Mtume (s.a.w) pia ametutajia dalili kubwa za kukaribia kwa siku ya Mwisho. Dalili hizo zinapatikana katika Qur’an na Hadith kama inavyobainishwa hapa chini:“Na kitakapokaribia Kiyama, tutawatolea mnyama kutoka ardhini atawaeleza (watu) kwa kuwa watu walikuwa hawaziamini aya zetu” (27:82)“Mpaka watakapofunguliwa Ya’juj na Ma’juj nao wataporomoka kwa kasi, na ikakaribia ahadi ya kweli kufunguliwa, hesabu na malipo, basi wakati huo macho ya makafiriyatatokeza mno juu ” (21:96 – 97)
Katika hadith aliyoipokea Imam Ahmad, na kusimuliwa na Khudhaifa Ibn Usaid Al – Ghifaar (r.a) amesema; Alitutokea Mtume (s.aw) kutoka chumbani kwake na sisi tukikumbushana jambo la kiyama, Mtume (s.a.w) akasema: Hakitosimama Kiyama mpaka muone alama kumi,
1. Kuchomoza jua Magharibi
2. Kutokea moshi mkubwa utakaochafua mazingira (pollution)
3. Mnyama atatokeza na kuwasemesha watu
4. Kufunguliwa Ya’juj na Ma’juj (21:96 97)
5. Kurudi kwa Issa mwana wa Maryam
6.Kuja kwa Masih Dajal (False Messayah)
7.Kutoka Moto (Volcano) katika pango la Aden ukiwaendesha watu
8.Dunia kugawika mapande matatu (Three Blocks); Pande la Mashariki (Eastern Block)
9.Pande la Magharibi na (western block)
10.Bara Arab (Mashariki ya kati - Middle East)
Kwa hakika Qur’an imetaja dalili nyingi mno, Rejea Suratul qiyaamah (75:6 – 9) na nyinginezo nyingi zilizotajwa katika hadith mbali mbali.
Kuamini siku ya mwisho ni kuamini kuwa kuna maisha ya milele baada ya maisha haya ya hapa duniani. Kwa mujibu wa mafundisho ya Qur-an, maisha hayo yatakuwa na
hatua kuu nne zifuatazo:
(i)kutokwa na roho
(ii)Maisha ya kaburini - Barzakh.
(iii)Kufufuka na kuhudhurishwa mbele ya Allah (s.w) na kuhesabiwa.
(iv)Maisha ya kukaa Peponi milele kwa watu wema au kukaa motoni kwa watu waovu.Aidha kwa kuzingatia matukio yatakayotokea katika hatua nne za maisha yajayo,
siku ya mwisho katika Quran imepewa vifuatayo:
(i)Siku ya Qiyama (21:47, 75:1, 75:6, 79: 42) Siku ya mwisho (2:4, 2:8, 58:22)
(ii)Siku ya malipo (1 :4, 82:9, 95 :7, 107:1, 83 :11) Msiba ugongao nyoyo (101:1)
(iii)Siku ya hukumu (77:13-14)Wakati maalumu (56:49-50)
(iv)Siku ya makamio (50:20)
(v)Siku ya makutano (40:15)
(vi)Siku iliyokaribu sana kufika (40:18)
(vii)Siku ya kuitana (40:32)
(vii)Siku ya kutoka makaburini (50:42)Tukio lilokaribu, limesogea
(viii)Siku zitakapotikisika mbingu mtikisiko wake 187
(ix)Siku ya kukaa daima (50:42)
(x)Siku zitakapofichuliwa siri (86:9)
(xi)Tukio la Haki (69:1-3)
(xii)Siku ya Haki (78:39)
(xiii)Tukio kubwa (56:1-2)
(xiv)Siku iliyokadiriwa (85:2)
(xv)Msiba ukumbao (88:1)
(xvi)Siku iliyokuu (83:5)
(xvii)Siku ya mkusanyiko (64:9)
(xviii)Siku ya Hisabu