Unapokuwa na kizunguzungu unashindwa kuudhibiti mwili wako, unaweza kuanguka kabisa.
Unapokuwa na kizunguzungu unashindwa kuudhibiti mwili wako, unaweza kuanguka kabisa. Kizunguzungu kinaweza kuwa ni dalili ya tatizo flani kwenye afya ya mtu. Maradhi mengi yanahusiana na kizunguzungu, hivyo baada ya huduma ya kwanza na mgonjwa akawa hajambo ni vyema aende kituo cha afya akajuwe chanzo cha kizunguzungu:
Mtu mwenye kizunguzungu anaweza kujipa huduma ya kwanza mwenyewe. Vinginevyo anaweza pia kupata maelekezo kutoka kwa mtu aliye karibu naye kwani siku zote mgonjwa anakosa uwezo wa kujimilikia\ hasa kujipa huduma ya kwanza.
1.Kwanza mwenye kizunguzungu anatakiwa akae chini
2.Kama alikuwa akitembea ama alikuwa akifanya shuhuli yeyote anatakiwa aache na akae chini kabisa na wala asichchumae.
3.Akaechini kipolepole na katu asiharakishe
4.Kama kukaa chini hakutoshi ni vyema alale, kama anaona kama dunia inazunguka asilale kichalichali.
5.Kama anakiu mpe maji ya kutosha anywe
6.Akae sehemu iliyotuia, isiyo na fujo wala mwanga mkali wa taa ama jua
7.Ni vyema kama atapata usingizi walau kidogo
8.Kizunguzungu kikiondoka kwanza akae chini kipolepole na anapotaka kusimama asimame kipolepole na katu asitumie kitu ili kimsaidie kusimama kama fimbo
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi malengo ya kutibu ukoma, ni malengo ambayo yamewekwa na wizara ya afya ili kuweza kutokomeza ukoma kwenye jamii
Soma Zaidi...Posti hii inahusu kazi ya chanjo ya kifua kikuu kwa kitaalamu huitwa BCG. Ni chanjo ambayo uzuia kifua kikuu na ukoma.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mbinu za kuondoa sumu mwilini, ni njia mbalimbali ambazo uweza kutumika ili kuondoa sumu mwilini.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria kwa kitaalamu huitwa vibrio cholera.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyuko
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa ovari kwenye mwili wa mwanamke. ovari ni sehemu ambapo mayai ya mwanamke hutunza, kwa hiyo kila mwanamke huwa na ovari ambayo husaidia kutunza mayai.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo mbalimbali ambayo husababisha kizunguzungu.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi njia za kuenea kwa ugonjwa wa Ukimwi. Ukimwi ni upungufu wa kinga mwilini.
Soma Zaidi...