image

Ni yupi mtume wa mwisho? na je ni kwa nini Muhammad ndiye mtume wa mwisho?

Ni yupi mtume wa mwisho? na je ni kwa nini Muhammad ndiye mtume wa mwisho?

Mwisho wa Utume



Maswali ambayo huweza kuulizwa ni: Kwa nini wahyi ukatike? Kwa nini Mitume wasiendelee kuletwa hadi kiyama? Kwa nini Muhammad (s.a.w) afunge mlango wa Utume?
Ili kulielewa vizuri suala hili la mwisho wa Utume yafaa kwanza tuzingatie kuwa kilicho muhimu na cha msingi kabisa kwa Mtume yeyote si kule kuwepo kimwili bali ni kule kuufikisha kwake ujumbe aliopewa na Mwenyezi Mungu (s.w) ili watu wake wasiwe na hoja tena iwapo watachagua kupotea.


Na lau ingekuwa lililo muhimu kwa Mtume ni kule kuwapo kimwili basi Mwenyezi Mungu angelimpeleka Mtume mara tu baada ya kufariki Mtumealiyetangulia. Kilicho cha msingi ni mafundisho aliyokuja nayo. Maadamu ujumbe aliouleta uko hai basi Mtume huyo yu hai. Hivyo kifo halisi cha Mtume ni kule kupotea kwa mafundisho aliyoyaleta. Mitume wote waliomtangulia Muhammad (s.a.w) mafundisho yao yalipotea, kwani yalichanganyika na hekaya mbali mbali. Katika vitabu vilivyoitangulia Qur-an, kwa mfano Taurat, Injil, na Zaburi hakuna hata kimoja ambacho kipo katika hali ya usahihi wake wa asili. Hata wafuasi wa vitabu hivyo wanakiri kuwa nakala walizonazo leo si zile walizopewa Mitume. Si hivyo tu bali hata historia za maisha ya Mitume waliomtangulia Muhammad (s.a.w) zimechanganywa na ngano za kushtusha kabisa, hata inakuwa vigumu kupambanua haki na batili.


Kinyume chake mafundisho aliyokuja nayo Muhammad (s.a.w) yako hai kabisa na hayajaharibiwa na katu hayawezi kuharibiwa. Qur-an, kitabu alichoteremshiwa kipo tena katika lugha ile ile ya asili bila ya kupunguza wala kuzidisha japo nukta moja. Historia kamili ya maisha yake, maneno yake, maagizo yake, vitendo vyake, vyote vimehifadhiwa kwa usahihi kabisa kiasi ambacho karne 14 zimepita lakini bado historia yake ni ya wazi na kamili kama kwamba tunamuona kwa macho yetu. Katika kila kipengele cha maisha yetu tunaweza kupata muongozo na mafundisho kutoka kwa Muhammad (s.a.w). hii ndio sababu hakuna haja ya kuletwa Mtume mwingine baada yake.
Zaidi ya hayo yapo mambo matatu ambayo husababisha kuhitajika kuja kwa Mtume mwengine baada ya yule aliyetangulia:



(1)Iwapo mafundisho ya Mtume aliyetangulia yamechanganywa na hekaya za nzushi, kuharibiwa na kupotea. Katika hali kama hiyo Mtume anahitajika ili aje aifundishe dini katika usahihi wake wa awali.



(2)Iwapo mafundisho ya Mtume aliyeondoka hayakukamilika na hivyo kukawa na haja ya kuyakamilisha, kuyarekebisha, au kuongeza jambo fulani.



(3)Iwapo Mtume aliyetangulia alipelekwa kwa watu wa taifa fulani maalum au nchi fulani maalum na hivyo kuwepo haja ya kuletwa Mtume kwa watu wa taifa au nchi nyingine. Au pengine Mtume anaweza kuletwa ili amsaidie Mtume mwingine, lakini kwa kuwa hii si kanuni ya kawaida, hatujaita kama sharti la nne. Katika Qur-an ipo mifano miwili ya hali kama hiyo. Nabii Haruni (a.s) alikuwa msaidizi wa Nabii Musa (a.s). Nabii Lut (a.s) Ismail (a.s) na Is-haq (a.s) walikuwa wasaidizi wa Nabii Ibrahim (a.s).
Haya matatu ndiyo masharti makuu ya kimsingi yanayohitajika ili aletwe Mtume mwingine. Kati ya hayo hakuna hata sharti moja lililopo leo. Kwanza mafundisho ya Mtume wa mwisho, Muhammad (s.a.w) yako hai, yamehifadhiwa na yatadumu hadi siku ya Kiyama. Mwongozo aliouleta kwa walimwengu wote ni sahihi na kamili na umehifadhiwa katika Qur-an humo kuna ahadi ya ulinzi wa Allah (s.w) kama tunavyofahamishwa:


“Hakika sisi ndio tulioteremsha mawaidha (haya hii Qur-an); na Hakika sisi ndio tutakaoyalinda.” (15:9).
Pia sunnah zake zimehifadhiwa kikamilifu kiasi ambacho mtu anaweza kujua pasi na shaka yoyote nini mafundisho ya Mtume juu ya jambo fulani. Hivyo sharti la kwanza linaondoka.
Pili, Mwenyezi Mungu amekamilisha mwongozo wake kwa Nabii Muhammad (s.a.w) na hivyo Uislamu ni dini kamilifu kwa ulimwengu wote. Allah (s.w) anasema katika Qur-an:


“… Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kukutimizieni neema yangu juu yangu na nim ekupendeleeni Uis lam u uw e dini yenu … (5:3)




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1072


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Njia anazotumia Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu
Njia ambazo Allah hutumia kuwasiliana na wanadamu nakuwafundisha elimu mbalimbali. (Edk form 1 dhana ya Elimu) Soma Zaidi...

Kina Cha uovu wa shirk
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mitume waliosimuliwa katika Qur-an ni hawa ishirini na tano (25) wafuatao:
Adam (a. Soma Zaidi...

Mtazamo wa makafiri juu ya dini
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Muhtasari wa sifa za waumini
Lengo tarajiwa la Muhtasari huu ni kutuwezesha kuzibaini fika sifa za Waumini zilizoainishwa katika Qur'an, kisha kujipamba nazo ili tuwe waja wema watakaorehemewa na kuridhiwa na Allah (s. Soma Zaidi...

Uchambuzi wa Neema Alizopewa Nabii Sulaiman(a.s)
(i) Kutiishiwa Upepo Qur'an inatufahamisha kuwa Nabii Sulaiman alitiishiwa upepo akaweza kuutumia apendavyo kwa amri yake. Soma Zaidi...

Ni yupi mtume wa mwisho? na je ni kwa nini Muhammad ndiye mtume wa mwisho?
Soma Zaidi...

Athari za kumuamini mwenyezi Mungu katika maisha ya kila siku
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

NGUZO ZA IMANI
Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:1 Kumuamini Allah (s. Soma Zaidi...

Maadili na malezi ya jamii
Soma Zaidi...

Kubisha hodi katika nyakati za faragha katika familia
“Enyi mlioamini! Soma Zaidi...

Nafsi ya mwanaadamu
Soma Zaidi...