Kifafa hakiambukizi na ugonjwa wa ubongo lakini kifafa pia hakiathiri akili au ubongo Ila kikiwa kifafa Cha kudumu na Cha nguvu ndio huweza kuadhiri. Pia Kuna kifafa Cha mimba na kifafa Cha kawaida.kifafa Cha mimba ndio kinahatari Sana kuliko Cha Kawaid
Dalili za kifafa
Kifafa kina dalili ambazo huonekana na mtu ukiziangalia unajua kuwa Ni mojawapo ya kifafa na dalili hizo Ni pamoja na;
1.mwenye kifafa lazima ataonyesha dalili ya kupoteza fahamu ; yaani hawezi kusikia,hawezi kuona, hawezi kusikia maumivu kwa huo muda yaani hatakuwa na ushirikiano wowote ule (unresponsive).
2.lazima atupe au kurusha rusha mikono na miguu,pamoja na kichwa kukigeuza geuza na huo muda mauvu anakuwa hasikii kabisa.
3.kuchanganyikiwa kwa mda
4.mate yenye mchanganyiko wa mapovu kutoka Mdomoni kwa huo muda aliopata kifafa( udenda)
5. Mwenye dalili za kifafa huwa anaduwaa kipindi kifafa kinamtokea.
Sababu za kifafa
1.kurithi; kifafa huweza Kurithi kutoka kizazi hadi kizazi.
2.magonjwa ya kuambukiza Kama vile ukimwi,au uti wa mgongo huweza kusababisha kifafa.
3.madhara kwenye ubongo; Kama vile maji kujaa kwenye ubongo, uvimbe kwenye ubongo, bacteria na virusi vinavyoshambilia ubongo husababisha kifafa pia.
4. Kichwa kuumia (head injury) mfano ukipata ajali ya kichwa pia husababisha kifafa.
Huduma ya kwanza kwa mwenye kifafa
Kifafa huweza kutibiwa nyumbani na kupona Kama hakijawa sugu au ikiwa Ni kifafa kilichopo na huwa mnamfanyia huduma ya kwanza anapona , namna ya kumpatia huduma ya kwanza kwa mwenye kifafa;
1.hakikisha sehemu aliyoangukia Ni Safi na Haina vitu vya kumuumiza ili anapopata fahamu asiwe na maumivu ya kuchomwa na kitu .
2.mgeuze mgonjwa alale upande (kiubavu) ili akicheua,akimeza mate au kutapika asipate shida maana yanaweza kurudi kwenye Koo la hewa na kumsababishia shida nyingine au yanaweza kumkaba.
3.mwekee kitu kilaini kwenye kichwa ili awe vizuri (comfortable).
4.mkague Kama amevaa hereni,cheni,au kitu kinachoweza kumuumiza umtoe .
5.mwache mgonjwa apate hewa watu wasimzunguke maana anaweza akakosa hewa.
6.usimzuie mgonjwa kurusha miguu na mikono hauruhusiwi kumshika mwache arushe akipata fahamu ataacha.
7. Usimpatie au kuweka chochote Mdomoni mwake Mana anawaze kutapika, kukabwa, au kurudi kwenye Koo la hewa na kupaliwa.
8.kaa na mgonjwa mapaka atakaporudi katika Hali yake na umuangalie yupo katika Hali gani Kama Ni mzuri au mbaya.
9kama mgonjwa Yuko katika Hali mbaya Sana au amechuku muda mrefu zaidj ya lisaa limoja haja pata fahamu fanya mipango sasa ya kumpeleka hospitali kwaajili ya matibabu .
Mwisho; Kama mgonjwa wa kifafa ndio Mara yake ya kwanza au ameanguka akachukua mda mrefu na Kama ana Hali ya kifafa na hajawahi kwenda hospitalini kwaajili ya uchunguzi Ni vyema kumpeleka akafanyiwe uchunguzi na vipimi na ushauri zaidi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi mabadiliko katika umri wa kubarehe kwa wsichana, ni kipindi ambacho watoto huelekea ujana, utokea Kati ya miaka kuanzia Kumi na kuendelea.
Soma Zaidi...Maziwa ni mojakati ya vinywaji ambavyo ni dawa na hutumikakutoa huduma ya kwanza pale mtu anapomeza ama kula sumu. Huduma ya kwanza hii inaweza kuokoa maisha na wakati mwingine inaweza kuwa ndio dawa kabisa wala hakuna haja ya kufika Kituo cha afya.
Soma Zaidi...Maumivu ya shingo ni malalamiko ya kawaida. Misuli ya shingo inaweza kuchujwa kutokana na mkao mbaya - iwe inaegemea kwenye kompyuta yako kazini au kuwinda benchi yako ya kazi nyumbani.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi vifaa vya kutumia wakati wa kusafisha vidonda, ni vifaa muhimu ambavyo mara nyingi kutwa hospitalini.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ya chakula kushindwa kumengenywa vizuri tumboni, haya ni madhara ambayo utokea kwa sababu ya chakula kushindwa kumengenywa vizuri tumboni.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mgawanyo wa matibabu ya kifua kikuu, tunajua kubwa kifua kikuu ni Ugonjwa ambao utumia mda mrefu kidogo katika matibabu kwa hiyo mgawanyiko wake uko kwenye sehemu mbili muhimu kama tutajavyoona
Soma Zaidi...