Katika soomo hili utakwenda kujifunza kuhusu class, maana yake, na jinsi ya kuitengeneza
Katika somo hili, utajifunza:
Maana ya class
katika Kotlin
Sababu za kutumia class
Sheria za uandishi wa class
Jinsi ya kuunda class yenye attributes
Jinsi ya kuandika methods ndani ya class
Mifano halisi na maelezo ya object creation
Katika Kotlin, class
ni msingi wa Object-Oriented Programming (OOP). Class ni blueprint au prototype ya kuunda vitu halisi vinavyoitwa objects. Class huweza kuwa na properties (sifa) na methods (tabia) ambazo zinahusiana na object.
Fikiria unataka kushughulika na data za magari mbalimbali. Kila gari lina sifa kama jina, rangi, na kasi. Kama utatumia variables peke yake bila class, code itakuwa ngumu kudhibiti. Class inakupa njia ya kupangilia vitu hivyo kuwa kama kitu kimoja kilicho na maana.
Katika Kotlin, class huandikwa kwa kutumia neno kuu class
likifuatiwa na jina la class:
class Gari {
// hapa ndani unaweka properties na methods
}
Class inaweza kuwa tupu kama hujaweka kitu ndani:
class Mbwa
Kotlin hutumia constructor kuanzisha property za class. Constructor ni sehemu maalum ya class inayochukua thamani za awali wakati object inapoundwa.
class Mbwa(val aina: String, val umri: Int)
Katika mfano huu:
val aina
ni property inayoonyesha aina ya mbwa
val umri
ni property ya umri wa mbwa
Object ni mfano halisi wa class. Tunatumia keyword val
au var
kuunda object mpya.
val mbwa1 = Mbwa("German Shepherd", 5)
println("Aina: ${mbwa1.aina}, Umri: ${mbwa1.umri}")
Method ni function iliyo ndani ya class. Hii inawakilisha tabia ya object.
class Mwanafunzi(val jina: String, val umri: Int) {
fun jitambulishe(): String {
return "Jina langu ni">
...Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu dhana ya module. Hata ivyo tutakwenda kuisoma zaidi kwenye android App
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza maana na features za object oriented Programming
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu operator na aina zake.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu set data type pamoja na method ambazo hufanya kazi kwenye set.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu when case na jinsi inavyofanya kazi kwenye Kotlin.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kuingia ndani zaidi kwenye somo la function. Hapa tutakwenda kuona aina za function.
Soma Zaidi...Jinsi ya kuchukuwa user input kwenye Kotlin kwa ajili ya kuongeza user interaction kwenye program.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu break na continue kwenye Kotlin loop za for loop na while loop.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza jinsi ya kushughulika na string kwenye Kotlin.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu historia ya Kotlin pamoja na kazi za kotlin. Pia utakwenda kujifunza kuhusu uhusiano wake na java.
Soma Zaidi...