika Suratul-Furqaan sifa za Waumini zinabainishwa tena kama ifuatavyo:


"Na waja wa Rahmaan; Ni wale wanaokwenda ulimwenguni kwa unyenyekevu; na wajinga wakisema nao (maneno mabaya) huwajibu (maneno ya) salama. (25:63)


Na wale wanaopitisha baadhi ya saa za usiku kwa ajili ya Mola wao kwa kusujudu na kusimama. na wale wanaosema:


"Mola wetu! Tuondolee adhabu ya Jahannam, bila shaka adhabu yake ni yenye kuendelea. (25:64-65)


Hakika hiyo (Jahannamu) ni kituo kibaya na mahali (pabaya kabisa) pa kukaa". Na wale ambao wanapotumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanaokuwa katikati baina ya hayo. (25:66-6 7)


Na wale wasiomuomba Mungu mwingine pamoja na Allah, wala hawaiui nafsi aliyoiharamisha Allah ila kwa haki, wala hawazini; na atakayefanya hayo atapata madhara (papa hapa ulimwenguni). (25:68).


Na atazidishiwa adhabu siku ya Kiyama na atakaa humo kwa kufedheheka milele. (25:69)


Ila yule atakayetubia na kuamini na kufanya vitendo vizuri, basi hao ndio Mwenyezi Mungu atawabadilishia maovu yao kuwa mema; na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu. (25:70)


Na aliyetubia na kufanya wema, basi kwa hakika yeye anatubu kweli kweli kwa Mwenyezi Mungu. (25:71)



Na wale ambao hawashuhudii shahada za uwongo, na wanapopita penye upuuzi, hupita kwa hishima (yao). (25:72)


Na wale ambao wanapokumbushwa aya za Mola wao hawaziangukii kwa uziwi na upofu. (25:73).


Na wale wanaosema: "Mola wetu! Tupe katika wake zetu na watoto wetu yaburudishayo macho (yetu) (nyoyo zetu), na Utujaalie kuwa waongozi kwa wamchao (Mungu). (25:74)


Hao ndio watakaolipwa ghorofa (za Peponi) kwa kuwa walisubiri, na watakuta humo hishima na amani. (25:75)


Wakae humo milele; kituo kizuri na mahali pazuri (kabisa pa kukaa). (25:76)



Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa sifa za Waumini ambao hapa wameitwa "Waja wa Rahman" ni pamoja na:
(i)Kuishi na watu kwa Wema
Waumini wa kweli huishi na watu kwa wema kwa kuwathamini na kuwaheshimu; kujizuia na kuwafanyia watu kibri, kujizuia na kujikweza na kujitukuza mbele ya wengine, kujizuia na kuwadhalilisha watu na kuwavunjia heshima. Kutembea katika ardhi kwa unyenyekevu ni pamoja na kuchungua barabara mipaka ya Allah(s.w) na mtume wake(s.a.w)


(ii)Huepukana ugomvi na Mabishano
Waumini wa kweli huepuka kabisa tabia ya ugomvi na mabishano. Waumini hufahamu fika kuwa kwenye ugomvi na mabishano shetani huwepo na huchochea faraka baina ya ndugu. Namna ya kuepukana na wagomvi kwa salama inaelekezwa katika Qur-an (41:36)



(iii)Hudumu katika Kuswali Tahajjud
Kuamka usiku na kuswali swala ya "Tahajjud" (kisimamo cha usiku - Qiyamullayl) kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah (s.w) na Rehema zake. Swala hii huswaliwa usiku wa manane hususan katika theluthi ya mwisho ya usiku inayokaribiana na Al-fajiri. Swala hii ni lazima kwa kila Muislamu mwenye azima ya kuulingania Uislamu na kuusimamisha katika jamii. Ukirejea Historia ya kushuka Qur-an, amri ya kwanza aliyopewa Mtume (s.a.w) kwa niaba ya umma wake ni Kusoma kwa ajili ya Allah (s.w) - Qur-an (96:1-5); amri ya pili ikiwa swala ya Tahajjud (Qur-an 73:1-5) ili iwe maandalizi ya kukabili shughuli nzito ya kuhuisha na kusimamisha Uislamu katika jamii. Msisitizo wa Qiyamullayl tunaupata vizuri katika aya ifuatayo:


"Je, afanyaye ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama na kuogopa akhera na kutarajia rehema ya Mola wake (ni sawa na asiyefanya hivyo)? Sema: "Je wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?" Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu." (39:9)



(iv)Huogopa adhabu ya Allah (s.w)
Waumini wa kweli huogopa adhabu ya Allah (s.w) aliyowaandalia watu waovu huko akhera kwa kujitahidi kutenda mema na kujiepusha na maovu na kila mara kuomba:


"Nawale wanaosema:Mola wetu! Tuondolee adhabu ya Jahannam, bila shaka adhabu yake ni yenye kuendelea. Hakika hiyo (Jahannamu) ni kituo kibaya na mahali (pabaya kabisa) pa kukaa." (25:65-66)



(v)Hutumia Neema kwa Insafu
Waumini wa kweli hutumia neema walizopewa na Allah (s.w) kwa insafu. Hawafanyi ubadhirifu au israfu wa neema kama vile kutumia vibaya mali, wakati, vipaji na ujuzi. Waumini daima huzigatia kuwa Allah (s.w) hawapendi waja wanaofuja neema walizotunukiwa na Allah (s.w). Wasiotumia neema kwa insafu, ni wafuasi wa shetani.


