image

KUAMINI MALAIKA WA ALLAH (S.W.)

KUAMINI MALAIKA WA ALLAH (S.W.)

KUAMINI MALAIKA WA ALLAH (S.W.)




Malaika ni nani?


Malaika ni katika waja na viumbe wa Allah(SW) walioumbwa kutokana na nuru. Tunafahamishwa katika hadithi ifuatayo kuwa:
Aysha (r.a.) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w.) amesema: Malaika wameumbwa na nuru na majini wameumbwa kutokana na ndimi za moto na Adamu ameumbwa kwa udongo kama ilivyoelezwa kwenu (katika Qur’an). (Muslim)Na katika Qur’an tukufu, Allah(SW) anatubainishia kuwa, katika maumbile yao halisi, malaika ni viumbe wenye mbawa.


“Sifa zote njema ni za Allah, Muumba wa mbingu na ardhi. Aliyewafanya malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbili-mbili, na tatu tatu, na nne nne. Huzid is ha katika kuumba apendavyo. Bila shaka ni mwenye uweza juu ya kila kitu”. (35:1)
Je malaika wanaishi wapi?Katika Qur,an tunafahamishwa kuwa Malaika wanayo makazi maalumu lakini si hapa duniani. Allah(SW) anawanukuu malaika wakisema:Hakuna yoyote miongoni mwetu ila anapo mahali pake mahususi. Na kwa yakini katika sisi wapo wajipangao safu. Na wako katika sisi wamtukuzao(Mwenyezi Mungu)(3 7:1 64-1 66)
Kutokana na kazi zao, Malaika wengi tunaishi nao humu hum u duniani na wako nasi muda wote.Kila mtu ana malaika wawili wenye kuandika amali zake.


Hakika juu yenu kuna wenye kuwatunza, malaika watukufu wenye kuandika. Wanayajua yote mnayoyatenda(82:1 0-12)
Aidha, tunafahamishwa katika Qur,an kuwa kila mmoja wetu ana kundi la malaika mbele na nyuma yake.Ana (kila mtu) kundi (la malaika) mbele yake na nyuma yake. Wanam linda kw a amri ya Mw enyezi Mungu. (13 :11)


Kwanini hatuwaoni Malaika?



Pengine mtu aweza akauliza kuwa kama tumezungukwa na malaika mbele na nyuma, kulia na kushoto, kwanini basi hatuwaoni? Jibu ni kwamba, mwanadamu yupo kwenye mtihani. Mtihani wenyewe ni kufanya mema kwa kutaraji malipo ya Allah(SW) na kuacha maovu kwa kuogopa adhabu zake.



Ametukuka yule ambaye Mkononi mwake umo ufalme(w ote); naye ni mwenye uw eza juu ya kila kitu. Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni; ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Naye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha(67:1-2)Malaika ndio wasimamizi wa mtihani huu, na wamefanywa wasionekane machoni petu ili kila mtu atumie uhuru wake wa ama kumuogopa Allah(SW) kwa kutenda mema au kumkufuru Allah(SW) kwa kumuasi. Lau malaika wangelionekana, watu wengi wangelitenda mema kinafiki(ria) badala ya kufanya kwa ikhilaswi.
Mfano wake, ingekuwa kama vile watu wenye dhamira za kufanya uhalifu wanavyojidai watu wema pale wanapokuwepo askari waliovalia rasmi. Utendaji kazi wa malaika ni kama mashushushu au askari kanzu. Mtu muovu anapanga na kutenda maovu akidhani yupo peke yake, kumbe malaika wapo wanaandika. Na ndiyo maana muovu atakapoona kila jambo lake limerikodiwa, atashangaa siku ya kiama kuwa alijulikanaje?


Na madaftari yatawekwa mbele yao. Utawaona wabaya wanayaogopa kwasababu ya yale yaliyomo; na watasema: “Ole wetu! Namna gani madaftari haya! Ha lia ch i dogo w ala ku bw a ila yam e lidh ib iti.Na watakuta yote yale w aliyoyafanya yamehudhuria hapo; na Mola wako hamdhulumu yeyote(18:49)
Siku mtu atakapowaona malaikaKuna siku na muda maalumu ambapo kila mtu binafsi ataanza kuwaona malaika katika umbile lao halisi.


