image

JAVASCRIPT - somo la 15: Jinsi ya kukusanya user input

Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu user input. Somo hili litaangalia html form na attribute zake na jinsi zinavyohusiana na user input. Mwisho wa somo hili utaweza kutengeneza simple Calculator kwa kutumia javascript.

User input ni nini? 

Tunasema user input tunaangalia taarifa ambazo mtumiaji ataziinguza kwenye system kwa ajili ya kukamilisha ufanyajivwakazi ama kwa ajili ya kuoatavout put fulani. 

 

Hivyo basi hapa tunazungumzia user interaction yaani muingiliano wake na hiyo system. 

 

Mfano wa uzee input ni kama unapojisajili,  ama unapojaza madodoso kwenye mitandao. Hata unapoandika meseji ama unapo upload faili hizo zote ni user input. 

 

Njia ambazo mtumiaji ataweka input kwenye javascript program. 

Zipo njia kadhaa ambazo utatumia ili kuweka input kwenye javascript program. Kwa mfano: -

  1. Kwa kutumia prompt() function

  2. Kwa kutumia html form

  3. Kwa kutumia batani

Katika somo hili tutakwenda kuzitumia njia zote hizo tatu. 

 

  1. Kwa kutumia prompt()

Hii ni javascript finction ambayo hutumika pale ambapo mtumiaji anatakiwa kuweka input. 

 

Function hii inabeba parameta 2 ambazo ni,  string na default. Kwenye string mtumiaji atajaza hicho anachotakiwa kujaza. Sasa unaweza kuweka defaul yaani unaijaza kwanza. Ili endapo mtumiaji hatajaza basi value ulizojaza wewe zitumike. 

 

Hiyo string hapo hutumika kama ile placeholder kwenye html form. Hapo unaweza kuandika je ni nini mtumiaje ajaze. 

 

Hiyo parameter ya default sio ya lazima. Inamaana unaweza kuiwacha .

 

Mfano 1:

<script>

  let h = prompt("Jina");

  document.write("Haloo"+ " "+ h);

</script>

Hapo sijatumia default. Sasa wacha tuone jinsi default inavyifanya kazi. Kwenye default mtumiaji atakuta tayari pameshajazwa hivyo ataamuwa abadili aweke majibu yake ama aache hivyo hivyo. 

 

 Mfano 2:

<script>

  let h = prompt("Jina", "Bongoclass");

  document.write("Haloo"+ " "+ h);

</script>

Kwa kutumia prompt pia tunaweza kufanya mahesabu. Kwa mfano tunaweza kutumia function ya eval() tulisha jifunza hapo awali. Unaweza kuingiza hesabu na kukupatia majibu. 

 

Mfano 3:

<script>

  let namba = prompt("weka hesabu");

  document.write("Jibu ni:-"+ " "+ eval(namba));

</script>

Sasa endapo mtumiaji hatajaza kitu basibitakupa majibu indefined. Angalia mfano hapo chini

 

Mfano 4: 

 

Kwa ufupi hivyo ndivyo tunavyoweza kuingiza usiwe input kwa kutumia javascript. Baada ya hapo utaweza kuzifanyia kazi hizo input kwa namna unavyotaka.

 

2.Kwa kutumia batani

Batani inaweza kutumika ku input data kwenye element za html. Kwa mfano kwenye paragraph, kwenye section element kama div, na kwenye textarea na zaidi ya hapo. 

 

Ili kuweza kupata data zilizopo kwenye batani tutatumia finction ndani ya batani. Kisha tutapata thamani ama input kwa kutumia .value ili kupata id ya hiyo batani tutatumia .id na ili kupata name attribute tutatumia .name na kujua type ya hiyo batani utatumia .type.  Wacha tuone mifano. 

 

Katika mfano wa hapo chini. Nimeweka maneno haloo Bongoclass kwenye batani kama value. Sasa tunataka kuyaingiza maneno hayo kwenye textarea element. Hivyo basi kwanza tutatengeneza function ya ambayo tutakwenda kwenye onclick event. Function yetu tutaiita myFunc. Kisha tutatengeneza variable kwa ajili ya kuwakilisha value yetu. 

 

Mfano 5:

<title>User input</title>

<textarea id="demo" name="txt"></textarea>

<br><button id="btn" name="myBtn" onclick="myFnc()" value="Haloo Bongoclass" type="submit">Bofya</button>

 

<script>

  function myFnc(){

    var btnId = document.getElementById("btn").value;

    

    document.getElementById("demo").innerHTML = btnId;

  }

</script>

 

...



Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: JavaScript Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 222


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

JAVASCRIPT - somo la 11: function maalumu zinazotumika kwenye string yaani string method
Katika somo hili utakwenda kujifunza baadhi ya function maaumu zinazotumika kwenye string yaani string method. Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 3: sheria za uandishi wa code za javascript yaani syntax za javascript
Katika somo hili utakwenda kujifunza sheria ama syntax za kuandika javascript. Hii itakuwezesha kuelwa zaidi code za javascript. Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 2: Jisi ya ku print output ya code za javascript.
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ambavyo utaweza ku display matokeo ya code za javascript. Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 20 Jinsi ya kutumia foOfloop kwenye javascript
Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutumia forOfLoop. Hii ni aina ya loop ambayo yenyewe inahusisha item zote kwenye array. Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 22: Jinsi ya ku set time na tarehe
Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu ku set time. Yaani tutaweka muda ambao code zinatakiwa ndio zilete matokeo. Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 10: Jinsi ya kuandika object na matumizi yake kwenye javascript
Ksomo hili litakwenda kukufundisha kuhusu object kwenye javascript, kazi zake na sheria zake katika kuiandika. Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 17: condition statement za if else, else if kwenye javascript
Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu condition statemant. Darasa hili ni moja katika madarasa muhimu programming. Katika somo hili tutajifunza kwa vitendo zaidi. Tutatumia mifano ya somo lililo tangulia. Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 9: Jinsi ya kuandika function kwenye javascript
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function kwenye javascript. Utajifunz apia namna ya kuitumia function hiyo Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 21: Jinsi ya kutumia while loop na do while loop
Katika somo hili tutakwenda kujifunza khusu while loop na do while loop. Soma Zaidi...

Game 3: Mchezo wa kufikiria namba kwa kutumia javascript
Hii ni game ambayo utafikiria namba, ambayo inatakiwa iwe sawa na namba ambayo game imeiweka. Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 6: Jinsi ya kufanya mahesabu kwenye javascript
Katika somo hili utajifunza kuhusu matendo ya hesabu ambayo ni kugawanya, kujumlisha, kuzidisha na kutoa Soma Zaidi...

JAVASCRIPT - somo la 8: Aina za data zinazotumika kwenye javascript
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu aina za data ambazo hutumika kwenye javascript Soma Zaidi...