Katika somo hili tutajifunza kuhusu method za String zinazotumika kwenye Kotlin.
Method ni nini?
Method ni kama function, lakini tofauti ni kuwa method zina uhusiano mkubwa na object. Hapa nitakuletea baadhi ya method za String:-
String length
Hii hutumika kujuwa je, string ina herufi ngapi.
fun main() {
val text = "haloo bongoclass"
println(text.length)
}
Hii itakupa jibu 16, kumaanisha hapo kuna herufi (character) 16.
Kubadili herufi kuwa ndogo au kubwa
Kubadilisha kuwa herufi ndogo utatumia toLowerCase na kubadilisha kuwa kubwa utatumia toUpperCase.
fun main() {
val text1 = "haloo bongoclass"
val text2 = "HALOO BONGOCLASS"
println(text1.toUpperCase())
println(text2.toLowerCase())
}
HALOO BONGOCLASS
haloo bongoclass
Kuigawa string kwenye (substring)
Kwa mfano, katika neno "bongoclass," tunataka kuchapisha neno "bongo" tu.
fun main() {
val text = "bongoclass"
println(text.substring(0, 5))
}
bongo
Kuchuja string (contains)
Kwa mfano, unahitaji kuangalia kama neno fulani lipo au halipo kwenye string.
Kama lipo, utapata jibu true, na kama halipo, jibu ni false. Wacha tuangalie je neno "class" lipo kwenye neno "bongoclass"?
fun main() {
val text = "bongoclass"
println(text.contains("class"))
}
true
Kubadili string kuwa list data type (split)
Hapa tutakwenda kuigawa string kwenye mafungu. Kwa mfano, neno "haloo karibu bongo class." Tutagawa kwa kila neno.
fun main(">...
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza maana na features za object oriented Programming
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu set data type pamoja na method ambazo hufanya kazi kwenye set.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza tofauti wa library na package
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kuzungumzia kuhusu parameter kwenye Kotlin function. Pia tutakwenda kuona mambo mengine yanayohusu function
Soma Zaidi...Katika somo hili unakwenda kujifunza kuhusu sheria na kanuni za undishi wa code za Kotlin yaani syntax za kotlin.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu when case na jinsi inavyofanya kazi kwenye Kotlin.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu dhana ya module. Hata ivyo tutakwenda kuisoma zaidi kwenye android App
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu while loop na do while loop zinavyofanya kazi katika Kotlin.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu historia ya Kotlin pamoja na kazi za kotlin. Pia utakwenda kujifunza kuhusu uhusiano wake na java.
Soma Zaidi...Katika soomo hili utakwenda kujifunza kuhusu class, maana yake, na jinsi ya kuitengeneza
Soma Zaidi...