Posti hii inaonyesha dalili,sababu na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa aliyepata jeraha kwenye ngozi kwa kuingiliwa na kitu Kama mwiba,Pini,sindano n.k
Ishara na Dalili za mwenye jeraha kwenye ngozi
1.kuwa na Maumivu.
2.kuvuja Damu sehemu iliyopata jereha.
3. Kuvimba
Vitu vinavyoweza kusababisha jeraha kwenye ngozi
1.miiba
2.vitu vyenye ncha Kali kama misumari, sindano za kushona, pini n.k.
3. Kioo cha glasi.
Mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa aliyepata jeraha kwenye ngozi
1. Osha mikono yako na safisha eneo vizuri kwa sabuni na maji.
2. Ikiwa kitu kiko ndani ya ngozi chukua sindano safi, yenye ncha kali ili kutolea Kama inawezekana
3. Inua ncha ya kitu kilichopo kwenye ngozi na ukishike kwa mkono wako
4. Finya jeraha taratibu il damu itoke na kuosha vijidudu.
5. Osha eneo hilo tena na kulikausha.
6. Tafuta usaidizi wa haraka wa matibabu Kama jeraha linaonekana kuwa kimewekwa ndani ya ngozi au misuli.
6. Usijaribu kuondoa kitu kilichoingia Ndani zaidi ya Ngozi kama huna ujuzi wa kufanya hivyo maana unaweza Kufanya hivyo kunaweza kusababisha madhara zaidi.
7. Ikiwezekana, dhibiti uvujaji wa damu kwa kukandamiza kwa nguvu ili Damu zisitoke.
8. Funga jeraha, weka kitambaa safi karibu na kidonda kabla ya kuifunga kidonda kwa bandeji au kipande cha kitambaa safi. Jihadharini usibonyeze sana kitu kilichoingia Ndani ya Ngozi.
9.mpeleke mgonjwa kituo Cha afya kwaajili ya matibabu zaidi
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu
Soma Zaidi...Mwanadamu ukifikiria vyema. Kuhusu nafsi yako, hakika utapatabfikra yabuwepp wa Mwenyezi Mungu
Soma Zaidi...(v)Kuwaombea dua wazazi.
Soma Zaidi...Elimu inaweza kugawanyika katika makundibmrngine mawili ambayo ni elimu yenye manufaa na elimubisiyi na manufaa
Soma Zaidi...Njia ambazo Allah hutumia kuwasiliana na wanadamu nakuwafundisha elimu mbalimbali. (Edk form 1 dhana ya Elimu)
Soma Zaidi...Je ni kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila ya kuwa na dini?. Vipawa alivyopewa na Allahni jibu tosha juu ya swali jilo
Soma Zaidi...