Katika somo hili utakwenda kujifunza tofauti wa library na package
Package ni njia ya kupangilia (organize) files/classes/functions katika kundi moja la mantiki ndani ya project.
Ni sehemu ya ndani ya code yako.
Inaonyesha wapi file fulani lipo, kama folder.
Haijitegemei peke yake – ni sehemu ya project nzima.
Haitolewi kama “file la kutumia” bali hutumika kwa ku-import ndani ya code nyingine.
package com.bongolite.utils
fun greet() = println("Hi!")
Library ni mkusanyiko wa code (mara nyingi tayari imeandikwa), ambao unaweza kutumiwa na projects tofauti. Inaweza kuwa na classes/functions nyingi, mara nyingi zimepakiwa kama
.jar
,.aar
, au.klib
.
Ni kitu cha kutumia tena (reusable)
Inaweza kuwa na packages nyingi ndani yake
Unaiweka kwenye project yako kupitia dependency (kama Gradle)
Unaweza kutumia library hata kama hujaandika hata package moja ndani ya project yako
implementation("com.squareup.retrofit2:retrofit:2.9.0")
Kisha unaweza kutumia:
import retrofit2.Retrofit