(a) Siku ya kukata roho


Hii ni siku na saa ambayo dakika chache baada ya hapo mtu hukata roho na kuiaga dunia. Kwa watu wema, watakuja malaika wa kuwaliwaza: Hao huwateremkia Malaika “msigope wala msihuzunike, na furahini kwa pepo mliyokuwa mkia hid iwa. Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya
dunia na (huku) katika Akhera ”.(41 :30-32)
Watu wanaotenda maovu watapata mshituko mkubwa na kujawa na huzuni kubwa mno pale watakapowaona Malaika. Watasikitika sana kwa jinsi walivyokuwa wakijidanganya nafsi zao, wakatenda maovu kwa kudhania kuwa hakuna Malaika wanaorekodi matendo yao waliyokuwa wakiyafanya hadharani na mafichoni. Watafadhaika na kusema:


....Mola wangu! Nirudishe(duniani). Ili nifanye mema sasa badala ya yale niliyoyaacha. (Malaika watamwambia): “Hapana! Hakika hili ni neno tu analosema yeye(mtu muovu)....(23:99-100)
(b) Siku ya kiyama
Kuanzia pale mtu anapowaona malaika hakutakuwa tena na kizuizi cha kutowaona kama ilivyokuwa hapa duniani. Kuonekana Malaika siku ya kiama itakuwa ni ishara mbaya kwa watu waovu kuwa umeshafika wakati wa wao kuhukumiwa naAllah(s.w) na kuanza kutumikia adhabu za kudumu katika Moto wa Jahannam. Qur’an inatufahamisha kuwa:


Siku w atakayow aona Malaika haitakuw a furaha siku hiyo kwa wenye makosa; na watasema:“(Mungu) atuepushie mbali adhabu hii iliyotukabili(lakini haitawafaa kitu dua hiyo)(25:22)
(c) Motoni na Peponi
Malaika watahudhuria katika uwanja wa hukumu siku ya Kiyama. Kila mtu atawaona wamejipanga safu wakisubiri amri ya Mwenyezi Mungu.Siku ambayo zitasimama Roho na Malaika safu safu; hatasema siku hiyo ila yule ambaye(Allah) Mwingi wa rehema amempa idhini, na atasema yaliyo sawa(78:38)
Wakipewa amri na Allah(s.w) malaika watawakamata waovu na kuwachungachunga kuelekea motoni kuadhibiwa.



Na waliokufuru watapelekwa katika Jahannam m akundi m akundi mpaka w atakapoifikia; itafunguliw a milango yake; w alinzi w ake(malaika) w ataw aambia: Je! haw akukujieni Mitum e m iongoni mw enu w akikusom eeni aya za Mola w enu na kukuonyeni juu ya makutano ya siku yenu hii(39: 71)
Watu wema watasindikizwa na malaika mpaka kwenye pep o tukufu, na malaika wa huko watawakaribisha.


Na w alinzi wake (mala ika) watawaambia: Amani juu yenu, furahini, na ingieni humu mkae milele(39:73)




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 964


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Dalili za kuwepo mwenyezi Mungu
Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

NGUZO ZA IMANI
Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:1 Kumuamini Allah (s. Soma Zaidi...

Kutopupia dunia
"Ewe mwanangu! Soma Zaidi...

Mgawanyiko wa Elimu kwa mtazamo wa kikafiri
Kwa mtazamo wa kikafiri elimu imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Elimu ya dunia na Elimu ya akhera. Soma Zaidi...

(c)Vipawa vya Mwanaadamu
Vipawa vya mwanaadamu ni sababu nyingine inayomfanya mwanaadamu asiweze kuishi bila ya kufuata dini moja au nyingine. Soma Zaidi...

Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu
Nguzo za imani (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu Soma Zaidi...

Mtazamo wa Uislamu juu ya maana ya dini
Uislamu unaitazama dini katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Hii ni tofauti na mtazamo wa kikafiri juu ya dini. Soma Zaidi...

maana ya dini
Soma Zaidi...

Kwanini Uislamu umeipa Elimu nafasi ya kwanza?
Soma Zaidi...

Mtazamo wa uislamu juu ya Elimu, nini maana ya elimu na nani aliye elimika.
Ni nini maana ya Elimu na ni nani aliye elimika? Uislamu una mtazamo gani juu ya Elimu? Soma Zaidi...

Upeo wa Elimu waliyokuwa nayo Mitume
Soma Zaidi...

Neema za Allah(s.w) Juu ya Bani Israil
Katika Qur'an tunakumbushwa neema mbali mbali walizotunukiwa Bani Israil (Mayahudi) na Mola wao ili kuwawezesha kusimamisha Ufalme wa Allah(s. Soma Zaidi...