KOTLIN somo la 12: Jinsi ya kupata user input
Jinsi ya kuchukuwa user input kwenye Kotlin kwa ajili ya kuongeza user interaction kwenye program.
User input ni nini?
User input ni kila ambacho mtumaji wa hiyo program atatakiwa kuwasilisha kwenye hiyo program mfano akiulizwa jina, akiulizwa namba na vinginevyo. Endapo atajaza hizo taaifa ndio zinaitwa user input. Kwa ufupi taarifa ambazo unahitaji mtumiaji wa program ajaze kwenye hiyo program ndio huitwa user input.
Katika Kotlin ili tuweze kupata user input tutatumia method ya readLine(), wacha tuone jinsi inavyoweza kufanya kazi:-
Mfano:
fun main() {
println("Andika jina kisha bofya Enter kwenye keyboard yako");
var name = readLine();
println("Jina lako ni ${name}")
}
Sasa kuna kitu nataka ujijuwe, ni kuwa user input zote ni string data type. Hivyo kama ukitaka kuweka data type kwenye kutengeneza variable utatakiwa kubadili string kuwa hiyo type ya data unayoitaka
Mfano:
Tunataka kutengeneza program ya kujuwa umri wa mtu. Program hii itahitaji mwaka aliozaliwa. Akishaweka mwaka aliozaliwa tutachukuwa 2023 - huo mwaka ili tupata idadi ya miaka yeke.
Sasa hapa kwanza tutabadilisha tada tulioipata kutoka kwenye readLine() kuwa namba. Wacha tutumie int. Hapa tutatumia function ya readLine()?.toInt() zingatia hapo tumeweka alama ya ?. hiyo hapo inaitwa self call operator hutumika kwa ajili ya ku tumia properties za object.
fun main() {
println("andika mwaka uliozaliwa")
var umri = readLine()?.toInt()
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 web hosting 👉4 ai web app 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
KOTLIN somo la 2: sheria na kanuni za uandishi wa code za Kotlin
Katika somo hili unakwenda kujifunza kuhusu sheria na kanuni za undishi wa code za Kotlin yaani syntax za kotlin.
Soma Zaidi...Kotlin somo la 24: Dhana ya Module katika kotlin
Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu dhana ya module. Hata ivyo tutakwenda kuisoma zaidi kwenye android App
Soma Zaidi...KOTLIN somo la 18: string na method zinazotumika kwenye list data type.
Katika somo hili tutajifunza method zinazofanya kazi kwenye list data type kwenye Kotlin.
Soma Zaidi...KOTLIN somo la 8: Jinsi ya kutumia when
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu when case na jinsi inavyofanya kazi kwenye Kotlin.
Soma Zaidi...KOTLIN somo la 20: method na properties za map
Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu method ambazo hutumika kwenye map data type
Soma Zaidi...KOTLIN somo la 5: operator na aina zake kwenye Kotlin
Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu operator na aina zake.
Soma Zaidi...