Katika somo hili utakwend akujifunza maana ya function, jinsi ya kuandika function na kuweka parameter kwenye function
Function ni nini?
Function ni kifungu cha code (block of code) ambacho hufanya kazi maalumu. Function inaweza kufanya kazi kwa kujirudia rudia bila ya kikomo kila itakapoitwa. Function husaidia kutokurudiarudia kuandika code.
Mambo ya kuzingatia:
Jinsi ya kuandika function
fun name (){
Code
}
Kwanza utaanza keyword fun kisha utaweka jina la hiyo function (name yaani jina la hiyo function), kisha utaweka mabano () ndani ya haya mabano tutakuja kuweka parameter. Kisha utaweka mabano {} ndani ya haya mabano ndipo utaweka code ambazo unataka zifanye kazi. Wacha tuone mifano huwenda ukaelewa zaidi:-
Mfano 1:
Tunatengeneza program ya kuandika neno bongoclass mara 10. Kwanza tuatatengeneza hiyo fnction ambayo ita print nrno bongoclass
fun main() {
fun bongo() {
print("Bongoclass")
}
}
Kisha tutaiita (call) hiyo funcyion kwenye main().
fun main() {
fun bongo() {
print("Bongoclass")
}
bongo()
}
Sasa kama tutaiita mara 10 itaprint hilo neno mara 10
fun main() {
fun bongo() {
println("Bongoclass")
}
for (x in 1..10) {
bongo()
}
}
Jinsi ya kuweka parameter kwenye function
Tuchukulie mfano kama huu wa mwanzo. Tunataka mtumiaji aweze kuandika mwenyewe anataka neno bongoclass litokee mara ngapi. Kwa mfano akitaka litokee mara 6 ataandika 6 kwenye user input kisha function yetu itafanya kazi husika.
Sasa katika hali hiyo tutahitaji kuweka variable ambayo itawakilisha hiyo 6 atakayowekamtu. Hiyo variable ndio parameter kwa mfano tutaiita idadi. Na hiyo namba 6 atakayoinginza mtu huitwa argument. Kwa ufup tunasema parameter ni jina ila argument ni value yenyewe.
Unapoweka parameter zingatia kuweka na aina ya data ambayo hiyo parameter inakwenda kutumia. Kwa mfano kama parameter itabeba namba tunatweka Int kama ni string tutaweka String unaweza kurejea aina za data. Sasa kuweka aina ya data kwana utaana za alama ya (:) kisha utaruka nafasi moja kisha utaandika aina ya data. Angalia hapo chini.
fun main() {
fun bongo(idadi: Int) {
for (x in 0 until idadi) {
println("Bongoclass")
}
}
println("ANDIKA IDADI")
val idadi = readLine()?.toInt()
bongo(idadi !!)
}
Ukicheki hizo code kuna alama ya (!!) hiyo huitwa double-bang operator au not-null operator. Hii hutumika kuieleza kompyuta kuwa hizo data sio tupu yaani notnull. Hivyo kama ni tupu utapata error. Ni vyema kutumia if kutest kama ni null nini kifanyike tofauti na kuleta error.
fun main() {
fun bongo(idadi: Int) {
println("Bongoclass")
}
println("ANDIKA IDADI")
val idadi = readLine()?.toIntOrNull()
if (idadi != null) {
bongo(idadi)
} else {
println("Invalid input. Please enter a valid number.")
}
}
Function yenye parameter zaidi ya moja.
Parameter zinaweza kuwa zaidi ya moja. Wacha tuone mfano mwingine wa kujumlisha namba mbili. Hapa sitatumia user input. Tutaweka wenyewe namba hizo. Kwa mfano tutaweka 5 na 7 ili program izijumlishe. Ikiwa parameter ni zaidi ya moja zote utatenganisha kwa alama ya koma ( , ).
fun jumlisha(x: Int, y: Int) {
println(x + y)
}
fun main() {
jumlisha(5, 6)
}
Ngoja tutengeneze program ya calculator ambapo itakuwa na parameter 3, ya kwanz ani namba ya kwanza, ya pili ni tendo la hesabu na ya tatu ni namba ya tatu.
Kwa kutumia if
fun jumlisha(x: Int, y: String, z: Int): Int {
val result: Int
if (y == "+") {
result = x + z
} else if (y == "-") {
result = x - z
} else if (y == "*") {
result = x * z
} else if (y == "/") {
result = x / z
} else {
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowKatika somo hili unakwenda kujifunza kuhusu sheria na kanuni za undishi wa code za Kotlin yaani syntax za kotlin.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu namna ambavyo program inaweza kufanya maamuzi kulingana na mashart fulani.ama namna ambavyo program inaweza ku run code zaii ya mara moja kulingana na mashart. Hapa tutazingumzia flow of control statement
Soma Zaidi...Katika somo hili tutajifunza method zinazofanya kazi kwenye list data type kwenye Kotlin.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutajifunza kuhusu method za String zinazotumika kwenye Kotlin.
Soma Zaidi...Jinsi ya kuchukuwa user input kwenye Kotlin kwa ajili ya kuongeza user interaction kwenye program.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu method ambazo hutumika kwenye map data type
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu aina za data zinazotumika kwenye Kotlin.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu set data type pamoja na method ambazo hufanya kazi kwenye set.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza jinsi ya kushughulika na string kwenye Kotlin.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu when case na jinsi inavyofanya kazi kwenye Kotlin.
Soma Zaidi...