KOTLIN somo la 5: operator na aina zake kwenye Kotlin
Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu operator na aina zake.
Operator hizi ni alama ambazo hutumika katika kufanya matendo mbalimbali kwenye variable ama thamani mbalimbali. Mfano 10 + 5, katika mfano huu 10 na 5 huitwa operand na hiyo alama ya kujumlisha (+) huitwa operator.
Kwenye Kotlin operator zimegawanyika kama:-
- Arthmetics operator
- Assignment operator
- Comparison operator
- Logical operator
Arithmetics operator:
Hizi ni operator ambazo hufanya kazi kwenye matendo ya kihesabu.
- Kujumlisha (+) mfano 5 +8
- Kutoa (-) mfano 7 -5
- Muzidisha (*) mfano 2 *3
- Kugawanya (/) mafno 6 /3
- Modulus (%) hii huonyesha namba inayobaki wakati wa kugawanya mfano 10%3 hapo jibu ni 1, kwa kuwa ndio inayobaki
- Increment (++) hii huongeza namba 1 kwenye namba ya mwanzo.
Mfano:
fun main() {
var a = 2
++a
print(a)
}
Hapa jibu ni 3 kwa kuwa imeongeza 1 kwenye namba ya mwanzo.
- Decrement (- -) hi hupunguza 1 kwenye namba ya mwanzo.
Mfano:
fun main() {
var a = 3
--a
print(a)
}
Hapo jibu ni 2 kwa kuwa imepunguza 1 mwenye namba ya mwanzo.
Assignment operator:
Hizi ni zile operator ambazo hutumika ku assign thamani kwenye variable, yaani kuipa variable thamani. Kama unaposema var x = 2 hapo assignment operator (=) imetumika kuipa x thamani yake.
Mifano ya assignment operator:-
- Alama ya (=) mfano a = 3
- Alama ya (+=) mfano a += 3 hii ni sawa na kuandika a = a+3
- Alama ya (-=) mfano a -=3 hii ni sawa na kuandika a = a-3
- Alama ya (*=) mfano a *=3 hii ni sawa na kundika a = a *3
- Alama ya (/=) mfano a /=3 hii ni sawa na kuandika a = a/3
- Alama ya (%=) mfano a %3 hii ni sawa na kuandika a = a %3
Comparison operator:
Hizi ni operator ambazo hutumika katika kulinganisha yhamani mbali...
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 web hosting 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Kotlin somo la 24: Dhana ya Module katika kotlin
Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu dhana ya module. Hata ivyo tutakwenda kuisoma zaidi kwenye android App
Soma Zaidi...Kotlin somo la 22: Package kenye kotlin
Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu nadharia ya package, kazi zake, aina zake na jinsi zinavyotumika
Soma Zaidi...KOTLIN somo la 10: Jinsi ya kutumia while loop na do while loop
Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu while loop na do while loop zinavyofanya kazi katika Kotlin.
Soma Zaidi...KOTLIN somo la 8: Jinsi ya kutumia when
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu when case na jinsi inavyofanya kazi kwenye Kotlin.
Soma Zaidi...KOTLIN somo la 11:Jinsi ya kutumia break na continue kwenye loop
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu break na continue kwenye Kotlin loop za for loop na while loop.
Soma Zaidi...Kotlin somo la 23: Utofauti wa package na library
Katika somo hili utakwenda kujifunza tofauti wa library na package
Soma Zaidi...