Labda itaulizwa: Kwanini Mtume Muhammad (s.
Labda itaulizwa: Kwanini Mtume Muhammad (s.a.w) awe Mtume wa walimwengu wote? Ama kuhusu suali hili, hapana jibu lolote lililotolewa katika Qur-an wala katika hadithi za Mtume (s.a.w). Hivyo ni Allah (s.w) pekee anayejua ni kwanini alimleta kwa ulimwengu mzima.
Lakini tunaweza kutumia akili zetu finyu tukajaribu kuona hikima iliyopo kwa Mtume (s.a.w) kuwa Mtume wa ulimwengu mzima jambo ambalo halikuwezekana kwa Mitume waliotangulia. Hapo awali, kabla ya Mtume (s.a.w), Mitume walikuwa wakitokea kwa kila nchi au kila taifa.
Sababu ya msingi tunayoweza kuona kirahisi ni kwamba katika wakati huo wa historia njia za usafiri na mawasiliano yalikuwa finyu sana kwa kiasi ambacho mawasiliano kati ya watu na nchi moja na nyingine yalikosekana kabisa.
Kila nchi au ukanda wa jiografia ulikuwa ni ulimwengu wa peke yake. Katika hali hii ilikuwa ni vigumu mno kuwa na Mtume mmoja kwa ulimwengu wote. Ndio tunakuta kila nchi au kila ukanda wa jiografia ukatumiwa Mtume wake.
Sote tunashuhudia kuwa katika umma huu wa mwisho wa Mtume Muhammad (s.a.w) pamekuwa na maendeleo makubwa sana ya mawasiliano kiasi kwamba dunia inakuwa kama kijiji. Suala la “Globalization” (utandawazi) kwa Waislamu sijambo geni
Tunafahamishwa katika Qur-an kuwa umma huu wa Mtume Muhammad (s.a.w) ni umma mmoja na unawajibika kuufanya Uislamu utawale ulimwengu mzima.
Kutokana na hoja hizi tatu itaonekana wazi ni kwanini hakuna haja ya Mtume mwingine baada ya Muhammad (s.a.w). Na ndivyo Allah (s.w) anavyotufahamisha katika Qur-an kuwa yeyeMuhammad (s.a.w) ni “Khataman-Nabiyyina” - yaani mwisho wa Mitu me:Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Allah na mwisho wa Mitume na Allah ni mjuzi wa kila kitu. (33:40)Na Mtume Muhammad (s.a.w) mwenyewe pia anasema:
Palikuwa na Mitume waliowaongoza Banii Israil katika njia sahihi.
Kila Mtume alipokufa, alifuatiwa na Mtume mwingine. Lakini hapana Mtume atakayekuja baada yangu. Kazi hii (ya kuufundisha Uislamu na kuusimamisha) inaweza kufanywa na makhalifa (viongozi wa Kiislamu). (Bukhari).
Na katika Hadithi nyengine Mtume (s.a.w) amesema: “Uhusiano wangu na (msururu mrefu) wa Mitume unaweza kueleweka vizuri kwa mfano wa nyumba nzuri ya kifalme. Nyumba hii ikawa imejengwa vizuri sana na ikawa inapendeza lakini pakawa na nafasi moja iliyobakia. Watu wakawa wanaizungumza nyumba hii nzuri na wakawa wanauliza kwa mshangao.Kwanini hii sehemu isiwe imejazwa! Nimejaza pengo hili na ni Mtume wa mwisho”. (Bukhari).
Umeionaje Makala hii.. ?
Ni upi mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu (EDK form 1: mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu
Soma Zaidi...Malaika wamepewa kazi ya kumtumikia Allah(SW) kwa kumtukuza na kumtakasa, kama wanavyosema wenyewe:Hakuna yoyote miongoni mwetu ila anapo mahali pake mahususi.
Soma Zaidi...Mtazamo wa uislamu kuhusu dini (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Wanapokujia wanafiki, husema: "Tunashuhudia ya kuwa kwa yakini wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Soma Zaidi...“Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana,ziko alama (hoja) za kuonyesha kuwepo Allah (s.
Soma Zaidi...Hii ni njia ambayo mwanaadamu huongeleshwa moja kwa moja na Allah (s.
Soma Zaidi...