picha

Historia ya Mwanadamu

Historia ya Mwanadamu

Historia ya Mwanadamu



Historia ya mwanadamu ukiichunguza tangu mwanzo wake utakuta matukio mengi yanayothibitisha kuwepo Allah (s.w) Mmiliki wa kila kitu na mwenye nguvu na uwezo juu ya kila kitu. Mara kwa mara tunatanabahishwa katika Qur-an:“Je! Haikuwabainikia tu kama (kaumu) ngapi tuliziangamiza kabla yao? Na hawa (makafiri wa sasa) wanatembeatembea katika maskani yao, (hawaoni alama za kuangamizwa kwao)? Bila shaka katika hayo zimo ishara kwa wenye akili. ” (20:128 “Je! Haw atembei katika nchi na kuona jinsi ulivyokuw a mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Walikuwa wenye nguvu zaidi kuliko wao na wakilima ardhi na kuistawisha zaidi kuliko wao walivyostawisha. Na mitume wao waliwajia kwa dalili waziwazi, basi hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wenyewe wakijidhulumu nafsi zao.” (30:9)“Je! Huoni Mola wako alivyo wafanya watu wenye ndovu? Hakujaalia vitimbi vyao kuharibika? Na akawapeleka ndege makundi kwa makundi, wakawapiga kwa mawe ya udongo wa kuchoma, Akaw afanya kam a majani yaliyotafunw a. ” (1 05:1-5)


Tukio hili la watu wenye ndovu lilitokea mwaka 570. A.D. miezi michache kabla ya kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w).


Mnamo mwaka wa 570 A.D. Abraha, gavana wa Yemen, chini ya himaya ya Kikiristo ya Uhabeshi alikusanya jeshi lenye askari 60,000 na ndovu (tembo) kumi na tatu (13) kwa nia ya kuibomoa na kuisambaratisha Al-Ka’abah, nyumba takatifu ya Allah (s.w) iliyopo Makka.


Walinzi wa Ka’abah, kabila la Quraish waliongozwa na Abdul-Muttalib, Babu yake Mtume (s.a.w), walimfahamisha Abraha kuwa wao hawana uwezo wa kupambana na jeshi lake hilo bali mwenye Ka’abah ndiye atakayeilinda. Abraha alipokaidi na kusisitiza kutekeleza azma yake ya kuivunja Ka’abah, Abdul-Muttalib aliwaamuru wakazi wa Makka wampishe na akaingia ndani ya Ka’abah na kumuomba Allah (s.w) kwa unyenyekevu kama ifuatavyo:“O Allah, mtu hulinda nyumba yake, nawe ilinde nyumba yako.


Usiuachie msalaba na hila zao kesho kushinda hila zako. Kama utaamua kuwaachia waifanye watakavyo Qibla yetu, Basi w ewe ni muweza wa kufanya upendavyo. Wanusuru leo watumishi wako dhidi ya watumishi wa Msalaba na waabudu wake.


Ewe Mola wangu, sina matumaini yoyote toka kwa yeyote dhidi yao isipokuwa kwako. Ewe Mola wangu, ilinde nyumba yako dhidi yao. Adui wa nyumba hii ni adui yako. Wazuie w asiiharibu nyumba yako”.
Kesho yake, Abraha na jeshi lake kabla hawajapiga hatua kutoka kwenye kambi yao, kilometa tano (5) tokea Makka, walizingirwa na jeshi la ndege wadogo wadogo walioitwa “Ababil” waliokuwa na silaha ya vijiwe. Kila ndege alimlenga askari wake na kijiwe hicho kilichomchakaza na kumfanya kama majani yaliyotafunwa na kutemwa.



Tukio hili la “watu wa ndovu” ni kielelezo tosha kutokana na historia ya binaadamu kuwa Allah (s.w) yupo na anauwezo ulio juu ya hila zote za binaadamu na juu ya kila kitu.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Views 2219

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Bongolite - Game zone - Play free game     👉3 Dua za Mitume na Manabii     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zinazofanana:

Njia anazotumia Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu

Ni zipo njia wanazotumia Allah katika kuwasiliana na kuwafundisha wanadamu? (EDK form 1: Dhana ya elimu katika Uislamu).

Soma Zaidi...
Kujiepusha na kula mali ya Yatima

Waumini wanawajibika kuwatunzia mayatima mali zao na kuwakabidhi wanapofikia baleghe yao baada ya kuwajaribu na kuthibitisha kuwa wanao uwezo wa kutunza mali zao - Rejea Qur-an (4:5-6).

Soma Zaidi...
Haki za kielimu za mwanamke katika uislamu

Haki ya ElimuKatika Uislamu kujielimisha ni faradhi inayowahusu Waislamu wote, wanaume na wanawake: "Soma kwa jina ?

Soma Zaidi...
Sifa za waumini zilizotajwa katika surat As-Sajida

Nao husema (kwa maskhara): "Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya?

Soma Zaidi...