Jinsi macho yanavyoweza kuzungumza kuhusu afya yako ya kimwili na kiakili

Jinsi macho yanavyoweza kuzungumza kuhusu afya yako ya kimwili na kiakili

MACHO YANAFAFANUA KUHUSU AFYA:


Macho ya mwanadamu yanaweza kuwa ni malango wa kufahamu afya ya mtu kiakili na kimwili. Kupitia macho p[olisi na wapelelezi wanaweza kufahamu mhalifu ni nani. Kupitia macho daktari anaweza kufahamu matatizo kadhaa katika afya ya mtu. Makala hii itakwenda kukufahamisha ni kwa namna gani macho yako yanaweza kuweka wazi kuhusu afya yako. Hapa tutakwenda kuona macho katika nyanja hizi:-
A.Umbo
B.Rangi
C.Michubuko
D.Na kama kuna vinyama vilivyoota kwenye macho.



Baada ya kusoma makala hii utaweza kufanya uchunguzi kuhusu afya yako wewe mwenyewe kabla hujakwenda hospitali. Unaweza kutumia kioo ama mtu aliye karibu nawe. Makala hii sio kipimo cha mwisho, hakikisha kuwa majibu kuhusu afya yako utayapata kwa daktari.



1.Mzunguruko wa macho. Kama kwenye mzunguko wa macho yako kwa nje kuna uvimbe hii inaweza kuashiria kuwa mtu huyu atakuwa anasumbuliwa na aleji. Pia inaweza kuwa ama infection (mashambulizi ya bakteria) kwenye machi yake. Hali hii pia inaweza kuashiria matatizo kwenye figo. Hali hii inaweza kuandamana na dalili kama macho kuwa mekundu, miwasho kwenye macho, kuvimba kwa macho. Daktari ataweza kupima mkojo wako ili kupata taarifa juu ya afya ya figo.


2.Kope; kope inaweza kuwa ni kioo cha kuonyesha afya ya mtu. Kama kwenye maoteo ya kupe kuna rangi nyekundu huashiria kuwa huwenda mtu anasumbuliwa na ugonjwa wa naemia (upungufu wa damu). dalili kuu ya ugonjwa huu ni kupauka kwa ngozi ya ndani ya kope. Kama mtu atashindwa kufunga na kufunguwa kope zake vyema itaweza kuashiria shida kwenye mfumo wa neva.



3.Mijongeo ya macho; misuli inayotumika katika mijongeo ya macho, (kwenda kulia, kushoto, juu na chini) ina mahusiano moja kwa moja na mfumo wa neva yaani mfumo wa fahamu hivyo kuwa na mahusiano ya moja kwa moja na ubongo. Sasa endapo mfumo wa fahamu na ubongo utakuwa na matatizo huweza kuathiri misuli hii na kusababisha mtu ,ushindwa kujongesha macho yake kwa ufasaha. Kwa mfamo mtu anaweza kushindwa kupeleka jicho lakoe upande mmoja kama wa kulia ama kushoto.



4.Mahala lilipo jicho lako; jicho lipo kwenye sehemu yake maalumu na linafiti vyema hapo. Sasa wakati mwingine jicho la mtu unaweza kuliona kama limeingia ndani sana ama wengine utaliona limetokeza nje sana. Sasa endapo mtu anasumbuliwa na upungufu wa maji mwilini utakuta macho yeke yameingia ndani. Na endapo macho yake yametokeza nje sana huwenda mtu uyu anasumbuliwa na shida ya tezi ya thyroid.



5.Mboni ya jicho lako; Mara nyingi utaona madaktari wanamulika jicho lako. Kinachoangaliwa ni namna ambavyo mboni ya jicho lako itafanya nini baada ya kumulikwa. Kikawaida mboni inatanuka na kusinyaa kulingana na mwanga ulioifikia. Hivyo endapo jicho lako litashindwa kufanya haya itaonyesha shida kwenye mfumo wa fahamu unaoungana kwenye macho.



6.Ndani ya jicho lako; ndani ya jicho kuzungukia hilo jiduara jeupe unalolioa ambalo ndio jicho kuna vimishipa vingi sana vya damu vimelishikilia. Kwa watu wenye hali mbaya ya shinikizo la juu la damu na wale wenye kisukari huweza kuathiri jisho na kusababisha uoni hafifu. Kufanya uchunguzi wa kina juu ya swala hili kunahitaji ujuzi zaidia, wakati mwingine datkari hutumua kimiminika maalumu ili kulegeza jicho. Dakatari ataweza kuchunguza zadi mpaka sehemu yenye makutano ya neva zinazopelekea taarifa kwenye ubongo



Kama kutakuwa na presha kubwa kwenye fuvu huwenda kutokana na stoke, uvimbe wa ubongo ama maradhi mengine, sehemu ya makutano ya mishipa ya neva (disc) kutakuwa na rangi ya mpaiko na vijimishipa vya damu vitakuwa na rangi ya utofauti.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Huduma Main: Afya File: Download PDF Views 1341

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

Huduma ya kwanza kwa mwenye jeraha linalotoa damu

Posti inahusu huduma ya kwanza kwa mwenye jeraha linalotoa damu.huduma ya kwanza Ni kumsaidia mtu alie pata jeraha au ajali kabla hajamwona dactari au kufika hospitalinia.

Soma Zaidi...
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATA JOTO LA JUU ZAIDI (HEAT STROKE)

Hii ni hali inayotokea ambapo wili unakuwa na joto la juu sana tofauti na kawaida.

Soma Zaidi...
Kuboresha afya

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mambo yanayosaidia kuboresha afya

Soma Zaidi...
Mkojo wa kawaida

Posti hii inahusu zaidi mkojo wa kawaida kwa kila mwanadamu na unavyopaswakuwa, mkojo wa kawaida kwa binadamu huwa na sifa zifuatazo.

Soma Zaidi...
Utaratibu wa lishe kwa vijana

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu utaratibu wa lishe kwa vijana

Soma Zaidi...
Namna ya kumfanyia usafi Mgonjwa kwa mwili mzima.

Posti hii inahusu namna ya kumfanyia mgonjwa usafi mwili mzima, ni njia ambazo utumika kumfanyia mgonjwa usafi mwili mzima au kumwosha Mgonjwa hasa wale walio mahututi na hawawezi kuamka kitandani.

Soma Zaidi...
Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu

Soma Zaidi...
Aina za kuungua

Post hii inahusu Aina za kuungua, kuungua ni Hali ya kubabuka kwa ngozi ya mwili na kusababisha madhara mbalimbali

Soma Zaidi...
Makundi manne ya damu na jinsi yanavyotumika

Post hii inahusu zaidi umuhimu wa makundi manne ya damu na jinsi yanavyotumika, Ni magroup manne ya damu ambayo husaidia kuongeza damu kwa mtu ambaye amepungukiwa damu

Soma Zaidi...
Huduma ya Kwanza kwa aliyeungua

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa aliyeungua

Soma Zaidi...