"Na wape jamaa wa karibu haki zao, na mayatima (vile vile) na masikini, wala usifanye ubadhirifu." (1 7:26)


Hakika wafanyao ubadhirifu ni marafiki wa shetani, na shetani ni mwenye kumkufuru Mola wake. (17:27)



(vi)Hawamshirikishi Allah (s.w)
Waumini wa kweli hawamshirikishi Allah (s.w). Hujiepusha na aina zote za shirk. Shirk katika dhati, shirk katika sifa, shirk katika hukumu na shirk katika mamlaka ya Allah (s.w). Kufanya shirk ni dhambi kubwa ya daraja la kwanza. Qur-an inaonya na kutahadharisha kuwa:



Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi (dhambi ya) kushirikishwa na kitu na husamehe yasiyokuwa haya kwa amtakaye. Na anayemshirikisha Allah bila shaka amebuni dhambi kubwa. (4:48). Pia rejea Qur-an (4:116) na (39:65)



(vii)Hulinda na kutetea haki ya Uhai wa Nafsi
Waumini wa kweli hulinda na kutetea haki ya uhai wa kila nafsi yenye haki ya kuishi. Hivyo, hujitahidi kujiepusha na ushiriki wa kusababisha au kufanya mauwaji ya nafsi ambayo kwa mujibu wa mwongozo wa Allah (s.w) hustahiki kuishi. Ulinzi wa utetezi huu wa haki ya uhai wa nafsi unatokana na mwongozo wa Allah katika Qur-an kuwa:


Mwenye kuiuwa nafsi pasina nafsi hiyo iliyouliwa kuuwa au kufanya fisadi katika ardhi, itakuwa kana kwamba ameuwa watu wote. Na atakayelinda nafsi hiyo, atakuwa kana kwamba amelinda uhai wa watu wote. (5:32)



(viii)Hawafanyi Uzinzi
Waumini wa kweli hawaikaribii zinaa wala kufanya uzinifu. Na zaidi hawashawishi wala kushiriki kwa namna yoyote ile katika mambo yanayosababisha zinaa kufanyika.


"Wala usikaribie zinaa. Hakika hiyo ni uchafu (mkubwa) na ni njia mbaya (kabisa)." (17:32)



(ix)Husema Kweli daima
Waumini wa kweli husema kweli daima. Hawatowi ushahidi wa uongo au kutetea batili. Wanapowajibika kutoa ushahidi juu ya jambo, husema ukweli hata kama ni dhidi ya nafsi zao wenyewe au watu wao wa karibu. (Rejea Qur-an 4:135, 5:8)



(x)Hawavutiwi na mambo ya Kipuuzi
Waumini wa kweli ni wale ambao hawavutiwi na mambo ya kipuuzi ambayo wafuasi wa Ibilisi huyatumia katika kuwavutia watu kwa lengo la kuwapumbaza na kuwateka akili zao. Muumini huwa hana muda wa kupoteza au fursa ya kuikabidhi akili yake kwa twaghuti aichezee. Hivyo, kwenye mambo ya kipuuzi waumini hupita haraka kwa heshima zao, na ikibidi kuweka jambo m-badala lenye maana na manufaa kwa jamii.



(xi)Humwitikia Allah (s.w) anapowaita
Waumini wa kweli humwitikia Allah (s.w) anapowaita kwa makatazo na maamrisho yake katika Qur-an. Hivyo hutii kwa unyenyekevu maagizo ya Allah (s.w) kila wanapokumbushwa kwa kusomewa au Kusoma wenyewe aya za Kitabu cha Allah (s.w) na Allah (s.w) ananadi katika Qur-an kuwa:


Na waja wangu wanapokuuliza kuhusu mimi, basi (waambie) hakika Mimi nipo karibu najibu maombi ya mwombaji pindi anaponiomba. Basi na waniitikie na waniamini Mimi ili wapate kuongoka. (2:186)


(xii)Hujenga Familia za Kiislamu
Waumini hujitahidi kujenga familia za Kiislamu kwa kumuongoza mke na kuwalea watoto na wale wote waliochini ya mamlaka yake katika mipaka ya Ucha-Mungu kwa kuwaamrisha kutenda mema na kuwakataza maovu. Pamoja na jitihada hiyo huomba msaada wa Allah (s.w) kwa kuleta dua ifuatayo:


β€œ Mola wetu! Tupe katika wake zetu na watoto wetu yaburudishayo macho (yetu) (nyoyo zetu), na Utujaalie kuwa waongozi kwa wamchao (Mungu). (25:74)
Kwa ujumla waumini wa kweli ni wale wanaojipamba na tabia njema kama iliyoelekezwa katika Qur-an na Sunnah na hao ndio watakao stahili kuingia peponi.




                   


Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 1146

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰2 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰4 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰5 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Elimu Yenye Manufaa

Kwenye kipengele hiki tutajifunza elimu yenye manufaa kwenye jamii na pia tutajifunza sifa za elimu yenye manufaa.

Soma Zaidi...
Athari za kumuamini mwenyezi Mungu katika maisha ya kila siku

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Kwa namna gani nabii Musa na Bi Mariam waliweza kuzungumza na Allah nyuma ya pazia

Nabii Musa na Mama yake nabii Isa bi Mariam waliweza kuwasiliana na Allah nyuma ya pazia.

Soma Zaidi...
Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu

Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu Ni upi? (EDK form 1: mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu)

Soma Zaidi...
Mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu

Ni upi mgawanyo sahihi wa elimu katika uislamu? Nini naana ya elimu ya muongizo. Je elimu ya mazingiravmaana yakeni nini. Ni upi utofauti wa elimu ya muongozo na elimu ya mazingira?

Soma Zaidi...